Bwana Harusi hakujiandaa au udhalilishaji?

Bwana Harusi hakujiandaa au udhalilishaji?

............Maandalizi ya harusi yamekamilika.. siku ya harusi bi harusi mtarajiwa anasubiri gari la kumpeleka saloon kupambwa ... gari halikutokea... akaamua kuchukua bajaj hadi saloon... yuko saloon anasubiri shela shela inakuja saa 9:30, baada ya kupambwa anasubiri gari lililopambwa aelekee kanisani gari halikutokea....anaamua kuchukua Bajaj hadi kanisani... kanisa la walokole... ameshachelewa lakini Mchungaji anafanya staha....... anawafungisha ndoa.... baada ya ndoa wanatoka nje ya kanisa ... hakuna cha gari la maharusi wala gari la wazazi wala wapambe..... kwa aibu ndugu wa mume wanaamua kukodi Taxi kuwachukua maharusi na kuelekea kusikojulikana ......na kuwaacha ndugu wa mke wasijue anakopelekwa mtoto wao......lakini ikumbukwe kwamba Bwana harusi alikuja siku ya sendoff na wapambe wake na ndugu wa chache ... walikula na kunywa .....kadi za mwaliko wa harusi walizopaswa kuja nazo siku ya sendoff hawakujanazo......ili bidi waalikwa wa sherehe hiyo nao kutawanyikia kila mtu na shughuli zake...My take:- Wazazi mnaotaka watoto wenu waolewe juu kwa juu bila kufanya utafiti wa binti yako anakwenda wapi liangalieni hili... fanyeni utafiti mjue hali ya baadaye ya binti yasije yakawakuta kama yalivyowakuta hawa jamaa zangu
Kuna wanaume wanatuaibisha sana....hadi naona kama hadithi vile....
 
Ndoa ilikwishatimilizika na kushughudiwa na watu, ila alikosea hakuwaanda wakwe kwa surprise aliyotoa.
 
Cha msingi ndoa ilifungwa,Mungu awabariki ktk ndoa yao.haya mengine yote ni mapambo na anasa za dunia hii.
 
Kuna wanaume wanatuaibisha sana....hadi naona kama hadithi vile....
hahahah nahisi ni kutotumia akili na hekma tu waambie watu kuwa huna uwezo,au hamna sherehe ,je unategemea nini baada yakurudi mtaani? hao ni wakwe zake atawaangaliaje ?hao ni ndugu wa mke wako lazima atarudi kwao watamwellewaje .inshort huyo jamaa ni mburula na hana akili tena ni mjinga kabisa maana umaskini unasemwa tu jamani hatuna sherehe tukituka kila mtu aende akujuapo ,baasi nani analazimisha kitu unakula saa sita unakunya saa 12asubuhi fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
bwanaharusi nadhani hakuwa muwazi tapeli huyu
Ha ha ha Smile.. wakati mwingine mahaba yanakulazimisha ufanye yasiotegemewa na wala sio utapeli.. Hii inaonyesha kulikuwa na makubaliano fulani kati ya mke na mume.. Kama hii story ni ya kweli lakini.. Maana imekaa ki-far fetched story
 
Last edited by a moderator:
Bwana harusi na ndugu zake wote wahuni"!! kwanini wasiliweke wazi mapema kwa wakwe zao
kuwa hatutakuwa na ratiba yoyote baada ya ndoa?!!
 
ila angesema mapema jamani loh!

Eti?! Hata mimi sioni tatizo la kufanya harusi ya minimum budget (or none at all, if any). Tunaongea kabla kuwa bwana mie mambo hayaeleweki, kwa hiyo tukitoka kanisani tu tuishie zetu nyumbani. Nami nawaandaa watu wangu wa karibu kuwa, jamani huko shughuli hamna, halafu taratibu baada ya ndoa tunajipakilia bajaji yetu, nyumbaniiii....kwa roho safi.

Sasa wewe mwanzoni ulikuja kwa mkao utafikiri unamiliki Hyatt, siku ya siku unakuja kunikimbiza na bajaji mji mzima siku yangu ya kumeremeta!........wapi na wapi?
 
Bwana harusi na ndugu zake wote wahuni"!! kwanini wasiliweke wazi mapema kwa wakwe zao
kuwa hatutakuwa na ratiba yoyote baada ya ndoa?!!
Hapana sio uhuni Mkuu, baada ya sendoff hakukuwa na Kadi ZA MWALIKO, manake kusingekuwa na Sherehe, Hiyo ilikuwa meseji tosha, Mi nafikiri umefika wakati sasa wa kuacha mamichango ya sherehe badala yake tuchangie elimu.
 
Hahaha. Yaani kabla hajachumbia jamaa angeambiwa apeleke bank statement za miezi 3? Labda wanakamati tu walimuangusha chalii wa watu, asingetaka kuoa asingetokea church
 
Ha ha ha ha, kwani anatafuta mkopo?

Hahaha. Yaani kabla hajachumbia jamaa angeambiwa apeleke bank statement za miezi 3? Labda wanakamati tu walimuangusha chalii wa watu, asingetaka kuoa asingetokea church
 
Ha ha ha Smile.. wakati mwingine mahaba yanakulazimisha ufanye yasiotegemewa na wala sio utapeli.. Hii inaonyesha kulikuwa na makubaliano fulani kati ya mke na mume.. Kama hii story ni ya kweli lakini.. Maana imekaa ki-far fetched story

................ Haya mambo yametokea kweli.. ndo maana nikasema Bwana harusi hakujiandaa au kudhalilisha... hebu soma baadhi ya wachangiaji humu wameshawahi kushuhudia mikasa tena kuzidi huu....sio stori ya kuungaunga...
 
We unadhani ndoa ni ule ufahari wa kusifiwa kuwa watu wamekula hadi wametapika na wengine wamekunywa hadi wanavua nguo.
 
Aaah hiyo kali japo inaumiza sana

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom