Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,318
- 8,229
Mimi maswali yangu ni haya;~
Utawala wa Magufuli unaonekana ulikuwa wa kipigaji sana, je aliwezaje
1. Kununua ndege 11 mpya tena bila mkopo?
2. Kujenga madaraja yote haya?
3. Kujenga Fly over hizi?
4. Kujenga meli kubwa mpya zile na kukarabati meli za zamani?
5. Kuhamishia serikali Dodoma na kuanza ujenzi wa Ikulu kubwa namna ile?
6. Kujenga viwanja vya ndege na kukarabati vya zamani kwa ujumla wake 13?
7. Kujenga Vituo vya Afya takriban 500 na Zahanati 1800?
8. Kujenga Hospitali za Wilaya, za rufaa na za kanda kwa kiwango kile?
9. Kusambaza umeme katika vijiji 7,000?
10. Kujenga masoko ya kimataifa ? Ukianzia Dar es salaam yako masoko kadhaa ya kimataifa, Kisutu, Magomeni, Mwananyamala, Iringa mjini, Dodoma pale soko la Ndungai.
11. Kujenga Mahakama za kisasa karibu kila mkoa?
12. Kujenga barabara za lami kila mahali mijini? Tena barabara za kiwango cha kimataifa na taa za barabarani?
13. Kujenga SGR_ Standard Gauge Railway tena yakutumia umeme?
14. Kujenga Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere?
15. Kujenga maabara za shule za kata na kuzikarabati shule zote za Sekondari Kongwe?
16. Elimu bure nchi nzima kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne?
17. Ununuzi na ufungaji wa Rada kuilinda anga ya Tanzania?
18. Kufufua Reli ya Dar es Salaam, Tanga Moshi Arusha iliyosimama kwa miaka 30?
Najiuliza aliwezaje kufanya yote haya kwa muda wa Miaka Mitano na Miezi Mitano tu? Aliwezaje kuimudu Corona na hatukupigwa Lockdown? Kwa muda wote wa uongozi wake.
Haya ndio maswali nahitaji majibu.
Mkuu wangu Zito pia mwanauchumi naomba jitokeze kuokoa hili jahazi.
Bro Lissu pia mwanasheria mkongwe mtaalamu wa sheria haya maswali yanahitaji majibu.
Mzee wangu Mbowe popote ulipo jitokeze katika huu mjadala.
Tujibu hili swali kwa weledi ili tuweze kupata walau elimu. Ni kipi kilichofanyika.
Ahsanteni kwa michango.