Ajali ya Ally's ni uzembe wa dereva, uzembe wa mamlaka na kiburi cha waendesha Train

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Poleni sana wafiwa kwa kuwa inaonekana vifo ni vingi kuliko idadi tuliyoambiwa.

Inasemekana bus lilikuwa limejaa kwa maana ya abiria 60, lakini tumeambiwa vifo ni 13 na majeruhi 25 kwa maana kwamba idadi ya abiria walioripotiwa ni 37 tu.

Tunawaombea wote waliojeruhiwa wapone upesi.

Bila kumumunya maneno, nikiri wazi ajali hii imetokana na uzembe mkubwa wa dereva wa basi.Hakufuata sheria za barabarani. Alitembea mwendo kasi mkubwa bila kujali anapita kwenye kivuko cha treni.Hakuchukua tahadhari.Alijiachia kama vile yuko peke yake barabarani.

Mamlaka zinazodhibiti vyombo hivi,wamewaamuru wafunge VTS.Pamoja na kuwa mabasi yamefunga vifaa hivyo,bado wanavunja sheria kila siku kwa kutembea mwendokasi usioruhusiwa kisheria na wachache tu ndio hupewa adhabu.

Jamii tumejaa ujinga mwingi kwa sababu tuliaminishwa ajali haina kinga.Kutokana na huu msemo,uzembe unaruhusiwa na kuonekana ni kitu cha kawaida. Hata dereva wa train alipaswa kujua eneo hilo anapaswa kupiga honi tangu mbali kutoa tahadhari kwa madereva wazembe wa mabasi. Hata kichwa cha train kilipaswa kuwa na taa zenye mwanga mkali ili kutoa ishara ya tahadhari. hata hivyo unaweza kuta hata dereva wa train naye alikuwa amelala usingizi wa pono.

Mungu atusaidie waja wake

Soma:
- Bus la Ally's lagonga Kichwa cha Treni Manyoni Singida, Watu 13 wafariki Dunia, 25 wajeruhiwa
 
Nadhani kumlaumu dereva wa bus au wa train ni makosa, wote ni wahanga wa mifumo mibovu ya hii nchi, hasa upande wa train (TRC).

Kwa kawaida kwenye njia busy kama hiyo palipaswa pawe na taa za kuruhusu au kutokuruhusu gari kupita. Mi nipo na wa bus ndiye namuonea huruma na hana makosa kabisa.

Kibaya inawezekana pia aliliona akafunga brake karibu na lenyewe likamvuta au alijikuta yupo katikati gari ikavutwa. Kwa ufupi TRC ndiye wanatakiwa wawajibike. Yaani hii kesi kwa wanasheria kama kuna ndugu wana hela TRC wanalipa kabisa!
 
1701296358125.png
1701296358125.png
 
Wote hawapaswi kulaumiwa kwasababu kifo ni deni, na hilo deni hata ukimbie vipi nilazma tu utalilipa, hata kama angejua treni lonakuja, bado hii tungetafsiri kuwa anakwepa deni, ila dawa ya deni ni kulipa.

R.i.p wote
 
kujua eneo hilo anapaswa kupiga honi tangu mbali kutoa tahadhari kwa madereva wazembe wa mabasi. Hata kichwa cha train kilipaswa kuwa na taa zenye mwanga mkali ili kutoa ishara ya tahadhari
Mkuu kuna hizo sehemu za reli ukikaribia zinafungwa km kuna treni inakuja.
Sasa wale wazembe hata pakifungwa ye anapita hivyohivyo ndo maana inaandikwa kagonga treni.
 
Nadhani kumlaumu dereva wa bus au wa train ni makosa, wote ni wahanga wa mifumo mibovu ya hii nchi, hasa upande wa train (TRC).

Kwa kawaida kwenye njia busy kama hiyo palipaswa pawe na taa za kuruhusu au kutokuruhusu gari kupita. Mi nipo na wa bus ndiye namuonea huruma na hana makosa kabisa.

Kibaya inawezekana pia aliliona akafunga brake karibu na lenyewe likamvuta au alijikuta yupo katikati gari ikavutwa. Kwa ufupi TRC ndiye wanatakiwa wawajibike. Yaani hii kesi kwa wanasheria kama kuna ndugu wana hela TRC wanalipa kabisa!
Likamvuta? Kitu gani kilichomvuta? Kwamba kichwa cha Garimoshi kinavuta vyuma? Huu utoto sasa
 
SWALI: 60

Vifo 13

Majeruhi 25

Je, vifo vilikuwa vingapi?

KAZI: Abiria 60-vifo 13-majeruhi 25= 22

Jibu: kwa hiyo, 13+22=35?
 
Hiyo basi imegongwa na treni,ila kwa tafsiri ya sheria yao ni kwamba basi ndio limegonga treni,lakini kiuharisia ukiangalia basi limegongwa eneo la ubavuni,bila shaka alikuwa katikati ya reli

Pasua kichwa;Hii kusema kuwa treni haikuwasha taa wala kupiga honi kwa mazingira ya kawaida injini ya treni ina muungurumo mkubwa na sauti hata bila honi ni wazi muungurumo unasikika
Yote haya yashatokea,tuwaombee marehemu zetu pamoja na manusura.
Amin.
 
SWALI: Abiria walikuwa 60

Vifo 13

Majeruhi 25

Je, vifo vilikuwa vingapi?

KAZI: Abiria 60-vifo 13-majeruhi 25= 22

Jibu: kwa hiyo, 13+22=35?
Ninavyodhani mie kuna vifo,majeruhi na manusura.
Inawezekana hiyo idadi isiyoonekana labda ipo kwenye manusura
Maana ukiangalia sehemu ya nyuma ya Basi wala haijaharibika sana.
 
Nadhani kumlaumu dereva wa bus au wa train ni makosa, wote ni wahanga wa mifumo mibovu ya hii nchi, hasa upande wa train (TRC).

Kwa kawaida kwenye njia busy kama hiyo palipaswa pawe na taa za kuruhusu au kutokuruhusu gari kupita. Mi nipo na wa bus ndiye namuonea huruma na hana makosa kabisa.

Kibaya inawezekana pia aliliona akafunga brake karibu na lenyewe likamvuta au alijikuta yupo katikati gari ikavutwa. Kwa ufupi TRC ndiye wanatakiwa wawajibike. Yaani hii kesi kwa wanasheria kama kuna ndugu wana hela TRC wanalipa kabisa!
Wewe unatetea uzembe wa dereva? Kwani yeye ni mgeni wa njia? Hakujua kama hakuna taa unazozisema? Mbona alama za railway crossing zipo? Haikumpasa kusimama kwanza kujiridhisha kama kuna usalama?
 
Back
Top Bottom