Bus la Ally's lagonga Kichwa cha Treni Manyoni Singida, Watu 13 wafariki Dunia, 25 wajeruhiwa

Pole sana kwa ndugu na jamaa wote waliopoteza wapendwa wao kwenye hiyo ajali.
Mungu awarehemu marehemu wote.

RISK ASSESSMENT AND CONTROL MEASURES.

Ningekuwa na mamlaka ningehakikisha kuanzia leo Tanzania haipati tena ajali za magari kugongana na train kama hivyo.

Ningetoa order kwamba katika kila sehemu yenye makutano ya railway na barabara za magari kuwe na flyover.

Full stop.
Uwezo huo upo, pesa zipo, Tanzania sio masikini.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Mkuu kabla ya kujenga hizo fly over, ungewaelimisha madereva wakiona Alana ya RAIWAY CROSSING wapunguze mwendo whatever the circumstances, iwe jua iwe mvua, iwe Kuna treni iwe Kuna baiskeli.
Pili matajiri waajiri responsible drivers waliopitia chuo Cha taifa Cha usafirishaji, madereva wasio Malaya, wasio vuta bangi Wala walevi.
KUNA SIKU NILIPANDA TAYASSAR KWENDA TANGA. KWA KWELI NILIFURAHI SANA. DEREVA HANA PAPARA, HAPENDI KUONGELESHWA NA KONDA. ANASEMA HIZO STORI UTANIAMBIA TUKIFIKA TANGA. BIG UP TAYASSAR BUS COMPANI NA NDUGU ZENU RAHALEO.
 
Jamii ambayo ajali zimekua desturi ya kawaida kabisa inayokubalika na jamii kila mwisho wa mwaka. Ati utasikia, "ni mwisho wa mwaka ajali ni kawaida".
Hii kauli ilinishangaza sana wakati fulani mwaka 2020.
 
Ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha Treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Mji wa Manyoni Mkoani Singida, imesababisha vifo vya Watu 13 na kujeruhi wengine 25.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema “Ajali imetokea leo Novemba 29, 2023 Saa 10 Alfajiri, basi lilikuwa na Watu 57, idadi ya majeruhi na vifo ni mpaka muda huu (asubuhi), kichwa cha Treni kilichohusika kina namba za usajili V1951-9006 kilikuwa kikitokea Itigi kuelekea Manyoni.”

============

Kwa masikitiko makubwa,, majonzi na huzuni naandika uzi huu kuwatangazia ajali mbaya iliyotokea eneo la Manyoni ukitoka Dodoma kabla ya kufika round about kati ya Bus la Allys lenye number ya usajili T 178 DVB na Kichwa Cha Train.

Sikupenda kupiga picha kutokana na hali ya huzuni, majonzi, kilio na maumivu makali ambayo wanapitia abiria manusura. Huku wakiwa wamezungukwa na maiti zikiwemo za watoto na watu wazima.

Ni hali ya kutisha mpaka kichwa cha train kimehama kabisa katika njia yake na bus limepinduka na kupondeka vibaya sana Ubavuni.

Police wanaendelea kuchukua manusura na maiti kupeleka Hospital ya karibu hapa Singida.

Chanzo inasemekana ni kichwa cha train kupita kikiwa hakijawasha taa wala kupiga horn. Na inasemwa hii si mara ya kwanza. Na mpaka hapo kichwa kinaonekana taa ikiwa haijawaka. Kinanguruma tu.

======

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, baada ya basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kugonga treni ya mizigo katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya mji wa Manyoni, mkoani Singida, leo Novemba 29, 2023 majira ya saa 11 alfajiri.

pole sana kwa wafiwa,
athari za mabasi kusafiri usiku zimeanza kuonekana.
Dreva wanatakiwa kuwa makini sana
 
Kama sikosei Kuna kipindi LATRA waliwafungia hii kampuni na KARSTAMU kusafirisha abiria usiku. Au nimekosea sio Hawa, na Kama Ni Hawa walijinasua lini na hiyo adhabu?
LATRA hebu simamieni maisha ya watanzania kwa weledi, mnalipwa na serikali kufanya hivyo.
Latra jukumu lao si kupandisha nauli tu au?
 
Afu kuna jamaa mmoja atasikika akisema kazi ya mola haina makosa.
 
T 178 DVB enzi za uhai wake
20231129_115118.jpg

Baada ya ajali
20231129_123703.jpg
 
Ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha Treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Mji wa Manyoni Mkoani Singida, imesababisha vifo vya Watu 13 na kujeruhi wengine 25.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema “Ajali imetokea leo Novemba 29, 2023 Saa 10 Alfajiri, basi lilikuwa na Watu 57, idadi ya majeruhi na vifo ni mpaka muda huu (asubuhi), kichwa cha Treni kilichohusika kina namba za usajili V1951-9006 kilikuwa kikitokea Itigi kuelekea Manyoni.”

============

Kwa masikitiko makubwa,, majonzi na huzuni naandika uzi huu kuwatangazia ajali mbaya iliyotokea eneo la Manyoni ukitoka Dodoma kabla ya kufika round about kati ya Bus la Allys lenye number ya usajili T 178 DVB na Kichwa Cha Train.

Sikupenda kupiga picha kutokana na hali ya huzuni, majonzi, kilio na maumivu makali ambayo wanapitia abiria manusura. Huku wakiwa wamezungukwa na maiti zikiwemo za watoto na watu wazima.

Ni hali ya kutisha mpaka kichwa cha train kimehama kabisa katika njia yake na bus limepinduka na kupondeka vibaya sana Ubavuni.

Police wanaendelea kuchukua manusura na maiti kupeleka Hospital ya karibu hapa Singida.

Chanzo inasemekana ni kichwa cha train kupita kikiwa hakijawasha taa wala kupiga horn. Na inasemwa hii si mara ya kwanza. Na mpaka hapo kichwa kinaonekana taa ikiwa haijawaka. Kinanguruma tu.

======

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, baada ya basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kugonga treni ya mizigo katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya mji wa Manyoni, mkoani Singida, leo Novemba 29, 2023 majira ya saa 11 alfajiri.

Dereva akamatwe anyongwe
 
Walikuwa kwenye mbio na basi la Happy Nation lililokuwa mbele yao

Davoo wa Happy Nation kamuuzia kicheche davoo wa Ally's

Happy Nation alivuka kwenye makutano ya barabara na reli fasta ila alishaiona treni ikija na huyu davoo wa Ally's naye akaforce, timing zikakataa wakala buyu
Hiki ndio chanzo halisi cha ajali walikuwa wanakimbizana.
 
Back
Top Bottom