Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

mmmmhhh honeymon? hiyo sijasikia..

oooh, bibie kaachwa rum mwanaume kadaiwa ameitwa na marafiki( jiulize marafiki gani hao wasioheshimu hiyo kitu), huwezi kuamini mwanaume karudi kesho yake asubuhi. dah! mie sijui ningemtoboa macho!!
 
inavosemekana huyo alikuwa mtu wake siku nyingi ila shem wangu hakujua..

Ndio maana kila mara huwa naandika hapa jamvini kuwa, kuelewa namna mwanamke anavyowaza na kupambanua mambo ni ngumu mno...
Siku hizi wanawake wanaolewa kwa kuwa tu wanahitaji ndoa, lakini ndani kabisa ya mioyo yao huwa kuna Mwanaume ambaye yeye mwanamke anamuamini ndiye Mfalme wa Moyo wake...
Wenyewe wanawake huwa wanajiaminisha kuwa watajifunza kupenda kadiri muda unavyoenda, yaani wanaifanya ndoa kama uwanja wa mazoezi ya kujifunza kupenda...
Hivyo binafsi kwa tukio kama hili wala sishangai sana...
 
Smile.. huyo dada hapendi ngono sema anampenda huyo aliekutwa nae anafanya ngono.. Lazima atakuwa ni mtu wake wa siku nyingi.. Haya ndio matatizo ya kuoa/kuolewa bila ya mahaba ya dhati..

ndio ni mtu wake wa siku nyingi inasemekana..lkn ni mume wa mtu
 
Ndio maana kila mara huwa naandika hapa jamvini kuwa, kuelewa namna mwanamke anavyowaza na kupambanua mambo ni ngumu mno...
Siku hizi wanawake wanaolewa kwa kuwa tu wanahitaji ndoa, lakini ndani kabisa ya mioyo yao huwa kuna Mwanaume ambaye yeye mwanamke ndio Mfalme wa Moyo wake...
Wenyewe wanawake huwa wanajiaminisha kuwa watajifunza kupenda kadiri muda unavyoenda, yaani wanaifanya ndoa kama uwanja wa mazoezi ya kujifunza kupenda...
Hivyo binafsi kwa tukio kama hili wala sishangai sana...

sio wote lkn, wengine wazur tu
 
oooh, bibie kaachwa rum mwanaume kadaiwa ameitwa na marafiki( jiulize marafiki gani hao wasioheshimu hiyo kitu), huwezi kuamini mwanaume karudi kesho yake asubuhi. dah! mie sijui ningemtoboa macho!!

mmmmmmmmhhhhhhh aiseeee, hiyo kali...
 
Unapooa sio kuwa huyo mwanamke hakuwa na mtu ila amekupa maksi za juu kuliko wengine.La muhimu jamani hizi ndoa za kuishi Dar Mke Dodoma mwisho ni hivyo hata yeye ni binadamu anaweza akapitiwa na akakukmbushia na zaidi yuko free na mbaya zaidi haina makombo!!!!!!!
 
Smile.. huyo dada hapendi ngono sema anampenda huyo aliekutwa nae anafanya ngono.. Lazima atakuwa ni mtu wake wa siku nyingi.. Haya ndio matatizo ya kuoa/kuolewa bila ya mahaba ya dhati..

ndo faida zake maana ndoa zimekuwa dil
 
Last edited by a moderator:
kuna jamaa mmoja ameanzisha kauzi hapo.. Honeymoon za nin miaka hii.?
 
Unapooa sio kuwa huyo mwanamke hakuwa na mtu ila amekupa maksi za juu kuliko wengine.La muhimu jamani hizi ndoa za kuishi Dar Mke Dodoma mwisho ni hivyo hata yeye ni binadamu anaweza akapitiwa na akakukmbushia na zaidi yuko free na mbaya zaidi haina makombo!!!!!!!

hatukatai kupitiwa ila kufanyia kwenye kitanda unacholala na mmeo/mkeo,..chumba chenu,..ni
kosa la aibu na halisemeheki..
 
Dah kweli huyo shemeji yako ana moyo wa kuhimili maana wengine hapo ni kwamba angeondoka hapo na kesi ya mauaji tena ya watu wawili kwa mpigo maana kama angekuwa na silaha karibu ambacho kingefuata ni kuwauwa wote wawili maana hilo ni fumanizi live
Kaeni nae karibu maana msongo wa mawazo alio nao anawez akuchukua hatua nyingine mbaya kabisa
Wala asiache kazi may be cha kufanya aombe ahamishwe kwenye kituo chake cha sasa ambapo kuna watu wake wa karibu wanaomjua na wanaojua kila kitu ahamie sehem ambako ni mbali na marafiki zake wa sasa
Ila msiruhusu kukaa peke yake au bila kazi ya kufanya anaweza kuchukua maamuzi ambayo siyo kabisa
Mtafutieni hata viongozi wa dini au watu wazima wenye kujua namna ya kutoa ushauri kuhusu hayo na wakae nae kwa karibu kumpa ushauri namna ya kuvuka kipindi hiki
Ajue kuna maisha baada ya haya na hapo sio mwisho wa maisha na yaliyotokea huenda Mungu amemuepusha na mengi maana ingekuwa na magonjwa angepata huko huko ila Mungu kapenda kumuonyesha mabaya ya huyo mwanamke mapema sana
 
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

Shemeji yangu (ndugu yake na mume wangu) ameoa mwishoni mwa mwezi April mwaka huu wa 2013 na harusi yenyewe ilifana sana...ilikuwa harusi ya kukata na shoka(naweza sema) kwa manjonjo yaliyokuwapo...kiukweli ilipendeza sana..
Lakini cha kusikitisha hivi majuzi tu huyu shemeji yangu amemfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine live..

Huyo shemeji yangu ni mfanyakazi wa bank hapa dar, na huyo mkewe ni mwalimu huko mkoani, kwa hivo baada ya kufunga ndoa na honeymoon kumalizika wife akarudi kazini kwake, na Mr akaendelea na kazi kama kawaida huku akihangaika kutafuta uhamisho wa mkewe aje jijini dar, au ikishindikana yeye ahamie huko mkoani alipo mkewe..

shemeji yangu alikuwa akienda huko alipo wife au mkewe anakuja dar wanapopata nafasi..Sasa siku moja shemeji yangu akaamua kwenda kwa mkewe kwa supraise, hakumwambia wife kama anaenda..alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kuongeza mapenzi kati yao hakujua kuwa atakutana na msiba badala ya furaha aliyotegemea..yeye anasema hakuwa anamhisi mkewe chochote na wala hakuwahi kufikiria kama mkewe anamsaliti

shemeji yangu huyu akaenda shopping ya nguvu kamnunulia wife zawadi, nguo, na makochokocho kibao..bila kusahau shoping ya vyakula mbalimbali...huyoo akawasha gari kwenda kwa wife kimya kimya bila kumwambia kama anaenda..akitegemea kumfurahisha mkewe na yeye mwenyewe kufurahi,...alipofika ilikuwa jioni mida ya saa 12 ivi jua halijazama na milango ilikuwa wazi (imerudishiwa tu haijafungwa) akaingia hadi chumbani akiwa na hamu ya kumuona mke wake kwa surprise na kupokelewa mazawadi aliyobeba..

Ghafula kuingia chumbani akakuta sinema live, wife akiwa na mwanaume mwingine wako bize kitandani...HEEE..LA HAULA..SHEMEJI YANGU NUSURA acolapse..lkn alijikaza kiume huku akitumbua macho asiamini kinachotokea...na wao kuona hivo wakasitisha zoezi na kubaki wanatumbua macho...uzuri shemeji yangu hakukurupuka kwa hasira na kuanza kuleta vurugu lkn alitoka nje na kuwafungia ndani na kuita majirani...walipofika wakakuta wameshavaa nguo huku bi harusi akilia na kuomba msamaha sana...

mbele ya majirani wazee waliwaambia kila mmoja aandike maelezo na kuweka sahihi yake akikiri kufumaniwa ambapo wote walifanya hivo na shemeji yangu naye akaandika maelezo jinsi alivyowakuta na wakasaini wote...

shemeji yangu akaondoka hapo nyumbani na kwenda kulala hoteli akisubiri kesho yake arejee dar.. ndipo alipowapigia simu ndugu zake na kuwaeleza alichokikuta na hatua waliyofikia ya kuandikisha na wote wakasaini..mpaka hapo alikuwa hajamuuliza wife wake chochote na wala hajamsemesha huyo mgoni wake..walipoandika maelezo na kusaini akawashukuru wazee na kuondoka zake...

kufika dar ndugu wameitisha kikao na mwenye mke amesema ndoa imefikia ukingoni wala hataki kikao na ndugu za mke wake wala hataki kumwona huyo mwanamke tena.(labda ni hasira baada ya muda zitapungua) ila imemdisturb sana..

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman

safi kabisa alivyofanya huyo mwanamke...mijanaume mingine haina akili...wee uoe alafu mke arudi mkoani maana yake nini? mwanamke kuombwa k na kugevedwa dio hulka yake sasa y umpe mazingira ambayo hago yanaweza tokea? imekula kwake kwa uninga wake mwenyewe.
 
Mwambie Shemeji yako ale Ganzi, hana Sababu ya Kumwambia kila mtu Mkasa uliompata.
So long as watu wanajua kuwa Mkewe yuko Mkoani, its a Good point kwa yeye kuendelea na Life, Hope hatapata Maswali mengi ya Mkeo yuko wapi.
PS, Mtafutieni House girl wa Kumsaidia vijikazi vidogo vidogo
 
Balaah!!

Ndio maana watu wanaogopa kuona aisee.

Nwy mpe pole sana shemeji yako. Inabidi mjitahidi kuwa karibu nae kila wakati na kama inawezekana mumtafutie mshauri kabisa. Badala ya kuacha kazi mpeni wazo la kuchukua likizo tu apumzike kwa muda huku akipewa ushauri na wataalam. With time , maumivu yatapungua, aibu nayo itapungua na atakubali matokeo kwamba huyo mwanamke hakuwa wake au pengine atamsamehe alisongeshe.
 
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman

Dah! ndo faida za wazungu waliotuletea suprise.
"Udhungu" noma suprise waachie wenyewe. We ukikaribia home kama kutoa taarifa imeshindikana jaribu basi hata kumtuma mtoto atangulize zawadi home basi.
 
Back
Top Bottom