CAF kupanga makundi Afrika Kusini Oktoba 06

Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
12,139
25,409
image-18-960x640.png

Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’ linasubiri Oktoba 06 ili kukamilisha mpango wa kupanga makundi ya Michuano ya ngazi ya vilabu iliyo chini ya shirikisho hilo kwa msimu huu 2023/24.

CAF imewalazimu kusubiri hadi Oktoba 06, ili kutoa nafasi kwa mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Mtoano ambao ulichezwa jana Jumatatu (Oktoba 02) kati ya Mabingwa wa Soka nchini Algeria Chabab Riadhi de Belouizdad (CR Belouizdad) dhidi ya Bo Rangers ya Sierra Leone.

Mchezo wa mkondo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo mjini Bo nchini Sierra Leone, Chabab Riadhi de Belouizdad ilichomoza na ushindi wa mabao 3-1, na matokeo ya mchezo wa Mkondo wa Pili Chabab Riadhi de Belouizdad imechomoza na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-2. By dar 24
 
Wazee wa papatu papatu ndiyo safari imefikia tamati. Nawatabiria kuyaaga mashindano kwa aibu kubwa.

JARIBU kuwa positive...

Hata mashindano ya kimataifa mnakuwa hivyo...

Tunapakujifunza kwa WENZETU, WAZUNGU.

Ama kweli UJINGA ni KIPAJI.
 
Back
Top Bottom