Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

kamusi

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
1,079
750
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

Shemeji yangu (ndugu yake na mume wangu) ameoa mwishoni mwa mwezi April mwaka huu wa 2013 na harusi yenyewe ilifana sana...ilikuwa harusi ya kukata na shoka(naweza sema) kwa manjonjo yaliyokuwapo...kiukweli ilipendeza sana..
Lakini cha kusikitisha hivi majuzi tu huyu shemeji yangu amemfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine live..

Huyo shemeji yangu ni mfanyakazi wa bank hapa dar, na huyo mkewe ni mwalimu huko mkoani, kwa hivo baada ya kufunga ndoa na honeymoon kumalizika wife akarudi kazini kwake, na Mr akaendelea na kazi kama kawaida huku akihangaika kutafuta uhamisho wa mkewe aje jijini dar, au ikishindikana yeye ahamie huko mkoani alipo mkewe..

shemeji yangu alikuwa akienda huko alipo wife au mkewe anakuja dar wanapopata nafasi..Sasa siku moja shemeji yangu akaamua kwenda kwa mkewe kwa supraise, hakumwambia wife kama anaenda..alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kuongeza mapenzi kati yao hakujua kuwa atakutana na msiba badala ya furaha aliyotegemea..yeye anasema hakuwa anamhisi mkewe chochote na wala hakuwahi kufikiria kama mkewe anamsaliti

shemeji yangu huyu akaenda shopping ya nguvu kamnunulia wife zawadi, nguo, na makochokocho kibao..bila kusahau shoping ya vyakula mbalimbali...huyoo akawasha gari kwenda kwa wife kimya kimya bila kumwambia kama anaenda..akitegemea kumfurahisha mkewe na yeye mwenyewe kufurahi,...alipofika ilikuwa jioni mida ya saa 12 ivi jua halijazama na milango ilikuwa wazi (imerudishiwa tu haijafungwa) akaingia hadi chumbani akiwa na hamu ya kumuona mke wake kwa surprise na kupokelewa mazawadi aliyobeba..

Ghafula kuingia chumbani akakuta sinema live, wife akiwa na mwanaume mwingine wako bize kitandani...HEEE..LA HAULA..SHEMEJI YANGU NUSURA acolapse..lkn alijikaza kiume huku akitumbua macho asiamini kinachotokea...na wao kuona hivo wakasitisha zoezi na kubaki wanatumbua macho...uzuri shemeji yangu hakukurupuka kwa hasira na kuanza kuleta vurugu lkn alitoka nje na kuwafungia ndani na kuita majirani...walipofika wakakuta wameshavaa nguo huku bi harusi akilia na kuomba msamaha sana...

mbele ya majirani wazee waliwaambia kila mmoja aandike maelezo na kuweka sahihi yake akikiri kufumaniwa ambapo wote walifanya hivo na shemeji yangu naye akaandika maelezo jinsi alivyowakuta na wakasaini wote...

shemeji yangu akaondoka hapo nyumbani na kwenda kulala hoteli akisubiri kesho yake arejee dar.. ndipo alipowapigia simu ndugu zake na kuwaeleza alichokikuta na hatua waliyofikia ya kuandikisha na wote wakasaini..mpaka hapo alikuwa hajamuuliza wife wake chochote na wala hajamsemesha huyo mgoni wake..walipoandika maelezo na kusaini akawashukuru wazee na kuondoka zake...

kufika dar ndugu wameitisha kikao na mwenye mke amesema ndoa imefikia ukingoni wala hataki kikao na ndugu za mke wake wala hataki kumwona huyo mwanamke tena.(labda ni hasira baada ya muda zitapungua) ila imemdisturb sana..

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman
 
duuh na huyo mdada ana nyege gani jamani?
mbona watu wanapenda ngono hivi?
kweli mshahara wa dhambi mauti

inavosemekana huyo alikuwa mtu wake siku nyingi ila shem wangu hakujua..ndio stori zinazosemwa baada ya tukio hilo na hata majirani walikuwa wanamjua huyo another mr ambaye ni mume wa mtu...sasa kalikoroga sijui huyo mume wa mtu atamuweka ndani jumla? ila aibu
 
Mapenzi ya bongo ukitaka kujiua na pressure we fanya hizo surprise..........!

Huyo jamaa anahitaji watu wakumshauri tena wenye ndoa zao/au wataalam wa mambo ya ndoa na ikiwezekana hata kiroho zaidi la sivyo atapotea au hata kuwa na roho ya kuua!!!!!!!

Ametendwa aiseeeeeee.........
 
duh nimepata suprise nimekosa hata cha kumshauri....labda azidi kuomba msamaha anaweza kumsamehe
 
Maskini daaah mpe pole sana shemeji yako,huyo mke mbona katia aibu jamani daaah!
Hatuwezi kumlaumu mume coz alikua anaenda kwake tena kwa mkewe halali.
Mi nashauri kueni nae karibu mpeni ushauri na msimuache akae peke yake na pia mumshauri asiache kazi coz akiacha kazi ndo stress zitazidi kwa kua ilde.
Hayo ni maisha hatupendi yatokee bt yanatokea kwa wengi ashukuru Mungu amelijua hilo mapema japo i vigumu kusahau bt atachangamka na kurudi hali ya kawida .
Cha msingi msimuache peke yake.
 
inavosemekana huyo alikuwa mtu wake siku nyingi ila shem wangu hakujua..ndio stori zinazosemwa baada ya tukio hilo na hata majirani walikuwa wanamjua huyo another mr ambaye ni mume wa mtu...sasa kalikoroga sijui huyo mume wa mtu atamuweka ndani jumla? ila aibu

Huyo jamaa atamuacha tu......hawawezi kudumu!!!!!!itakula kwake mpaka achanganyikiwe.
 
Mapenzi ya bongo ukitaka kujiua na pressure we fanya hizo surprise..........!

Huyo jamaa anahitaji watu wakumshauri tena wenye ndoa zao/au wataalam wa mambo ya ndoa na ikiwezekana hata kiroho zaidi la sivyo atapotea au hata kuwa na roho ya kuua!!!!!!!

Ametendwa aiseeeeeee.........

mwenyewe alikuwa innocent, kajipanga na mazawadi yake, yaaaaani we acha tu
 
duh nimepata suprise nimekosa hata cha kumshauri....labda azidi kuomba msamaha anaweza kumsamehe

sijui, kwa jinsi ilivyo, kila mtu amekuwa surprised, huyo mwenye mke ndio anatia huruma, labda atasamehe, lkn sijui, hakuna dalili
 
duuh na huyo mdada ana nyege gani jamani?
mbona watu wanapenda ngono hivi?
kweli mshahara wa dhambi mauti
Smile.. huyo dada hapendi ngono sema anampenda huyo aliekutwa nae anafanya ngono.. Lazima atakuwa ni mtu wake wa siku nyingi.. Haya ndio matatizo ya kuoa/kuolewa bila ya mahaba ya dhati..
 
Last edited by a moderator:
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

Shemeji yangu (ndugu yake na mume wangu) ameoa mwishoni mwa mwezi April mwaka huu wa 2013 na harusi yenyewe ilifana sana...ilikuwa harusi ya kukata na shoka(naweza sema) kwa manjonjo yaliyokuwapo...kiukweli ilipendeza sana..
Lakini cha kusikitisha hivi majuzi tu huyu shemeji yangu amemfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine live..

Huyo shemeji yangu ni mfanyakazi wa bank hapa dar, na huyo mkewe ni mwalimu huko mkoani, kwa hivo baada ya kufunga ndoa na honeymoon kumalizika wife akarudi kazini kwake, na Mr akaendelea na kazi kama kawaida huku akihangaika kutafuta uhamisho wa mkewe aje jijini dar, au ikishindikana yeye ahamie huko mkoani alipo mkewe..

shemeji yangu alikuwa akienda huko alipo wife au mkewe anakuja dar wanapopata nafasi..Sasa siku moja shemeji yangu akaamua kwenda kwa mkewe kwa supraise, hakumwambia wife kama anaenda..alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kuongeza mapenzi kati yao hakujua kuwa atakutana na msiba badala ya furaha aliyotegemea..yeye anasema hakuwa anamhisi mkewe chochote na wala hakuwahi kufikiria kama mkewe anamsaliti

shemeji yangu huyu akaenda shopping ya nguvu kamnunulia wife zawadi, nguo, na makochokocho kibao..bila kusahau shoping ya vyakula mbalimbali...huyoo akawasha gari kwenda kwa wife kimya kimya bila kumwambia kama anaenda..akitegemea kumfurahisha mkewe na yeye mwenyewe kufurahi,...alipofika ilikuwa jioni mida ya saa 12 ivi jua halijazama na milango ilikuwa wazi (imerudishiwa tu haijafungwa) akaingia hadi chumbani akiwa na hamu ya kumuona mke wake kwa surprise na kupokelewa mazawadi aliyobeba..

Ghafula kuingia chumbani akakuta sinema live, wife akiwa na mwanaume mwingine wako bize kitandani...HEEE..LA HAULA..SHEMEJI YANGU NUSURA acolapse..lkn alijikaza kiume huku akitumbua macho asiamini kinachotokea...na wao kuona hivo wakasitisha zoezi na kubaki wanatumbua macho...uzuri shemeji yangu hakukurupuka kwa hasira na kuanza kuleta vurugu lkn alitoka nje na kuwafungia ndani na kuita majirani...walipofika wakakuta wameshavaa nguo huku bi harusi akilia na kuomba msamaha sana...

mbele ya majirani wazee waliwaambia kila mmoja aandike maelezo na kuweka sahihi yake akikiri kufumaniwa ambapo wote walifanya hivo na shemeji yangu naye akaandika maelezo jinsi alivyowakuta na wakasaini wote...

shemeji yangu akaondoka hapo nyumbani na kwenda kulala hoteli akisubiri kesho yake arejee dar.. ndipo alipowapigia simu ndugu zake na kuwaeleza alichokikuta na hatua waliyofikia ya kuandikisha na wote wakasaini..mpaka hapo alikuwa hajamuuliza wife wake chochote na wala hajamsemesha huyo mgoni wake..walipoandika maelezo na kusaini akawashukuru wazee na kuondoka zake...

kufika dar ndugu wameitisha kikao na mwenye mke amesema ndoa imefikia ukingoni wala hataki kikao na ndugu za mke wake wala hataki kumwona huyo mwanamke tena.(labda ni hasira baada ya muda zitapungua) ila imemdisturb sana..

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman

Kwanza naqmnpongeza sana shemji yako. Ninachoweza kusema kwa harakaharaka ni kwamba fanyeni haraka sana kumtafutia mtu wa Counselling, Pamoja na ushauri Nasaha naomba kama ni Mkristo asome kitabu cha Hosea chote ama waqweza kukisoma hata wewe na kujaribu sana kumsaidia kuelewa suala lake na uzoefu wa jambo hili.

Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kukabiliana na jambo hili, sio rahisi na wala usishangae kwa hatua ya yeye kuwa mpweke ni hatua ya frustration na lazima awe lonely.
 
huyo mtaalam anapatikana wapi aisee, ni wazo zuri ngoja tulifanyie kazi
 
Back
Top Bottom