CAG abaini ufisadi nyumba ya gavana BOT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG abaini ufisadi nyumba ya gavana BOT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Aug 4, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 03 August 2010

  Sadick Mtulya na Salim Said

  BENKI Kuu (BoT) ilikiuka sheria na kanuni za manunuzi ya umma pamoja na mkataba wa makubaliano ya mradi wa ujenzi wa nyumba za Gavana Benno Ndulu na mmoja wa manaibu wake zilizo Masaki jijini Dar es Salaam, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza.

  Mwananchi ilikuwa ya kwanza kuripoti ubadhirifu huo wa fedha za umma mwaka jana ilipoeleza kuwa BoT ilitumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba ya gavana na manaibu wake watatu, lakini Prof Ndulu akatoa ufafanuzi haraka kuwa nyumba hizo hazikukarabatiwa bali zilijengwa upya kwa gharama ya Sh1.27 kila moja.


  Lakini, ripoti mpya ya CAG imeonyesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia uzabuni wa mradi huo na kusababisha gharama zake kupanda.

  Ripoti hiyo inasema kuwa baadhi ya huduma za majengo hayo na mabwawa ya kuogelea hayakuwamo katika mahitaji ya msingi ya mradi na kwamba yalipendekezwa na mshauri.

  Ripoti hiyo iliyotolewa Julai, mwaka huu na kusainiwa na CAG Ludovick Utouh imeeleza kwamba kama
  BoT ingefuata taratibu za manunuzi pamoja na mkataba, gharama ya mradi isingefikia kiwango hicho.

  "Kutokana na mazingira hayo, nahitimisha kwamba, japokuwa maamuzi ya mradi yalikuwa sahihi, menejimenti ya BoT haikufuata taratibu ambazo zingeweza kupunguza gharama za mradi huo," inasema ripoti hiyo.


  Ukaguzi huo ulifanyika baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) kuagiza kufanyika kwa uchunguzi huo wa tuhuma za taasisi hiyo kuu ya fedha nchini kufanya ubadhirifu katika ujenzi wa nyumba hizo. POAC ilitoa agizo hilo Januari 21 mwaka huu katika mkutano wake na Gavana Ndulu.


  Ripoti hiyo imefafanua kuwa bodi ya wakurugenzi wa BoT, Juni 28, 2008, ilithibitisha na kupitisha Sh 1,478,136,184.54 kwa ujenzi wa nyumba iliyo Mtaa wa Mtwara, kiwanja namba 57, lakini baada ya kukamilika gharama zilifikia Sh1,517,821,819.95.

  Gharama za nyumba iliyo Mtaa wa Tumbawe kiwanja nambari 12, zilipitishwa kuwa Sh1,330,965,114.90, lakini baada ya kukamilika gharama zilifikia Sh1,407,655,434.75.

  Hata hivyo, ripoti imeweka wazi mchanganuo wa awali ulionyesha gharama zote za majengo hayo na malipo ya mshauri, ingefikia Sh3.2 bilioni lakini, uthamini uliofanyika unaonyesha kwamba, thamani ya nyumba iliyopo Mtaa wa Mtwara ni Sh2.8 bilioni na ile ya Tumbawe Sh2.9 bilioni.

  "Na kufanya gharama zote za mradi kuwa Sh5.7 bilioni,''
  inaeleza taarifa hiyo.

  Ripoti inaeleza kuwa hakukuwa na upembuzi yakinifu uliofanyika kwa mradi huo, hivyo gharama za ujenzi katika hatua ya kubuni, haikukadiriwa.


  Kuhusu hoja ya mchakato wa manunuzi kama uliendana na Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPA) ya 2004 na kanuni zake, ripoti hiyo ilibainisha kuwa mchakato huo una mapungufu kadhaa yanayokiuka sheria hiyo.


  "Njia iliyotumika kumchagua mshauri ilibanwa na haikuwa na ushindani kama kanuni ya 34(1) ya Notisi ya Serikali (GN) Nambari ya 2005 inavyotaka. Kampuni zilizoteuliwa hazikuwa nyingi za kutosha kuhakikisha kwamba kunakuwa na ushindani na ni kampuni tatu tu zilizoitwa huku mbili pekee zikiwasilisha mchanganuo wao," inasema ripoti hiyo.


  Ripoti hiyo inabainisha kuwa kwa mujibu wa kanuni za manunuzi na GN, ili kuweka ushindani, BoT ilipaswa kuziita kampuni za ushauri kuanzia tano hadi 10 na kwamba walioitwa hawakuthibitishwa na Bodi ya Zabuni, kinyume na mahitaji ya kanuni ya 50(7) ya GN nambari 98 ya 2005.


  Ripoti inasema kuwa muda uliotolewa kwa mshauri kufanya kazi yake na kuwasilisha mchanganuo ulikuwa mdogo wa siku 12 tu, kinyume na Kanuni 56(1), na GN nambari 98 inayotaka mshauri apewe angalau siku 30 kufanya kazi na kuwasilisha mchanganuo.


  Ripoti inaeleza kwamba, aina ya mkataba uliotumika ilikuwa imeegemea kwa asilimia ambayo haitoi namna ya kupunguza gharama.

  "Kinyume chake ni kwamba inaweza kumshawishi mshauri kuchagua mchanganuo wenye gharama kubwa ili kuongeza gharama za ujenzi na kuongeza thamani ya ada ya kazi yake ya ushauri. Aina hii ya mkataba imependekeza iwapo itahusu gharama zisizobadilika (fixed costs)," inasema ripoti hiyo.


  "Hata huduma nyingine za majengo hayo pamoja na mabwawa ya kuogelea hayakuwamo katika mahitaji ya msingi ya benki, lakini yalipendekezwa na mshauri," inaongeza ripoti hiyo.


  Ripoti hiyo ya CAG inasema mshauri alilipwa zaidi kiasi cha Sh33.5 milioni, gharama ambazo zingeweza kuepukwa.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kulikuwa na ucheleweshwaji wa kusaini mikataba bila ya sababu za msingi wakati sheria inataka mikataba yote isainiwe ndani ya siku 28 baada ya makubaliano; ucheleweshwaji wa kuwalipa wahandisi huku wengi wakilipwa baada ya siku 14 na kuendelea.


  Ripoti inabainisha kuwa ongezeko la muda wa mradi huo lilikuwa linafanywa na mshauri wa ujenzi badala ofisa mhasibu wa BoT, huku madokezo yote ya vikao vya Bodi ya Zabuni yaliyoafikiwa, hayakusainiwa kulingana na mahitaji ya kisheria.


  Ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na timu ya wataalamu wa majengo kutoka ofisi CAG, ulioanza mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

  Taarifa ya matumizi hayo makubwa ya fedha kwa ajili ya kujengea nyumba mbili za watumishi hao wa umma ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili zikionyesha kuwa nyumba ya gavana ilikarabatiwa kwa takriban Sh1 bilioni.

  Lakini baadaye BoT ilitoa ufafanuzi ikieleza kuwa nyumba hizo hazikukarabatiwa bali zilijengwa upya kwenye viwanja vya BoT na kwamba baada ya taratibu zote za zabuni kufuatwa, nyumba hizo kujengwa kwa gharama ya takriban Sh1.274 bilioni kila mmoja.


  Awali kabla ya BoT haijajibu tuhuma za matumizi hayo ya fedha, Profesa Ndulu alikiri matumizi hayo lakini akafafanua kuwa kilichofanyika ni kujenga upya nyumba hizo na sio kuzikarabati.


  "Nyumba haijakarabatiwa bali imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu, ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema," alilalamika gavana huyo.


  Source: Mwananchi.

  Mtazamo:

  Tukisema BOT kuna uozo mtupu tunaambiwa tuna chuki hebu tizameni hii biashara ya ajabu kabisa. Kwanza ujenzi hauna makadirio ya awali na hakuna mtu anayehoji kuhusu hilo. Ikisha kuna disparity ya majenzi from estimated figures to the actual figures (difference ya kama Tshs 1 Billion kila nyumba!!!) hii haijafafanuliwa why? (Possible reasons watu wanajitungia tu gharama za majenzi possibly wakiinflate prices, na wajenzi nao wanaongeza tu bei kwani BOT ni kisima cha pesa). Ndio maana sijashangaa kwanini gavana anatetea biashara chafu kama hii. Nyumba ya Gavana wa BOT ina thamani kubwa kuliko nyumba ya gavana wa US na UK

  Haya mabadiliko makubwa kama haya ya swimming pool na vitu venginevyo yamechangia kukua kwa gharama za ujenzi. Je Bodi ilikuwa wapi kuliona hili au wanaenda kunywa chai tu ndani ya bodi?. Halafu pia isitoshe kuna delay katika kusainiwa mkataba kwanini? (Au ndio wananegotiate 10% of contract). Sina mengi but waungwana mengine mjazie ila BOT kumeoza!!!!
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Tuangalie tutawasiaidia watu walioathika na mabomu wapendanasema hivi tangu nisikie cag kasema haya kasema yale hata siku moja sijasikia action watu wanapewa adhabu sasa akuna haja ya kupoteza muda na cag...huyu kikwete kamtuma anapeleka mafaili ya riport imetoka akuna jipya ...
   
 3. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baada ya ripoti hiyo ni hatua gani zitafuata?
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni kweli Samson but tujiulize kwanini hakuna action inamaana it goes down kwamba system nzima imeoza ndio maana watu hawaoni ajabu watu kufanya ufisadi. Now ndio naona umuhimu wa mtu kama Dr Slaa kwani anaweza kuleta mabadiliko ijapokuwa bado nina shaka na baadhi ya wajumbe wa chadema (mfano marando na mbowe) but at least ni time kubadilisha uongozi kwani hakuna utawala wa sheria tanzania sasa hivi.
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiyo taarifa ya nyumba ya Gavana wa BOT na gharama zake nilivyoiona mara ya kwanza nilijua something wasnt right. hiyo nyumba ni ya kawaida kucost that much kwa kweli ukiangalia na swimming pool sijui na nini yani mkanganyiko tu.there is nothing exrta-ordinary in tha house. Sasa naona CAG kaja na ripoti mpya but what will they do baada ya kuona ripoti hiyo?? au ndo itapotezewa tu kama kawaida ya mambo ya ubadhirifu/ufisadi wa fedha yanavyofanyikaga?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,728
  Likes Received: 82,657
  Trophy Points: 280

  Kutakuwa hakuna hatua yoyote ile maana toka katika awamu ya ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi...hakuna lolote ni USANII TU!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  tunaitaji ari ya jino moja arimoja mkono mmoja apo tutatoka kimaisha
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  You can have the best controller/auditor but if the management/government do not utilise that office and implement the actions, then it is useless!
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Indeed they are using the CAG as guinea pig to document that they are doing an effective job but zero implementation
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndani ya hizo hela sio ajabu fedha za DECI imo humo kama haijasokomezwa kwenye uchaguzi mkuu.
   
 11. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
   
 12. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nikumbusheni,
  Katika hotuba ya mh. JK wakati akifunga Bunge nilisikia akisema kuanzia sasa tumempa madaraka CAG kupeleka mahakamani moja kwa moja wale wote wanaobainika kutumia vibaya pesa za serikali. Au nachanganya mambo?

  Kama ni hivyo let the useless BoT staff face the cuff. Then get to hell with this uncultured so called professor.

  Hata hivyo jamani CV ni muhimu hata tuzungushe namna gani maana ya elimu. Huyu gavana ni profesa toka chuo gani? chuo gani kilimpa u-profesa? Tunataka kumfahamu baadaye tufahamu vyuo vyenye rekodi za aina hii.
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Haya ndiyo madhara ya administration inayonuka rushwa kama ya JK!!

  Bado anakuja kutudangaya na ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi!!! What a crap?

  If you need chages, vote for Dr. Slaa; uwe CCM uwe upinzani vote fro Slaa period.
   
 14. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu ulichoadika ni kweli na imekuwa kawaida hawa viongozi kufanya maamuzi bila kufuata taratibu. Wanapoulizwa kazi kujitetea na kulalamika kuwa watu hawapendi maendeleo. Hapa hakuna kumung'unya maneno waondoke kwenye hivyo viti vyao na pia hii BOT inabidi ibadilishwe takataka zote zitolewe waingize damu mpya iliyo safi. Iliyopo ina virusi.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Tutawachukuaje siriasi wakati hawajui tofauti kati ya thamani na gharama? Utajumlishaje thamani na kupata gharama? Thamani si lazima ilingane na gharama. Ingekuwa hivyo basi zile nyumba za mbavu za mbwa kariakoo zisingeuzwa kwa mamia ya mamilioni!

  Na hizo gharama za ujenzi wakati wa kubuni ni zipi? Ubunifu mara nyingi unafanyika kabla ya ujenzi kuanza kwa sababu ujenzi unaongozwa na matokeo ya huo ubunifu.

  Vitu kama hivi ndivyo vinavyonikatisha tamaa.

  Amandla......
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huko peke yako mkuu sometimes najiuliza maswali mpaka naona kama nachanganyikiwa nashindwa kuamini kama BOT hakuna wajuzi au wahandisi makini. Na kama ni hivyo basi wanatangaza nini wanahitaji first class degree kuwapa ajira!!!!
   
 17. R

  Ramos JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Taarifa ya CAG kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za umma katika ukarabati wa nyumba za makazi za gavana na naibu wake imebainisha ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kiserikali na kuonyesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Taarifa hiyo inakuja huku ikikumbukwa kuwa wakati sakata hili lilipoibuliwa na vyombo vya habari gavana ndulu alijitokeza na kutetea matumizi hayo na kusema kwanza nyumba hizo hazikukarabatiwa bali zilijengwa upya kwa tsh billion 1.2 kwa kila moja.

  Ripoti ya CAG inaainisha matumizi hayo mabaya kuwa ni pamoja na gharama kubwa zisizoakisi kazi iliyofanyika, kukiukwa sera ya manunuzi ya serikali na mchakato usiokuwa halali wa kutafuta wazabuni pamoja na mapungufu mengine mengi...

  Kinachonisikitisha ni kuwa wakati akateuliwa gavana Ndulu aliingia kuchukua nafasi ya Balali aliyeonekana kuwa fisadi mkubwa na hivyo Ndulu aliletwa pale kama mtu msafi na atakayerudisha heshima ya BoT. Sasa kwa madudu haya aliyofanya, kumbe naye ni wale wale!!!!!

  Kwa kweli ingependeza huyu jamaa awajibishwe, lakini sasa tunajua hakuna anayewajibishwa kwani hata aliyemteua hakumteua kwa mapenzi yake bali kwa mapenzi ya yule 'aliyempeleka'

  Eee baba Mungu tenda miujiza Tanzania ikombolewe maana twaaafa bondeni huku kwenye machozi tunakoshindana na wenye nguvu wakaao gizani...
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kuna random errors na systematic errors. Sehemu kubwa ya kinachofanyika serikalini ni systematic errors. Watu wanapanga kwa makusudi kabisa kwamba leo tukiamua tufanye kosa la aina hii. Hii yote ni kwa malengo maalumu, yaani kujinufaisha.

  Siyo BoT tu! PPF, LPF NSSF, PSPF, nk. mashirika haya yote ambayo yameamua kujiingiza ktk ujenzi. Angalia thamani ya nyumba zao ukilinganisha na gharama zinazotumika. Ni wizi tu na kwa kulifahamu hilo ndo maana hawakupi mkopo wa fedha bali wanajenga wao wenyewe.

  Miradi hii imekuwa ni conduit ya kufyonza pesa ya wastaafu.
   
 19. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwe
  Hivi siku zote Gavana alikuwa anaishi wapi? leo mnamjengea nyumba mpya na kusahau walimu wangu na wauguzi kule vijijini.
  Nilifeli hesabu za algebra lakini hizi za kugawa na kujumlisha hazinipi tabu. kwa Bilioni 1.5 utapata nyumba za walimu zipatazo 500 za kuwahifadhi walimu 1000 mpaka 1500 kama ni maseja.
  Nafikiri hili dubwashika linafika mwisho. Hongera CAG kwa kutuwekea rekodi ya matukio haya, wahusika wajiandae kuvirudisha vitu vyote hivi serikali ya umma itakapoingia madarakani. Na hili haliko mbali tusubiri kidogo tu.
  Mungu anawaona na imani zenu feki juu ya uwepo wake kwa kumtolea sadaka za wizi (Mnajiliwaza tu, hukumu yenu ipo palepale)
  Inaumiza sana
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I think we should be calling these mistakes and not errors, hope you get it bro!
   
Loading...