CAG abaini ufisadi nyumba ya gavana BOT

Mwe
Hivi siku zote Gavana alikuwa anaishi wapi? leo mnamjengea nyumba mpya na kusahau walimu wangu na wauguzi kule vijijini......

Mkuu hujui kuwa:
1- Gavana ndiye guardian wa EPA - na anahitajika.

2 - hao walimu na wauguzi wako si wa muhimu kwao, hata kura zao hawazihitaji?
 
Mkuu hujui kuwa:
1- Gavana ndiye guardian wa EPA - na anahitajika.

2 - hao walimu na wauguzi wako si wa muhimu kwao, hata kura zao hawazihitaji?

Ukiangalia pia Gavana ni mtanzania mmoja, wauguzi, walimu na wafanyakazi ni 300,000 sijui ratio ikoje hapa anyway JK alisema haihitaji kura za wafanyakazi labda ana kura zake tayari.
 
Huko peke yako mkuu sometimes najiuliza maswali mpaka naona kama nachanganyikiwa nashindwa kuamini kama BOT hakuna wajuzi au wahandisi makini. Na kama ni hivyo basi wanatangaza nini wanahitaji first class degree kuwapa ajira!!!!

Tatizo hapa, Mkuu ni huko kwa CAG walikoandika hiyo ripoti. Kwa ripoti hii, hakuna anayekamatwa!

Amandla....
 
Katika procurement methods za construction projects kuna hii ya kuweka fixed price......yaani client analipa pesa Fulani na mjenzi anakula hasara ikiwa pesa ya ujenzi imekuwa kubwa kuliko aliyoitarajia au kupata faida kubwa Kama gharama zitakuwa ndogo.

Project managers wa BOT either si wajenzi by profession na wakashindwa kufanya makadirio ya gharama na kuidhinisha pesa nyingi hivyo au kuna mtu kafanya kwa kusudi ale pesa na mjenzi

nafikiri ingekuwa bora kulipa kwa mujibu wa matumizi na kuweka faida ya mjenzi fixed
 
dah nataman kuwa mchawi tu yaani ningewatengeneza woote kwa sababu naona njia ya kawaida haifai as long as watawala wenye mamlka wameamua kupiga kimya juu ya ili.
yani ningewaloga wao na nyumba zao ningezijaza mamba na kenge na maji kibao km mafuriko vile !!!!!!!!!!!!
ahhh we wajenga nyumba ya gharama na anasa km ivyo wkt watu wanakufa uko ata sh kumi ya panadol hawana then we wajenga anasa watu wenyewe matumbo makuuuuuuuuuuuuuuuubwa ata kuogelea hawawezi....dah yan wananiboa awa wanyama .yeeeess wanyama tu cz hawana sense of humanity .
 
Dr.. Slaaa anza kuweka kumbu kumbu za kufanyia kazi pindi utakapo APISHWA....
 
Hiyo ni kweli Samson but tujiulize kwanini hakuna action inamaana it goes down kwamba system nzima imeoza ndio maana watu hawaoni ajabu watu kufanya ufisadi. Now ndio naona umuhimu wa mtu kama Dr Slaa kwani anaweza kuleta mabadiliko ijapokuwa bado nina shaka na baadhi ya wajumbe wa chadema (mfano marando na mbowe) but at least ni time kubadilisha uongozi kwani hakuna utawala wa sheria tanzania sasa hivi.
Kwa nini hakuna action ni kwa sababu JK anayo PHD ya msikitini haifanyi kazi ya ukweli na walioiba ni watu wake wa karibu. hana usemi kudadeki keshakula limbwata huyo.
 
leo kuna gazeti (sikumbuki ni lipi) limeandika kuwa CAG na Zitto Kabwe wametetea gharama zilizotumika kujenga nyumba ya Gavana (na msaidizi wake) kuwa sahihi kwa kuwa zinaendana na hadhi ya nyumba hizo na waliojengewa. Sasa nikabaki kujiuliza CAG si ndiye huyu aliongea kuhusu kutokuwepo upembuzi yakinifu wa gharama za mradi na kusababisha kutofuatwa kwa taratibu za kupunguza matumizi ya mradi??
 
Gharama nyumba ya Gavana halali - Utouh
Na Joseph Mwendapole
6th August 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ametetea gharama za ujenzi wa nyumba mbili za Gavana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilizofikia Sh. bilioni tatu, na kusema Watanzania hawapaswi kushangazwa na hali hiyo.

Pia Utoah ametetea ujenzi wa majengo pacha ya BoT, kwa madai kuwa yanakidhi matumizi ya muda mrefu.

Utouh alisema pamoja na thamani hiyo kuonekana kubwa, lakini kama nyumba hizo zitauzwa hivi sasa kwa bei ya soko, thamani yake itafikia Sh bilioni 5.7.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wadau wa ukaguzi wa hesabu ulioandaliwa na ofisi yake.

Alisema uchunguzi uliofanywa na ofisi yake ulibaini kwamba hapakuwa na matumizi mabaya katika ujenzi wa nyumba hizo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Alisema umaskini wa Watanzania hauwezi kusababisha nyumba za viongozi zikajengwa kwa viwango vya chini na kuongeza kuwa, kuna Watanzania ambao wana nyumba zinazozidi thamani ya nyumba hizo.

Utouh alisema nyumba hizo zina manufaa kwa umma kutokana na ukweli kwamba si mali binafsi, hivyo zitaendelea kumilikiwa na serikali na zitatumiwa na magavana na manaibu wao kwa miaka yote.

“Zile nyumba sio za watu binafsi, wanaokaa mle ni watumishi wa serikali na mtu yeyote anayeteuliwa kuwa na wadhifa wa ugavana au naibu gavana ataishi mle, ina maana, mnataka kwa kuwa nchi ni maskini viongozi waishi kwenye vijumba vibovu,” alihoji.

Aliongeza: “Hata majengo pacha ya BoT, watu waliyashupalia wakidai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma, hivi mnataka kila baada ya miaka kumi tujenge majengo ya Benki Kuu?

“Kwani mnadhani yale majengo ni ya Gavana, yale majengo ni ya Watanzania hivyo hakuna kibaya kilichofanyika kuyajenga na yamejengwa kwa matumizi ya muda mrefu,” alisema.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) aliyemaliza muda wake, Zitto Kabwe, alisema Gavana ni mtu mkubwa anayeshikilia uchumi wa nchi, hivyo anapaswa kuishi sehemu yenye usalama zaidi.

Alisema kulikuwa na ulazima wa kujenga nyumba za viwango hivyo, kwa kuwa makazi aliyokuwa amepangiwa yaliligharimu taifa fedha nyingi. Zitto alisema gharama iliyokuwa ikitumika kulipia pango la gavana kwa miaka miwili linafikia kiasi kilichotumika kujengea nyumba hizo.

CHANZO: NIPASHE

Mtazamo: Hapa ndio napochoka na nchi yetu mtu anaandika report inasema lengine yeye anaenda kuyazungumza mengine. Ukiangalia wanachotetea ni argument kuwa gavana anastahili kuwa nyumba nzuri (which hakuna mtu anayepinga hilo) but is it justifiable kwa gavana kuishi katika nyumba ya gharama kubwa kama hiyo. Kama ni ndio je vipaumbele vya nchi ni vipi? Tatu wanaposema gharama ni justifiable (in relative to what? Wameshafanya comparison na nyumba za magavana wengineo duniani wakatupa vigezo vya kuwa gharama zile ni justifiable?). Mbona tunafanyana wajinga????
 
asante Mdondoaji, I was puzzled this morning when I heard the contradicting statement made by the CAG, hiyo ripoti ya mwanzo ni yake kweli? aliandikiw atu na hakuisoma?? na mbona sasa yamtokayo ni tofauti na aliyoripoti?? Hapo sasa hata kama ulitaka kujiaminisha ndo una ahirish akabisa maana wameshanitia mashaka.
 
asante Mdondoaji, I was puzzled this morning when I heard the contradicting statement made by the CAG, hiyo ripoti ya mwanzo ni yake kweli? aliandikiw atu na hakuisoma?? na mbona sasa yamtokayo ni tofauti na aliyoripoti?? Hapo sasa hata kama ulitaka kujiaminisha ndo una ahirish akabisa maana wameshanitia mashaka.

Fanta unajua nchi kwetu kuna visa kweli. Zitto anasema kuwa gharama za ujenzi ni nafuu kuliko pale mwanzo walipokuwa wanampangishia but kuna ulazima gani kwanza gavana akapewa nyumba (niliwahi kusema mwanzoni kuwa hii culture ya kupeana nyumba inabidi iishe kwani si nzuri ndio inaencourage ufisadi kwanini wasipewe allowance ya nyumba au wakaruhusiwa kukopa nyumba serikali ikasubsidies part of the payment (mfano gavana analipa 75% serikali inamsaidia 25%)). Sasa kupangishiwa nyumba ya gharama nalo ni swali jengine kwanini amepangishiwa nyumba ya gharama kubwa? Wakati wenzetu wanasave pesa wasiaibike sie Tanzania tunatumia na kukopa sijui tutafika wapi kwakweli.
 
Alisema kulikuwa na ulazima wa kujenga nyumba za viwango hivyo, kwa kuwa makazi aliyokuwa amepangiwa yaliligharimu taifa fedha nyingi. Zitto alisema gharama iliyokuwa ikitumika kulipia pango la gavana kwa miaka miwili linafikia kiasi kilichotumika kujengea nyumba hizo.

Kaka Zitto,
Hii gharama kubwa ya pango imelinganishwa na nini mpaka ikaonekana kubwa?ni kiasi gani kwani?huyu gavana hawezi kukaa nyumba sawa na waziri au na wao ni kama yeye wanaishi nyumba za 2bn(x63???)...ngumu kidogo kuamini hii kitu...
 
Ndio maana nilisema hapo awali kuwa ile ripoti ilikaa kisanii. Hakuna mtu anayebisha kuwa wakuu hawa na ofisi hizi zinatakiwa kuwa na majengo mazuri na salama. Lakini tunachojiuliza ni kuwa tumepata value kwa fedha zetu? Kweli kuna ulazima wa nyumba za viongozi wetu kuwa na swimming pool? Swimming pool hiyo inaongezea vipi usalama wake? wanavyotuambia kuwa majengo hayo yatadumu kwa muda mrafu, wana uhakika na wanachokisema? Gharama kubwa imeingia kwenye finishes na installations ambazo shelf-life yake ni fupi sana. Kwa mfano, hizo security systems zinabidi ziwe updated kila mara ili ziende na wakati. Hizi ni gharama tutakazozibeba. Na kwa wale wanaojua, yale majengo ki-usanii hayana sifa yeyote! Ni majengo mabaya mno yanayotuvutia sisi malimbukeni peke yetu. Inatia kichefu chefu.

Amandla.....
 
CAG, yeye anaangalia ankra kama ziko sawa---check and Balance na wala si mhakiki wa nyendo za ruswa na ufisadi... Serikali imejiuzia nyumba (MKAPA TIME), KIKWETE yeye anajenga nyumba.... Zile nyumba walijiuzia kwa bei chee, sasa uliza nyumba za viongozi zinazojengwa gharama zake upate Blood pressure.

CCM wameleta umaskini mkubwa sana baada ya Nyerere.

CHAGUA CHADEMA, CHAGUA SLAA, its a sign of VICTORY''
 
Maswali ya kujiuliza ni haya:
Kwanza, Nyumba alizokuwa anakaa za kuopangisha kwanini ziwe expensive hivyo? Hawezi kukaa nyumba ya Mil 5 or less kwa mwezi?
Pili, hizo nyumba zilizojengwa zina value for money, yani ya 500 au 600 isingemfaa?
Tatu, kazi ya CAG ni pamoja na kufanya value for money audit, ameifanya au anakokotoa mahesabu tu?
Bilioni 3.2?
BOT kazi ipo bado.
 
Hiyo valuation ya kuwa zina thamani ya 5.7 bilioni imefanywa na nani? Usanii mtupu!

Amandla.......
 
Ndio maana nilisema hapo awali kuwa ile ripoti ilikaa kisanii. Hakuna mtu anayebisha kuwa wakuu hawa na ofisi hizi zinatakiwa kuwa na majengo mazuri na salama. Lakini tunachojiuliza ni kuwa tumepata value kwa fedha zetu? Kweli kuna ulazima wa nyumba za viongozi wetu kuwa na swimming pool? Swimming pool hiyo inaongezea vipi usalama wake? wanavyotuambia kuwa majengo hayo yatadumu kwa muda mrafu, wana uhakika na wanachokisema? Gharama kubwa imeingia kwenye finishes na installations ambazo shelf-life yake ni fupi sana. Kwa mfano, hizo security systems zinabidi ziwe updated kila mara ili ziende na wakati. Hizi ni gharama tutakazozibeba. Na kwa wale wanaojua, yale majengo ki-usanii hayana sifa yeyote! Ni majengo mabaya mno yanayotuvutia sisi malimbukeni peke yetu. Inatia kichefu chefu.

Amandla.....

Mkuu thanks nilitaka kuuliza swali hilo hilo je Gavana ana umuhimu gani wa kuwa na swimming pool kwani asiende kujiandikisha umember pale collesium Gym pale masaki akawa anaogelea kila siku kama yeye ni mpenzi kweli wa kuogelea au ni muhimu kwa usalama wake. Sijaona uhusiano hapa naomba kueleweshwa!!!
 
Mkuu thanks nilitaka kuuliza swali hilo hilo je Gavana ana umuhimu gani wa kuwa na swimming pool kwani asiende kujiandikisha umember pale collesium Gym pale masaki akawa anaogelea kila siku kama yeye ni mpenzi kweli wa kuogelea au ni muhimu kwa usalama wake. Sijaona uhusiano hapa naomba kueleweshwa!!!

Swimming pool ni fesheni. Ni accessory na wala sio ya matumizi. Ni bling bling. Wengi wenye nazo hata mpango wa kuogelea hawana na hawataruhusu wake zao na mabinti zao kuvaa nguo za kuogelea. Lakini kwa vile Ikulu iko basi kila kiongozi anataka.

Kinachofanyika hapa ni kufanya Swimming Pool na hayo maupuuzi mengine ( sakafu za marble, isecurity systems n.k.)l kuwa ni sehemu ya mahitaji ya nyumba za viongozi wa juu, CAG akiwemo. Sasa tungeje nyumba zao zitakapokarabatiwa ili zifikie hivyo viwango vilivyowekwa na BOT. Halafu tunashangaa vibaka wanavyokuwa hawana huruma?

Amandla.....
 
By PIUS RUGONZIBWA, 5th August 2010 @ 16:00,
DAILY NEWS

THE Controller and Auditor General (CAG) on Thursday defended the decision by the Bank of Tanzania (BoT) to build two residential houses for its top officials for 3.2bn/-.

The CAG, Mr Ludovick Uttoh, clarified that there was no misappropriation of funds in the construction of the two houses and some sections of the media wrongly reported that the cost was 5.7bn/-.

"The market price for the two houses is estimated at 5.7bn/- and that is not the construction cost," Mr Uttouh told a news conference on an audit conducted on the construction of the two houses.

He was briefing the reporters on the report by his office shortly after it was submitted to the Parliamentary Committee for Parastatals Organizations Accounts (POAC). "We want to make it clear that the cost stated in the construction of the two houses is genuine.

"The only anomaly was in the procurement procedures where some 35m/- were dubiously spent," noted the CAG. The CAG said 35m/- which was dubiously spent had to be recovered by the bank.

Mr Utouh further said it was wise for the government to build good and durable houses for its top officials in sensitive government institutions like the Central Bank.

He said it was more expensive to keep such officials in hotels or rented houses where the bank could be spending 3.2bn/- on rent for just two years.

"These two houses will accommodate these officials for more than 100 years.. How much rent would have to be paid during that period? After all, those houses are public property and big assets as well," he stressed.

The POAC Chairman, Mr Zitto Kabwe, said he was satisfied with findings of the CAG report and insisted there were no misappropriation of funds as reported by some sections of the media.

"The BoT governor is an important public figure. He or she is entitled to maximum security," he said.

Meanwhile, lack of board of directors in many of public institutions has been cited as the cause for the organisations' failure to publish their accounts reports as required by the law.

The CAG said some of public institutions have been failing to prepare and submit their financial statements for audits within the required time, citing the example of about ten which completely failed to submit 2008/2009 accounts by February, this year.

The CAG was speaking shortly after the opening of the two days stakeholders' forum on the challenges in the audit of public authorities and other bodies which started in the Dar es Salaam on Thursday.

Opening the Forum, the Chief Secretary, Mr Philemon Luhanjo, said auditors must maintain their crucial role in ensuring financial statements were prepared in accordance with relevant reporting standards.

He said the government was satisfied with the performance of the National Audit Office under the CAG, and that it will do whatever possible to enhance its capacity.


MY OPINION: Mafisadi watateteana kwa kila hali. Wakati wanafunzi chungu nzima nchini hawana madawati, hawana walimu, hawana madarasa, mahospitali yetu hayana vitanda, madawa na vifaa muhimu bado wakuu wa nchi hawaoni tatizo la Governor wa BoT kuishi katika jumba la shilingi 1.4 billioni!!!! Hivi aneishi katika nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 300 au hata mia 400 hadhi yake kama governor wa BoT ingeshuka?

Bado tuna safari ndefu sana ya kupambana na mafisadi ambao wamejaa katika sehemu mbali mbali nchini hata ofisi ya CAG.
 
Back
Top Bottom