CAF yazindua Nembo Rasmi ya AFCON 2027, Kenya, Tanzania na Uganda waungana kwenye Utambulisho wa Mashindano.

CAF yazindua Nembo Rasmi ya AFCON 2027, Kenya, Tanzania na Uganda waungana kwenye Utambulisho wa Mashindano.

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
351
Reaction score
333
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua rasmi nembo ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda.



​
Nembo hiyo imebeba taswira ya utamaduni na utambulisho wa Afrika Mashariki, ikiwa na rangi za bendera za mataifa hayo matatu ambazo ni kijani, nyekundu, njano, nyeusi na bluu.


8173.jpg
8174.jpg

​
Kwa mujibu wa maelezo ya muundo huo, nembo imejengwa kwa kuunganisha taswira ya kombe la AFCON na ngao inayowakilisha utambulisho wa mataifa matatu mwenyeji.

Uzinduzi huo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayokuwa ya kihistoria kwa ukanda huu, huku Kenya, Tanzania na Uganda zikipata nafasi ya kuwa mwenyeji wa AFCON kwa pamoja.

Mashindano hayo ya mwaka 2027 yanatarajiwa kuleta pamoja mataifa mbalimbali ya Afrika katika kile kitakachokuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya soka kuwahi kuandaliwa Afrika Mashariki.
 
safi wasilete uarabu na ukristo.. walete u Africa
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Novemba 19, 2026 lilizindua rasmi nembo ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, inayotarajiwa kufanyika katika Mataifa ya Tanzania(Dar esSalaam, Arusha na Zanzibar), Kenya na Uganda.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotajwa, michuano ya AFCON 2027 inatarajiwa kuanza Juni 19 na kumalizika Julai 17, 2027 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
file_00000000caec81f4ac78a7753151d389.png
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Novemba 19, 2026 lilizindua rasmi nembo ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, inayotarajiwa kufanyika katika Mataifa ya Tanzania(Dar esSalaam, Arusha na Zanzibar), Kenya na Uganda.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotajwa, michuano ya AFCON 2027 inatarajiwa kuanza Juni 19 na kumalizika Julai 17, 2027 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.View attachment 3713431
Safi sana
 
Sioni viwanja vya kuchezea michuano ya caf Kwa Tanzania
 
Back
Top Bottom