Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

Asee naomba kujulishwa kama lara 1 ameshakomment hapa?
 
Last edited by a moderator:
Mimi kwakweli nimeipenda sana hekima aliyotumia huyo mtendwa!! huu ni mfano wa kuigwa kwani mwisho wa siku ni mwanamke ndio anabaki na simanzi baada ya kutemwa bila malumbano wala ugomvi. Wanaume tunatofautiana kimaamuzi ila jamaa kama atasimamia maamuzi yake ya FINITO basi atakua perfect kabisa, huwezi kuishi tena na mke kama huyo hata ukishauriwa wa tanzania nzima!

hiyo staili ni wachache wanaweza aisee, angekuwa mwingine sa izi angekuwa jela muda mrefu tu
 
Dah.... Pole yake shemejio... Badala ya yeye kumsurprise mkewe, mkewe nduye kamsurprise!!!!

Any way ..... !!!Ausikize moyo wake

hizi surprise hizi zimemtokea puani bana shem wangu...ila mwenyewe hakuwa na was was wowote ule ukizingatia ndoa yenyewe miez 3, yaaani ilikuwa bado mbichi kbs
 
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

Shemeji yangu (ndugu yake na mume wangu) ameoa mwishoni mwa mwezi April mwaka huu wa 2013 na harusi yenyewe ilifana sana...ilikuwa harusi ya kukata na shoka(naweza sema) kwa manjonjo yaliyokuwapo...kiukweli ilipendeza sana..
Lakini cha kusikitisha hivi majuzi tu huyu shemeji yangu amemfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine live..

Huyo shemeji yangu ni mfanyakazi wa bank hapa dar, na huyo mkewe ni mwalimu huko mkoani, kwa hivo baada ya kufunga ndoa na honeymoon kumalizika wife akarudi kazini kwake, na Mr akaendelea na kazi kama kawaida huku akihangaika kutafuta uhamisho wa mkewe aje jijini dar, au ikishindikana yeye ahamie huko mkoani alipo mkewe..

shemeji yangu alikuwa akienda huko alipo wife au mkewe anakuja dar wanapopata nafasi..Sasa siku moja shemeji yangu akaamua kwenda kwa mkewe kwa supraise, hakumwambia wife kama anaenda..alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kuongeza mapenzi kati yao hakujua kuwa atakutana na msiba badala ya furaha aliyotegemea..yeye anasema hakuwa anamhisi mkewe chochote na wala hakuwahi kufikiria kama mkewe anamsaliti

shemeji yangu huyu akaenda shopping ya nguvu kamnunulia wife zawadi, nguo, na makochokocho kibao..bila kusahau shoping ya vyakula mbalimbali...huyoo akawasha gari kwenda kwa wife kimya kimya bila kumwambia kama anaenda..akitegemea kumfurahisha mkewe na yeye mwenyewe kufurahi,...alipofika ilikuwa jioni mida ya saa 12 ivi jua halijazama na milango ilikuwa wazi (imerudishiwa tu haijafungwa) akaingia hadi chumbani akiwa na hamu ya kumuona mke wake kwa surprise na kupokelewa mazawadi aliyobeba..

Ghafula kuingia chumbani akakuta sinema live, wife akiwa na mwanaume mwingine wako bize kitandani...HEEE..LA HAULA..SHEMEJI YANGU NUSURA acolapse..lkn alijikaza kiume huku akitumbua macho asiamini kinachotokea...na wao kuona hivo wakasitisha zoezi na kubaki wanatumbua macho...uzuri shemeji yangu hakukurupuka kwa hasira na kuanza kuleta vurugu lkn alitoka nje na kuwafungia ndani na kuita majirani...walipofika wakakuta wameshavaa nguo huku bi harusi akilia na kuomba msamaha sana...

mbele ya majirani wazee waliwaambia kila mmoja aandike maelezo na kuweka sahihi yake akikiri kufumaniwa ambapo wote walifanya hivo na shemeji yangu naye akaandika maelezo jinsi alivyowakuta na wakasaini wote...

shemeji yangu akaondoka hapo nyumbani na kwenda kulala hoteli akisubiri kesho yake arejee dar.. ndipo alipowapigia simu ndugu zake na kuwaeleza alichokikuta na hatua waliyofikia ya kuandikisha na wote wakasaini..mpaka hapo alikuwa hajamuuliza wife wake chochote na wala hajamsemesha huyo mgoni wake..walipoandika maelezo na kusaini akawashukuru wazee na kuondoka zake...

kufika dar ndugu wameitisha kikao na mwenye mke amesema ndoa imefikia ukingoni wala hataki kikao na ndugu za mke wake wala hataki kumwona huyo mwanamke tena.(labda ni hasira baada ya muda zitapungua) ila imemdisturb sana..

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman

Yamemkutaaa eeeehhh!!! Akome kukurupuka kuoa vicheche. Mpe pole yake. Hiyo ndio dunia. Hayajaanza leo. Yapo. Yalikuwepo. Na yataendelea kuwepo. Ndio.

hiyo staili ni wachache wanaweza aisee, angekuwa mwingine sa izi angekuwa jela muda mrefu tu
Ni kweli kabisa, lakini Mungu alimpa uwezo wa kuvumilia!! kilichobaki ndugu na marafiki zake wakae nae huyo mwanaume wajaribu kumpa moyo tu na kumhakikishia kwamba huyo aliekua nae hakuwa mke mwema, bali azidi kuomba na kusubiri atakae mfariji. Hata huyo bibi harusi's nae anahitaji maombi na ushauri nasaha vinginevyo wandugu wanaweza wakamkosa pia!!!!
 
Ndio maana kila mara huwa naandika hapa jamvini kuwa, kuelewa namna mwanamke anavyowaza na kupambanua mambo ni ngumu mno...
Siku hizi wanawake wanaolewa kwa kuwa tu wanahitaji ndoa, lakini ndani kabisa ya mioyo yao huwa kuna Mwanaume ambaye yeye mwanamke anamuamini ndiye Mfalme wa Moyo wake...
Wenyewe wanawake huwa wanajiaminisha kuwa watajifunza kupenda kadiri muda unavyoenda, yaani wanaifanya ndoa kama uwanja wa mazoezi ya kujifunza kupenda...
Hivyo binafsi kwa tukio kama hili wala sishangai sana...

Ndiyo suala linapokuja hapo kwamba kwann wanawake waolewe na wanaume wasiowapenda? Kwann usiolewe na unaempenda? Mi nailaumu jamii!
Mnalazimisha wanawake kuingia kwny ndoa pasipo kupenda!
Tunaposema mwanamke lazima uolewe, usipoolewa wewe ni nuksi, wewe malaya, wewe huna mvuto, wewe kahaba, umri unaenda, miaka 25 ikifika hujaolewa huo ndio mwisho wako, usichague sana, ndipo hachagui sana anasema nitajifunza kupenda humohumo!
Badala yake tuwatie moyo, tunaodhani wamechelewa kufikia ivyo, tuwaombee wapate wenza... sio kuwasimanga na kauli za kukatisha tamaa
 
Uchagani wazee wenye nyumba wakitoka safari hata siku moja hawaendi nyumbani moja kwa moja...watatafuta mtoto wanamtuma apeleke mizigo hata kama ni gazeti then wao wanapitia kwanza baa....nimegundua ni kwa nini wale wazee wanaishi maisha marefu aiseee........
 
wazee wana busara bana, sie wa mujini tunafanya suprise, kumbe tunajifanyia wenyewe
 
Ndiyo suala linapokuja hapo kwamba kwann wanawake waolewe na wanaume wasiowapenda? Kwann usiolewe na unaempenda? Mi nailaumu jamii!
Mnalazimisha wanawake kuingia kwny ndoa pasipo kupenda!
Tunaposema mwanamke lazima uolewe, usipoolewa wewe ni nuksi, wewe malaya, wewe huna mvuto, wewe kahaba, umri unaenda, miaka 25 ikifika hujaolewa huo ndio mwisho wako, usichague sana, ndipo hachagui sana anasema nitajifunza kupenda humohumo!
Badala yake tuwatie moyo, tunaodhani wamechelewa kufikia ivyo, tuwaombee wapate wenza... sio kuwasimanga na kauli za kukatisha tamaa

ila mtu mwenyewe si ana akili, kwa nn amkubali kaka wa watu kumbe ana yake ya kale, wanawake saa ingine tunajishushia hadhi wenyewe
 
Dah, huo moyo alionao huyo jamaa ni kiboko, najaribu kufikiria muda aliotumia kulishuhurikia hilo swala kwa kuita wazee, kuandikishiana n.k huku akiendelea kumuangalia huyo mke wa kichina na jamaa lake.
Binafsi sijui kipi kingetokea, ila kingekuwa ni kibaya sana.

Ushauri, everything happen for a reason. So asisononeke sana, kikubwa ni kwamba amegundua hilo mapema; ingawa naamini litamchukua muda mrefu sana kumtoka ndani ya kichwa chake. Ajitahidi kuwa yeye kama yeye, aanze ukurasa mpya.
 
Ni kweli kabisa, lakini Mungu alimpa uwezo wa kuvumilia!! kilichobaki ndugu na marafiki zake wakae nae huyo mwanaume wajaribu kumpa moyo tu na kumhakikishia kwamba huyo aliekua nae hakuwa mke mwema, bali azidi kuomba na kusubiri atakae mfariji. Hata huyo bibi harusi's nae anahitaji maombi na ushauri nasaha vinginevyo wandugu wanaweza wakamkosa pia!!!!

huyo bi harusi hata ndg zake wanaona aibu amewaaibisha sana....wamenyamaza kimyaaaaaa, mana jamaa amewapiga hadi picha
 
Dah, huo moyo alionao huyo jamaa ni kiboko, najaribu kufikiria muda aliotumia kulishuhurikia hilo swala kwa kuita wazee, kuandikishiana n.k huku akiendelea kumuangalia huyo mke wa kichina na jamaa lake.
Binafsi sijui kipi kingetokea, ila kingekuwa ni kibaya sana.

Ushauri, everything happen for a reason. So asisononeke sana, kikubwa ni kwamba amegundua hilo mapema; ingawa naamini litamchukua muda mrefu sana kumtoka ndani ya kichwa chake. Ajitahidi kuwa yeye kama yeye, aanze ukurasa mpya.

ndio ht sis tunamshauri ajitahidi kusahau, ni bahati mbaya, haina mwenyewe...tunaamin atacoup tu baada ya muda fulan
 
Yamemkutaaa eeeehhh!!! Akome kukurupuka kuoa vicheche. Mpe pole yake. Hiyo ndio dunia. Hayajaanza leo. Yapo. Yalikuwepo. Na yataendelea kuwepo. Ndio.

kwan utajua kwa nje basi ndg yangu, mdada mwenyewe anaonekana decent tu, usingedhan km ni kicheche eti, ni bahati mbaya tu imemtokea shem yang
 
Ningekuwa mimi ni kuachana naye tu, kwani atafute vidogdogo vipo vizuri vingi tu. Uzuri wanaume huwa hatuna expiry date, ni hela ya mboga tu basi. Yeye avumilie, akipata aende kufunga ndoa ya serikali.
 
mwenzangu, ndugu wanamlaumu kwenda kwa surprise, wanamwambia hii ni dunia nyingine bora angemwambia tu..lkn yy anasema anashukuru Mungu kamuonysha mapema

Ndugu wanamlaumu?? Badala ya kumpongeza kwa kugundua huo uozo?! Tupa kule..! Nachukia sana watu wanaowasababishia wenzao maumivu! ------- kabisa huyo dada, kwa nini usimwage picha zake za harusi hapa ajulikane tu!!Unamtia mtu hasara ya mali na hali...kupendwa unapendwa, kukuhudumia anakuhudumia, unataka nini tena! Kama ni hiyo kugegedwa kama alikuwa hakutimizii ipasavyo yanini kumtia hasara ya mali na hali! Tupa kule..

Jamaa yetu jitahidini mumuweke karibu kwa maana ya ku socialize kutembeleana, outing etc etc. Muhimu pia asogee pande za kiimani zaidi atapata ushauri mzuri kwa wanaolinda mioyo yetu!

Lete picha za harusi ya huyo bidada hapa! Edit ili umuhifadhi ndugu yetu huyo asionekane
 
Back
Top Bottom