Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Jamaa alijiwekea takribani milion sita hivi akajiamini harusi yake itakuwa nzuri. Michakato ya mahari jamaa akamaliza kama milioni mbili hivi zikabaki nne. Akaitisha kikao cha ndugu wa karibu akatumia kama laki mbili, kikao cha kwanza akatumia laki tano. Milioni mbili na laki nane ikiwa imebaki.
Ahadi yake kwa kamati ilikuwa milioni moja na nusu ambayo alilipia advance ya ukumbi akawa amebaki na milioni moja laki nane. Maandalizi yake pamoja na ya bibi harusi mpaka sasa kabaki na pesa ya mbuzi.
Bajeti ya harusi milioni 20, Cash iliyopatikana mpaka sasa milioni 4. Kikao cha mwisho kitakuwa jumapili ijayo, jamaa kachanganyikiwa. Kachukuwa ukimbi wa kifahari, sijui itakuwaje. Nimemshauri hapo afanye bia moja na soda moja kama hali aitageuka.
Kwa nini watu wagumu sana kuchangia harusi siku hizi, mtawauwa maharusi kwa pressure.