CAG aagiza ukaguzi wa uchunguzi mji wa Babati

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ameagiza kuanzisha ukaguzi wa uchunguzi kwenye Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara, ambayo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 imepata hati yenye mashaka.

Kichere ametoa agizo hilo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji huo cha kujadili taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kilichohudhuriwa na mkuu wa mkoa huo, Queen Sendiga.

Kichere amesema kuna nyaraka zimetolewa na wataalam wa idara ya fedha baada ya halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka hivyo zichunguzwe ili kubaini zilikuwepoaawali au zimetengenezwa.

Amesema halmashauri hiyo ilipopata hati yenye mashaka kuna maelezo walipaswa kutoa wataalam wa idara ya fedha ila wakawasilisha nyaraka nyingine zikiwa tofauti na awali.

“Majibu yanayotolewa ni ya ajabu, hakuna ushirikiano unatoa nyaraka ambazo wakaguz hawakuziona tangu mwezi Desema mwaka 2022 wakaja kuzileta mwishoni nadhani hamtutendei haki,” amesema.

"Tusaidie mamlaka ifanye kazi yake kwani tutazifanyia uchunguzi hizo nyaraka kama ni halisi au zimetengenezwa na ikiwa ni ubabaishaji itakuwa siyo hoja tena bali uvunjifu wa sheria," amesema Kichere.

Amesema serikali inatoa fedha nyingi za maendeleo hivyo ni wajibu wa madiwani kuzisimamia ili zifanikishe utendaji kazi kwa wananchi na siyo kutumika vibaya kama ilivyotokea.

“Mtaalam umesomea taratibu za fedha na una CPA kisha unashindwa kusimamia kanuni na taratibu za fedha hadi kusababisha halmashauri inapata hati yenye mashaka?” amehoji Kichere.

Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo, Queen Sendiga ameagiza watumishi waliosababisha halmashauri ya mji wa Babati, kupata hati yenye mashaka kuchukuliwa hatua.

“Wale wote waliosababisha halmashauri ya mji wa Babati kupata hati yenye mashaka wachukuliwe hatua kwa kufanyiwa uchunguzi na watakaobainika vyombo vya kisheria vifanye kazi yao,” amesema.
 
Babati. Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ameagiza kuanzisha ukaguzi wa uchunguzi kwenye Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara, ambayo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 imepata hati yenye mashaka.

Kichere ametoa agizo hilo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji huo cha kujadili taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kilichohudhuriwa na mkuu wa mkoa huo, Queen Sendiga.

Kichere amesema kuna nyaraka zimetolewa na wataalam wa idara ya fedha baada ya halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka hivyo zichunguzwe ili kubaini zilikuwepoaawali au zimetengenezwa.

Amesema halmashauri hiyo ilipopata hati yenye mashaka kuna maelezo walipaswa kutoa wataalam wa idara ya fedha ila wakawasilisha nyaraka nyingine zikiwa tofauti na awali.

“Majibu yanayotolewa ni ya ajabu, hakuna ushirikiano unatoa nyaraka ambazo wakaguz hawakuziona tangu mwezi Desema mwaka 2022 wakaja kuzileta mwishoni nadhani hamtutendei haki,” amesema.

"Tusaidie mamlaka ifanye kazi yake kwani tutazifanyia uchunguzi hizo nyaraka kama ni halisi au zimetengenezwa na ikiwa ni ubabaishaji itakuwa siyo hoja tena bali uvunjifu wa sheria," amesema Kichere.
Amesema serikali inatoa fedha nyingi za maendeleo hivyo ni wajibu wa madiwani kuzisimamia ili zifanikishe utendaji kazi kwa wananchi na siyo kutumika vibaya kama ilivyotokea.

“Mtaalam umesomea taratibu za fedha na una CPA kisha unashindwa kusimamia kanuni na taratibu za fedha hadi kusababisha halmashauri inapata hati yenye mashaka?” amehoji Kichere.

Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo, Queen Sendiga ameagiza watumishi waliosababisha halmashauri ya mji wa Babati, kupata hati yenye mashaka kuchukuliwa hatua.“Wale wote waliosababisha halmashauri ya mji wa Babati kupata hati yenye mashaka wachukuliwe hatua kwa kufanyiwa uchunguzi na watakaobainika vyombo vya kisheria vifanye kazi yao,” amesema.

CREDIT: MWANANCHI
 
Kicheere fuatilia mauzo batili ya
1. Rasilimali za taifa.
2. Usalama wa hili taifa.
3. Kuvunjwa katiba
4. Tetesi za kuuzwa kwa bunge na jitihada za kukosekana uzalendo kunakofanywa hadharani na wazenj
 
Back
Top Bottom