Nipo, majukumu ya hapa na pale tu.
nakuona upo umejaa tele wedding planner.
Jamaa alijiwekea takribani milion sita hivi akajiamini harusi yake itakuwa nzuri. Michakato ya mahari jamaa akamaliza kama milioni mbili hivi zikabaki nne. Akaitisha kikao cha ndugu wa karibu akatumia kama laki mbili, kikao cha kwanza akatumia laki tano. Milioni mbili na laki nane ikiwa imebaki.
Ahadi yake kwa kamati ilikuwa milioni moja na nusu ambayo alilipia advance ya ukumbi akawa amebaki na milioni moja laki nane. Maandalizi yake pamoja na ya bibi harusi mpaka sasa kabaki na pesa ya mbuzi.
Bajeti ya harusi milioni 20, Cash iliyopatikana mpaka sasa milioni 4. Kikao cha mwisho kitakuwa jumapili ijayo, jamaa kachanganyikiwa. Kachukuwa ukimbi wa kifahari, sijui itakuwaje. Nimemshauri hapo afanye bia moja na soda moja kama hali aitageuka.
Kwa nini watu wagumu sana kuchangia harusi siku hizi, mtawauwa maharusi kwa pressure.
oky karibu kwa huduma hiyo ya kuplainiwa harusi yako au wewe bado tayari?
Ndo mana kila siku nasema ukitaka kuoa hakikisha wewe kama bwana harusi unachangia 80% ya gharama zote
Mi mwnyw sichangii harusi cku hizi,watu wanaweka bajeti ya harusi kuuubwaaaaa kwa kutegemea michango ya watu akhaaa!wajitegeme!
Nimevaa shela lako safiii! bwana harusi suti nzuri ! tukienda kanisani baadaye hotel na ndugu zangu na marafiki wachache tunakula chakula cha pamoja na picha za ukumbusho baasi inatosha .Maisha mengine yaendelee
Safi sana mama unajua muda mwingine wanawake ndio sababu ya wanaume kuwa na stress za kuoa katika maongezi dada mipango ni harusi ya mamilioni! kaka lazima aumwe kichwa .lakini ukiwa kawaida unamsaidia hata huyo bwana harusi mtarajiwa.Mungu anipe uhai nioleww,hiii ndio aina ya haruc nataka,uwiiii ctaki strees mm
My statement implies that IT FEELS BETTER TO CRY ON MERCEDES BENZ THAN ON A BICYCLE.
My statement implies that IT FEELS BETTER TO CRY ON MERCEDES BENZ THAN ON A BICYCLE.
Ha ha ha dada hata mm hutonichangia?
Mkishaolewa ndo mnageuka hivyo....tumewashtukia
siamini kwenye hiyo taasisi.
Waache wenye imani zao waingie.
La sivyo uwe mchangiaji mzuri waharusi za wenzako!