Busha linaniua jamani naomba msaada!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,147
Busha Lenye Kilo 45 Lamtesa.. Aomba Msaada

6008614.jpg

Wesley Warren Jr
Wednesday, October 19, 2011 4:22 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ana busha lenye uzito wa kilo 45, busha hilo linamtesa sana kiasi cha kushindwa kutembea na hata kwenda chooni.
Wesley Warren Jr anateseka sana kutokana na busha linalomnyima raha na kumfanya ashindwe kuendelea na maisha yake ya kawaida.

Wesley ameanzisha kampuni ya kuchangisha watu pesa ili aweze kupata dola milioni moja ambazo ameambiwa azipeleke hospitali kwaajili ya gharama za operesheni ya kuliondoa busha hilo.

Wesley anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa scrotal elephantiasis. Busha lake ni kubwa sana lenye uzito wa kilo 45 kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na kupata tabu kwenda haja.

"Ni vigumu sana kutembea, kutwa nashindwa ndani", alisema Wesley.

Wesley mwenye umri wa miaka 47, anasema kuwa ingawa baadhi ya watu wanamcheka kutokana na hali yake, hajakata tamaa na aliamua kujitokeza kwenye vipindi vya televisheni na redio kuelezea hali yake ili kuomba msaada wa kuchangisha fedha za operesheni yake.

Hali aliyo nayo Wesley ni nadra sana kuiona kwenye nchi ambazo si za Tropiki zaidi ya Afrika na Asia, ambako ugonjwa huo husababishwa na maambukizi yanayosambazwa na mbu.

Wesley anasema kuwa hajawahi kusafiri kwenye nchi za tropiki na anaamini kuwa hali aliyo nayo inasababishwa na tukio lililotokea mwaka 2008 wakati alipozibana korodani zake katikati ya miguu yake wakati alipokuwa akijigeuza kitandani.

Wesley aliongeza kuwa siku iliyofuatia korodani zake zilivimba na kufikia ukubwa sawa na mpira wa soka.
 
Attachments

  • BUSHALIII.jpg
    BUSHALIII.jpg
    12.6 KB · Views: 110
Hilo ni busha au ni mtindo fulani wa kuvaa suruali kiroba??? Nevertheless, kama kweli ana busha aka shipa basi aje Tanzania, aende kule Rufiji kewenye mradi wa NIMR wa matende na mabusha atatibiwa, na tutakuwa tumekuza utalii.
 
Nimeona video yake nimeshangaa hasa maana wanasema virusi vinavyosababisha busha kikawaida havijaonekana mwilini mwake!
 
Busha Lenye Kilo 45 Lamtesa.. Aomba Msaada
6008614.jpg

Wesley Warren Jr
Wednesday, October 19, 2011 4:22 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ana busha lenye uzito wa kilo 45, busha hilo linamtesa sana kiasi cha kushindwa kutembea na hata kwenda chooni.
Wesley Warren Jr anateseka sana kutokana na busha linalomnyima raha na kumfanya ashindwe kuendelea na maisha yake ya kawaida.

Wesley ameanzisha kampuni ya kuchangisha watu pesa ili aweze kupata dola milioni moja ambazo ameambiwa azipeleke hospitali kwaajili ya gharama za operesheni ya kuliondoa busha hilo.

Wesley anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa scrotal elephantiasis. Busha lake ni kubwa sana lenye uzito wa kilo 45 kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na kupata tabu kwenda haja.

"Ni vigumu sana kutembea, kutwa nashindwa ndani", alisema Wesley.

Wesley mwenye umri wa miaka 47, anasema kuwa ingawa baadhi ya watu wanamcheka kutokana na hali yake, hajakata tamaa na aliamua kujitokeza kwenye vipindi vya televisheni na redio kuelezea hali yake ili kuomba msaada wa kuchangisha fedha za operesheni yake.

Hali aliyo nayo Wesley ni nadra sana kuiona kwenye nchi ambazo si za Tropiki zaidi ya Afrika na Asia, ambako ugonjwa huo husababishwa na maambukizi yanayosambazwa na mbu.

Wesley anasema kuwa hajawahi kusafiri kwenye nchi za tropiki na anaamini kuwa hali aliyo nayo inasababishwa na tukio lililotokea mwaka 2008 wakati alipozibana korodani zake katikati ya miguu yake wakati alipokuwa akijigeuza kitandani.

Wesley aliongeza kuwa siku iliyofuatia korodani zake zilivimba na kufikia ukubwa sawa na mpira wa soka.

Duh! hii balaa.., pole zake sana
 
Kuna msemao unasema hujafa hujaumbika ndio hayo !!!pole wesley
 
Huo ni ugonjwa mwingine tofauti na mabusha tuliyoyazoea huku pwani yetu.
Tumwombee mungu amsaidie kuondokana na mateso hayo.
 
Nimejikuta nacheka baada ya kutizama picha ya huyu jamaa.. Dah mzigo mzito hadi jamaa ameuweka kwenye stuli ilikupata sapoti...

Kweli jamaa anateseka sana na huo uvimbe maana chakula cha usiku hakiliki tena, kwa kweli anahitaji msaada...

Pdidy, nikihitaji kumchangia huyu jamaa nitumie njia ipi? Au una Mpesa yake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom