Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

Bwana harusi amfumania mkewe live miezi 3 tu baada ya ndoa

Dah kweli huyo shemeji yako ana moyo wa kuhimili maana wengine hapo ni kwamba angeondoka hapo na kesi ya mauaji tena ya watu wawili kwa mpigo maana kama angekuwa na silaha karibu ambacho kingefuata ni kuwauwa wote wawili maana hilo ni fumanizi live
Kaeni nae karibu maana msongo wa mawazo alio nao anawez akuchukua hatua nyingine mbaya kabisa
Wala asiache kazi may be cha kufanya aombe ahamishwe kwenye kituo chake cha sasa ambapo kuna watu wake wa karibu wanaomjua na wanaojua kila kitu ahamie sehem ambako ni mbali na marafiki zake wa sasa
Ila msiruhusu kukaa peke yake au bila kazi ya kufanya anaweza kuchukua maamuzi ambayo siyo kabisa
Mtafutieni hata viongozi wa dini au watu wazima wenye kujua namna ya kutoa ushauri kuhusu hayo na wakae nae kwa karibu kumpa ushauri namna ya kuvuka kipindi hiki
Ajue kuna maisha baada ya haya na hapo sio mwisho wa maisha na yaliyotokea huenda Mungu amemuepusha na mengi maana ingekuwa na magonjwa angepata huko huko ila Mungu kapenda kumuonyesha mabaya ya huyo mwanamke mapema sana

kwa kweli amejitahidi, mume wng mwenyewe anasema km ni yy sa izi angekuwa jela...hata sie tunajarib kuwa karib nae na tumemshauri asiache kaz lkn anaonekana kukata tamaa kbs..sijui labda siku zikipita atazoea
 
Jamani Jamani, dunia imekwisha,

Shemeji yangu (ndugu yake na mume wangu) ameoa mwishoni mwa mwezi April mwaka huu wa 2013 na harusi yenyewe ilifana sana...ilikuwa harusi ya kukata na shoka(naweza sema) kwa manjonjo yaliyokuwapo...kiukweli ilipendeza sana..
Lakini cha kusikitisha hivi majuzi tu huyu shemeji yangu amemfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine live..

Huyo shemeji yangu ni mfanyakazi wa bank hapa dar, na huyo mkewe ni mwalimu huko mkoani, kwa hivo baada ya kufunga ndoa na honeymoon kumalizika wife akarudi kazini kwake, na Mr akaendelea na kazi kama kawaida huku akihangaika kutafuta uhamisho wa mkewe aje jijini dar, au ikishindikana yeye ahamie huko mkoani alipo mkewe..

shemeji yangu alikuwa akienda huko alipo wife au mkewe anakuja dar wanapopata nafasi..Sasa siku moja shemeji yangu akaamua kwenda kwa mkewe kwa supraise, hakumwambia wife kama anaenda..alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kuongeza mapenzi kati yao hakujua kuwa atakutana na msiba badala ya furaha aliyotegemea..yeye anasema hakuwa anamhisi mkewe chochote na wala hakuwahi kufikiria kama mkewe anamsaliti

shemeji yangu huyu akaenda shopping ya nguvu kamnunulia wife zawadi, nguo, na makochokocho kibao..bila kusahau shoping ya vyakula mbalimbali...huyoo akawasha gari kwenda kwa wife kimya kimya bila kumwambia kama anaenda..akitegemea kumfurahisha mkewe na yeye mwenyewe kufurahi,...alipofika ilikuwa jioni mida ya saa 12 ivi jua halijazama na milango ilikuwa wazi (imerudishiwa tu haijafungwa) akaingia hadi chumbani akiwa na hamu ya kumuona mke wake kwa surprise na kupokelewa mazawadi aliyobeba..

Ghafula kuingia chumbani akakuta sinema live, wife akiwa na mwanaume mwingine wako bize kitandani...HEEE..LA HAULA..SHEMEJI YANGU NUSURA acolapse..lkn alijikaza kiume huku akitumbua macho asiamini kinachotokea...na wao kuona hivo wakasitisha zoezi na kubaki wanatumbua macho...uzuri shemeji yangu hakukurupuka kwa hasira na kuanza kuleta vurugu lkn alitoka nje na kuwafungia ndani na kuita majirani...walipofika wakakuta wameshavaa nguo huku bi harusi akilia na kuomba msamaha sana...

mbele ya majirani wazee waliwaambia kila mmoja aandike maelezo na kuweka sahihi yake akikiri kufumaniwa ambapo wote walifanya hivo na shemeji yangu naye akaandika maelezo jinsi alivyowakuta na wakasaini wote...

shemeji yangu akaondoka hapo nyumbani na kwenda kulala hoteli akisubiri kesho yake arejee dar.. ndipo alipowapigia simu ndugu zake na kuwaeleza alichokikuta na hatua waliyofikia ya kuandikisha na wote wakasaini..mpaka hapo alikuwa hajamuuliza wife wake chochote na wala hajamsemesha huyo mgoni wake..walipoandika maelezo na kusaini akawashukuru wazee na kuondoka zake...

kufika dar ndugu wameitisha kikao na mwenye mke amesema ndoa imefikia ukingoni wala hataki kikao na ndugu za mke wake wala hataki kumwona huyo mwanamke tena.(labda ni hasira baada ya muda zitapungua) ila imemdisturb sana..

huyu shemeji yangu kwa sasa hapendi kusocialize kama zamani,muda mwingi yuko peke yake, amekonda ghafla, sijui hali chakula, kazi anataka kuacha japo hajapata kazi nyingine (anaona aibu jinsi watu walivyohangaika kumchangia) leo hii hata miezi 6 haijafika ndoa imevunjika..
Kwa nature yake ni mchangamfu sana, lkn siku hizi amekuwa mkimya sana..ninaamini atakuwa anaumia sana ndani kwa ndani...
sijui tufanyeje katika kumsaidia maana kwa jinsi alivyo anaweza kucomit hata suicide, mawazo yenu jaman


ingekuwa inawezekana angejitokeza mdada mwenye huruma ampe company bila sharti lolote na aweze hata kukubali kulala naye anapohitaji hilo pasipo usumbufu mwingi wa hard to get. kuna mambo mengine dawa hailetwi na sheria, mahesabu-hesabu na kufikiri kwingi. mambo mengine dawa yake ni mapenzi tu. huyu mtu atakuwa anajihisi hapendeki, hatoshi, hatoshelezi, kadharauliwa kupita kipimo; gusa kitu chochote ambacho kinahesabika mali ya mwanamume, usiguse ile sehemu. ile sehemu ipo karibu sana ha kujiamini kwa mwanamume, kujipenda kwa mwanamume na mengine yote yanayohusu heshima ya mwanamume. siijui dharau kubwa mwanamke anaweza kumfanyia mwanamume kuzidi hii ya kutangaza kuwa mume huyo hatoshi. tiba ya huyu shemeji yako apate mbadala haraka. Wewe unayeandika nakuhisi una jinsia ya kike. Kumsaidia shemeji yako msaidie ampate mwingine--hata kama kwa ajili ya huruma tu ya kumsaidia ajirudi.
 
Unaona..! Inawezekana kuna sababu iliokuwa nje ya uwezo wao wakashindwa kuwa pamoja (as man & wife) sasa wanaendeleza mahaba yao.. Na jamaa yako awe makini mara nyingi mwanamke anaamua kumzalia mtoto huyo wake wa mahaba na jamaa yako akabaki kulea damu isio yake.. Mifano ya ukweli iko mingi sana ya haya nikuambiayo..

ila watu watakata tamaa kuoa mtu wa mbali
 
Jamaa avumilie maumivu huwa yanaisha,,kama uko kalibu nae na una kampani ya wadada wazuri2 uwe unamtoa out ukiwa na hao wadada watamsahaulisha machungu,,akimludia huyo kicheche bada ya watoto kama wa2 kuendelea anaweza rudia tena kumsaliti jamaa

out hataki na anakaa kwake sikae nae, mkitaka kumtoa out anakataa kbs
 
Poleni sana, jamaa anamaumivu ya kusalitiwa na fedheha aliyoipata mbele ya rafiki/jamaa na wafanyakazi wenzie ambao walimsaidia katika kufanikisha harusi yake, sasa pamoja na yote bado ofisini atakua hana raha, asiache kazi aombe transfer kwenda mkoa mwingine, ajipange upya kimaisha
 
Mpe pole lakini baada yakuandikisha alikua atoe displin ili atoe hasira ili kuondoa sumu pia afkirie je alimkuta bikra

displine ingemfikisha jela ni bora tu alipojinyamazia
 
nimechokaaaaa kabisa!!!
hapa hakuna njia sahihi sana ya kusaidia mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo.
ngoja nijaribu hivi
1.msimwache hata kidogo peke yake,kadri mda unavyoenda maumivu na msongo wa mawazo utapungua japo ni taratibu sana.
2.ushauri aendelee kupewa lakini msijipe matumaini makubwa,mana kukaa kwake kimya ni ishara ya maumivu makali sana,msongo wa mawazo na anachokiwaza anajua mwenyewe,ushauri unaweza kumwingia ama hapana.
3.binafsi nashauri baba na mama zake ndio wakae wampe matumaini na waonyeshe upendo kwa mwanao mana hao pekee ndio heros kwake baada ya tegemeo kwa mke kushindikana.WAZAZI WAMWONYESHE UPENDO NA UKARIBU MKUBWA.kama kuna dada zake pia wakae nae na kumpa matumaini,msisahau watu wazima na hekima zao wanaweza nao kusaidia.
4.msimulazimishe sana kufanya kazi kwa sasa kama hali yake ni mbaya sana,asije akagongwa hata gari,ama kupata ajali akiendesha mana atakuwa na mawazo.
5.depression is the best killer,kwa hiyo lazima muwe makini sana.
6.jitahidini kumubembeleza ale hata kidogo.
 
hahaha mie nawaambia watu ukweli wa mambo wao wanadhani mie napiga story tuu. kila leo hapa watu wanalalamika wamegegedewa wake au demu zao kisa wapo katika long distance relationship....learn from makosa ya wenzio sio unarudia makosa yale yale

ina maana wa mbali wasiolewe? ni tabia tu ya mtu sio wote
 
Dah! Almost copy and paste!! Usiombe yakukute!

Huyu alienda ghafla. Piga picha sasa . . . umempeleka wife likizo sehemu tena nje ya nchi kwa mapenzi yako> then ghafla bin vuu unamsikia wife akiongea na jamaa tofauti jinsi wanavyompa raha na jinsi anavyo wamiss na mambo mengine kibao jinsi wanavyomegana . . . grrrrrrrrrrrrrr

Mwambie jamaaa amtose tu kwa amani hakuna jinsi.

mwenyewe kashasema basi inatosha
 
ingekuwa inawezekana angejitokeza mdada mwenye huruma ampe company bila sharti lolote na aweze hata kukubali kulala naye anapohitaji hilo pasipo usumbufu mwingi wa hard to get. kuna mambo mengine dawa hailetwi na sheria, mahesabu-hesabu na kufikiri kwingi. mambo mengine dawa yake ni mapenzi tu. huyu mtu atakuwa anajihisi hapendeki, hatoshi, hatoshelezi, kadharauliwa kupita kipimo; gusa kitu chochote ambacho kinahesabika mali ya mwanamume, usiguse ile sehemu. ile sehemu ipo karibu sana ha kujiamini kwa mwanamume, kujipenda kwa mwanamume na mengine yote yanayohusu heshima ya mwanamume. siijui dharau kubwa mwanamke anaweza kumfanyia mwanamume kuzidi hii ya kutangaza kuwa mume huyo hatoshi. tiba ya huyu shemeji yako apate mbadala haraka. Wewe unayeandika nakuhisi una jinsia ya kike. Kumsaidia shemeji yako msaidie ampate mwingine--hata kama kwa ajili ya huruma tu ya kumsaidia ajirudi.

mmmh ni kweli lkn hili nalo gumu, unaza kumpatia jingine kumbe nalo tatizo si ndio atamalizika kbs? muda tu ukipita ataricover pole pole au lbda vidada vimmendee ila kumtafutia naogopa
 
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa!! Copy Prof jay! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii watanzania tunasifika na mataifa y anje kwa uzinzi, cheatings! Tupewe awards basi! Ila wanawake jamani tushoneni hizi nyapu zetu pulizzzzzzzzz, kha!
 
Last edited by a moderator:
Fanya kama unamuomba akusaidie kitu kwenye mizunguko yako ili mladi asikae peke ake,,na inashauliwa kazin aende ila asipewe kazi ngumu,,,itamfanya asiwaze jambo hilo2 tu,,,asikae nyumbani tu ni hatari zaidi
 
Poleni sana, jamaa anamaumivu ya kusalitiwa na fedheha aliyoipata mbele ya rafiki/jamaa na wafanyakazi wenzie ambao walimsaidia katika kufanikisha harusi yake, sasa pamoja na yote bado ofisini atakua hana raha, asiache kazi aombe transfer kwenda mkoa mwingine, ajipange upya kimaisha

labda hiyo ya transfer inweza saidia, lkn akikaa mbali si ndo atazidi kuwa mpweke sana? ndg zk wanaogopa asije commit suicide
 
Iruhisiwe kama wenzetu India mke mmoja wanaume wawili hadi wanne kama ilivyo ruhuswa kwa wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja na pia ndoa za mkataba ziwepo kuwe na kifungu kuainisha nini ch kufanya hasa kuzuia mafumanizi mf. Hakuna kuviziana kuchunguzana nk nk hii itasaidia kuondoa hii maneno
 
Aiseeeeeee!!!!! dah sipati picha hiyo hali. mimi namshauri wala asimsamehe huyo mke, bora asahau tu maisha yaende mbele, hafai kuwa mke wake huyo. Jamani mimi naogopa ndoa za kukaa mbalimbali kweli, mungu anisaidie tuu!!!
inavyoonyesha iko ivo, huyo mwizi ni mume wa mtu
 
Back
Top Bottom