Kuelekea 2024/2025 tujiulize maswali kuntu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Salaam kwenu nyote.

Tujiulize haya maswali na unaweza kuongeza ya kwako. Maswali haya yanahoji uwezo wa CCM kutuvusha kama nchi kuelekea maendeleo mtambuka.

  1. KATIBA MPYA: Serikali imepora mamlaka ya wananchi kwa kukataa mchakato halali wa kupata Katiba inayoendana na wakati. Majibu ya serikali kupitia Rais ni kwamba wananchi hawana uelewa na ufahamu wa Katiba hivyo serikali inajipanga kuwarlimisha wananchi kitu wanachokitaka kwa mtazamo wa serikali. Tuwawajibishe CCM au Wapinzani?
  2. UMEME: Bado nchi ipo kwenye tatizo kubwa la umeme ambapo kila awamu ilikuja na ahadi kem kem ingawa awamu ya 5 Taifa lilianza kusahau tatizo la umeme. Leo zinatolewa kauli za ajabu ajabu kuhusu uhakika wa nishati hii. Je wawajibishwe kati ya CCM au Wapinzani?
  3. Huduma za Afya: Kauli za viongozi haziendani na uhalisia kwenye mahospitali ya umma. Bado gharama za matibabu zipo juu na wananchi hawapati huduma bora. Tumesikia malalamiko kila kona dhidi ya huduma mbovu za afya hata wananchi kupoteza maisha kizembe wawapo kwenye hospitali za umma. Watu pia wanaumizwa na biashara ya huduma za vyumba vya kuhifadhia maiti. Serikali imelenga kukusanya mapato kutoka hata kwa marehemu bila kujali uhalisia na kipato cha jamii, gharama zipo juu na huduma hazina ubora. Je tuiwajibishe CCM au Wapinzani?
  4. Mfumuko wa bei usiozingatia vipato na mzunguko wa fedha. Mamlaka za serikali hususan EWURA, TRA, LATRA n.k. zimekuwa mwiba kwa kuhakikisha inaongeza tozo na bei mbalimbali za huduma muhimu kwa jamii. Upandaji wa nishati ya mafuta haulingani na bei ya soko la dunia. Upandaji wa nauli za usafirishaji wa watu na mizigo hauzingatii asilimia za mfumuko wa bei. Inafika mahala LATRA wanawaza upatikanaji wa chenji badala ya kuset viwango vinavyoendana na kipato cha Mtanzania. Kupandisha nauli kwa zaidi ya asilimia 30 ni pigo kwa jamii inayopambana kukua kwa uchumi. Je tuiwajibishe CCM au Wapinzani?
  5. UFISADI: Serikali imekuwa inapokea ripoti za CAG na haizifanyii kazi, yaani kuchukua hatua kurekebisha kasoro zilizoanikwa. Imekuwa ni kama tunatimiza matakwa ya wafadhili ya kujikagua kisha nothing is happening. Je ni CCM au Wapinzani tuwawajibishe?
Hoja mufilisi zinazotolewa na watetezi wa mfumo dhalimu ni kwamba, tukiiondoa CCM tumpe nani nchi?

watanzania tufahamu kwamba nchi ya Tanzania haitokaa ifutike tukiiondoa CCM madarakani. Pia nchi itapata kiongozi Mtanzania atakayeunda serikali.

Serikali ya CCM imezuia serikali mseto. Lakini mazingira ya sasa yanahitaji serikali mseto ambayo haihitaji vyama kuungana kabla ya uchaguzi
 
Hakuna mbadala wa CCM Katika nchi hii.CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kuongoza Taifa letu na kutuvusha katika kila hatua kutupeleka nchi ya ahadi itiririshayo asali na maziwa.
 
Hakuna mbadala wa CCM Katika nchi hii.CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kuongoza Taifa letu na kutuvusha katika kila hatua kutupeleka nchi ya ahadi itiririshayo asali na maziwa.
Imetuvusha wapi mpaka sasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom