Bwana Heri jiandae mapema, unatafutiwa uchochoro wa kutokea

Habari Bwana heri, Kipenzi cha watu.
Na hakika u-mzima wa afya tele na unaendelea na majukumu yako ya kulijenga taifa hili changa.

Najua unavyopata shida kutoka kwa boss wako, hujui boss wako anataka nini.

Nikueleze tu wazi Bwana Heri, siku zako zinahesabikaa.

Unajua nini?

Hili sakata la wakulima wa figo huko sauzi ndio chambo yako ya mwisho, jiangalie sana.
Unajua hata wadogo zako hawakuheshimu sanaa.

Yule kijana wa New York city anasema wazi kwamba hakuna wa kumtisha zaidi ya boss wenu wote. Tena anaenda mbali zaidi na kudai kwamba akiamua hata wewe utang'oka kwani mnaweka sana uzibe katika mambo yake na babake.

Juzi kati ulimpogia simu boss wako na kumwuliza kuhusu yule muhindi aliyetekwa, akakuchana live, fanya Mambo yako, hii si kazi yako.

Nashukuru sakata limepita bila ya neno lako. Mwezio King masuti na raba alipigiwa Simu akaambiwa aseme lolote kuhusu huyo mhindi, ikabidi aje akulalamikie eti kwanini missions zinafanya hashirikishwi wakisha haribu ndo wanamtafuta, ulisikitika sana, ila ushauri uliompa ulimsaidia.

King Masuti alichelewa kutekeleza maagizo ya boss, bwana mdogo wa New York akakasirika sana na ndipo akapewa maagizo yatekelezwe kabla ya saa 6 mchana bila ajizi nafikiri king alimaliza.

Ni mengi sana mmetofautiana na Boss wako, kuna kipindi ulimtaka amwondoe yule jamaa aliekuwa chambachamba wa Yanga, lkn majibu yake yalikukata maini.

Sasa hili sakata la wafanyabiashara wa figo nadhani jana alikupa alert kuwa hata wewe anaweza kukung'oa na atakung'oa kweli.

Akikung'oa atanunua figo zote kwa bei nzuri tu, na wewe utaonekana msaliti.

Unajua nini, wafanyabiashara nao wamekasirika, wengine wameapa kutonunua kwa bei ya boss wako. Omba mungu yasitokee haya, mana yakitokea kibarua chako kitaingia mchanga.

Kijana wa newyork ampaka sasa anamlilia baba, anashangaa kukuacha wewe mpaka leo. Pole sana.

Mi ni hayo tu Bwana heri, kwa ushauri wangu wa mwisho, bora ufanye maamuzi kama ya mzee mawingu, ule pensions na 80% ya mshahara wako, vinginevyo Utafyekelewaa mbali.

Mimi si mtu wa huko, mimeziokota toka kwa watu wa hukoo.

Nakutakia kazi njema.
Kwaheri.
Nimetoka kapa,ngoja nkanywe kwanza bia then maisha yaendelee
 
Inamaana prezidaa alikua anazusha kua anaweza kumtoa?
Wewe unajua uchapaji kazi wake kuliko JPM?
Huo ni uzushi hakuna wa kumtoa majaliwa maana yeye na magufuli wanapiga kazi, kazi anayofanya majaliwa hakuna mtu ambaye kaifikia kiurahisi, namaanisha ukimlinganisha na mawaziri wakuu kama.Lowassa na warioba au sumaye
 
Nashukuru sakata limepita bila ya neno lako. Mwezio King masuti na raba alipigiwa Simu akaambiwa aseme lolote kuhusu huyo mhindi, ikabidi aje akulalamikie eti kwanini missions zinafanya hashirikishwi wakisha haribu ndo wanamtafuta, ulisikitika sana, ila ushauri uliompa ulimsaidia.

King masuti na raba ndo yule boss wa mambo ya jikoni, mwenye mifuko ya bendera
 
Kijana wa newyork ampaka sasa anamlilia baba, anashangaa kukuacha wewe mpaka leo. Pole sana.

Mi ni hayo tu Bwana heri, kwa ushauri wangu wa mwisho, bora ufanye maamuzi kama ya mzee mawingu, ule pensions na 80% ya mshahara wako, vinginevyo Utafyekelewaa mbali.

Mimi si mtu wa huko, mimeziokota toka kwa watu wa hukoo.
DUH! KAZI IPO
 
Back
Top Bottom