Bwana Mtei matatani kwa kumchukua mwanamke msukule

Bwana Mtei matatani kwa kumchukua mwanamke msukule

Siku moja nilikwenda kwenye kanisa la Ufufuo,Ubungo,yule Askofu,mhubiri akawa anasema wapo misukule wengi,akawaita mmoja mmoja wasimame,pale pale walipo,waeleze experience zao. Wale wanawake,four or five,or more,wakawa wanaeleza jinsi walivyopelekwa mortuary Muhimbili halafu wakazinduka. Medical phenomena ambaye inaweza kuelezwa na daktari yoyote,wao wanafikiria ni mambo ya ushirikina.
 
huyo dada inasemakana sio msukule bali ana matatizo ya akili juzi alienda kituo cha polisi mbezi akaingia chooni akakaa muda sana baadae askali wa kike wakamuogesha na kumsitili na akawakimbia
anawezekana akili yake inamtuma kukaa chooni tuu
Duu hatari
 
Mtoto wa mtei kapiga mkwara endapo gazeti lolote litaandika habari hii kuihusisha na familia yao atawasue. Tusubiri tuone
 
Sasa huyu Bibie Haika mbona ameshaharibu, fursa hiyo bana! angekaa kimya waandike alafu waisome namba.
Una uhakika huyu ni mwanamke mkuu? Kuna tofauti kati ya aika na haika refer Freeman mbowe nae anatumia haika.
 
Bora amekanusha maana sasahivi kila mtu ana smartphone! Anaona kila kitu!

Jana niliziona pic za huyo msukule na nyingine ikimtaja huyo Mtei huku akiwa kafungwa pingu kwa kukutwa msukule kwenye Tank la maji taka aiseee....
Picha kiukweli hazitazamiki
 
Poleni sana wachagga tatizo la kupenda pesa kupitiliza mpaka mnawaharibu ndugu zenu
 
Sasa huyu Bibie Haika mbona ameshaharibu, fursa hiyo bana! angekaa kimya waandike alafu waisome namba.

Huyo Haika naona anazingua tu aiseeee.....
Maana hiyo habari fully Jana ilkuepo hadi Instagram na picha kadhaa
 
Wabongo kwa ushirikina.. Apimwe akili huyo dada.. Atakuwa mgonjwa tu!
 
Ila hii biashara ya umiliki wa vyombo vya usafiri niliikataa katakata kwasabab wabongo ni watu wa ajab sana ajali ikitokea iue abiria utasingiziwa umetoa kafara na wako serious nakulazimisha iwe kweli. Hata kama ni wazi ni uzembe wa dereva ama mwengine wewe mmiliki utaambiwa umetoa kafara tuuuuu.

Tunaish katika taifa linaloamini ushirikina kwa kila kitu. Nyambaff zetu
Kweli kabisa mdau, imani za ushirikina, uchawi ni katiba ya watanzania. Huyo mama/dada aliyeonekana kwa Mtei ana dalili zote za ukichaa (hutembea uchi), lakini watu wanang'ang'ania ni msukule wa Mtei.
Ndio maana huwa nawaza sana hivi: Akitokea bibi kizee asiyetunzwa na familia yake (ni mchafu, ana njaa na kakondeana sana) akitoka kwenda kuomba msaada kisha kwa bahati mbaya akajikwaa na kuanguka chini, kuna watu watasema huyo bibi ni mchawi kadondoka kwenye ungo.Watampiga na kumuua bibi wa watu kwa imani za kijinga za ushirikina.
 
Huyo Haika naona anazingua tu aiseeee.....
Maana hiyo habari fully Jana ilkuepo hadi Instagram na picha kadhaa
Atujibu pia yule Babu yake kule Babati ameacha kutembea kwa miguu..
 
Kweli kabisa mdau, imani za ushirikina, uchawi ni katiba ya watanzania. Huyo mama/dada aliyeonekana kwa Mtei ana dalili zote za ukichaa (hutembea uchi), lakini watu wanang'ang'ania ni msukule wa Mtei.
Ndio maana huwa nawaza sana hivi: Akitokea bibi kizee asiyetunzwa na familia yake (ni mchafu, ana njaa na kakondeana sana) akitoka kwenda kuomba msaada kisha kwa bahati mbaya akajikwaa na kuanguka chini, kuna watu watasema huyo bibi ni mchawi kadondoka kwenye ungo.Watampiga na kumuua bibi wa watu kwa imani za kijinga za ushirikina.

Ni kweli kabisa Shieka, Tanzania tumefikia pabaya sana. Miaka ya zamamni Vichaa walikuwa na haki zao na walilindwa ndani ya jamii leo hii km unavyosema kila kitu kinahusishwa na uchawi. Tena ukithubutu kukemea utakuta ooh hata vitabu vya dini vinasema. maajabu yenyewe imani za kishirikina badala ya kupubngua ndio zinazidi!
 
mh...,jamani..mi mbona message nilizopata hata hazikuspecify Mtei gani...kwani wachaga mna Mtei mmoja tu au
 
hata yule jamaa aliyefungwa pingu amechomekewa tu kwenye hili tukio,
hilo tukio lake la kufungwa pingu limetokea miaka mitatu iliyopita halihusiani na msukule wala kosa la dereva aliyetanua barabarani anaitwa Salimu Athumani baba yake ni lecturer chuo cha ushirika moshi.
 
baba yake anaitwa nani couz mi niko ushirika hapa
 
Back
Top Bottom