Bwana Harusi amzibua kibao Bi harusi-siku ya harusi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bwana Harusi amzibua kibao Bi harusi-siku ya harusi.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by fazaa, Dec 29, 2011.

 1. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nasoma gazeti moja la kuwait linaitwa Rai....nimekuta news moja inasema kama kichwa cha habari kweye thread hii.

  Sababu ya bwana harusi kumzabua kibao mke wake huyo mpya wakati wa harusi yao....ni pale bi harusi alipomcheka mama wa mme wake kwenye harusi yao...Mama wa bwana harusi alikuwa mnene sana sa alipo amka kucheza kufarahia harusi ya mwanae ndo pale alipoanguka na bi harusi akashindwa kujizuia akaanza kucheka....Alipocheka aakapata kipigo pale pale kutoka kwa mme wake.

  Swali kw awanaume; Je we kama bwana harusi pale utafanya nini-utafanya kama alivyo fanya mme wa huyo bi harusi....au uta-mezea tu mke wako amcheke mama yako.

  Kwa wanawake we kama bi harusi pale utacheka kama huyo bi harusi au utajikaza ili usichekee.

  Ukumbi wenu.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  mi ningejikausha.....japo inachekesha....he he he he......
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Ah!Huyo jamaa nae kiboko!Mwanaume hayupo hivyo bana.Sisi wanaume wakati mwingine hasira zinazidi!
   
 4. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mwanamume wa kikurya nini?
   
 5. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  :smash::smash::smash:
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ningemzaba kibao
   
 7. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Atakuwa mkurya huyo
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  wote wawili sio wazima hao

  mke, hata kama inachekesha alipaswa awe na staha, angeomba kwenda maliwato akachekee huko

  mume, hakupaswa kumpiga mkewe, angetafuta njia ya kumwonya asicheke (hata kumfinya) na si kumpiga,maana kajidhalilisha,kamdhalilisha mkewe na kamdhalilisha mama yake maana kila mtu kanoti kuwa kaanguka,na sasa ulimwengu mzima wanajua kaanguka
   
 9. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Huyo bwana harusi ana bahati. Ingekuwa mimi, tungezikunja ukumbini.

  Hakuwa na sababu ya kumdharirisha mkewe. Kile kitendo kilikuwa cha ghafla mno na cha kuchekesha, hakikuwa kimekusudiwa, kicheko kilimtoka bibi harusi kwa bahati mbaya kama kikohozi.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  "Eeh mama wee, kama ingekuwa we ungefanyaje?"
   
 11. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  This is a very good comment.
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Swali la nyongeza: Je angekuwa ni mama yako mzazi ungemcheka?
   
 13. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi sijawahi kupiga mwanamke toka nimezaliwa-nakumbuka baba yangu alisema toka nimezaliwa sijawahi kupiga mwanamke-na mama yangu alisapoti hapo hapo....


  Yani tokea siku hio nikajua my father was a great man.

  Mimi ningempa kichapo cha kitandani cha kiana yake...Afu siku ya pili ningemuambia akaombe samahani kwa mama yangu.
   
 14. MERCIFUL

  MERCIFUL JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,471
  Likes Received: 746
  Trophy Points: 280
  Si jambo jema ila kwa kusema ule ukweli inachekesha. Na kicheko ni kama kikohozi, huwezi kukizuia, angepaliwa mwali wa watu buuure kisa kuzuia kicheko! Mbaya zaidi, kama bi harusi ni mwenzangu na mie ambae kicheko hakikai mbali basi ni tabu tupu..hapo hastahili kulaumiwa hata chembe!
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapana mimi nadhani bond kati ya mtu na mkwewe haipo kabisa. Ingekuwepo Bi arusi asingethubutu kucheka sana sana angejikuta anatoka mbio kumkimbilia kwa kuhofia pengine mama yake ameumia!
  Mama wa mumeo ni mama yako je angeanguka mama yake mzazi yeye angecheka?

  Mume nae, kwani ukumbini alicheka mkewe peke yake? Haikuwa busara kumrushia kibao! Angeuchuna kisha akamnyime hanemuni.
   
 16. 1

  19don JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hata huyo mume kofi lilimtoka kwa bahati mbaya kama kicheko , angemuongeza lakwangu moja ingekuwa poa sana huwezi kumcheka baba au mama mkwe kwa kisingizio chochote , kwangu wazazi ni mungu wa pili na mungu huwa hachekwi
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mie ningecheka, sababu sicheki kwa sababu nam-undermine
  nacheka sababu kanichekesha. Hata angekuwa mama yangu mzazi ningecheka kwa uhuru.

  Baada ya kucheka ningejizaba kibao kimoja saafi to serve trouble kwa mume kuchafua kanzu yake.
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Je, wewe ndo ungekuwa bibi Arusi, ungekubali kupigwa hadharani?

  Nionavyo mimi hiyo ndoa itakuwa inasuluhisha tofauti zake kwa kuchapana. Very sad.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama ni mie, nasimama na kumpa Koni ya Bakresa alambe......

  Alamba, Alamba ............... Amhhh, Amhh..............

  Kicheko Kwishieni.
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jibu kutoka kwa Ibrah
  Yaani ndio jibu la swali langu!?

  Ah ah ah, kuna mdau hapo juu amesema hata icho kibao nacho kilitoka kwa bahati mbaya kama kilivyotoka kicheko.... Bahati mbaya kwa bahati mbaya...!

  Je angekuwa mama yako mzazi ungemcheka?
   
Loading...