Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

Katika Jambo ambalo Nyerere alikosea ni Kuruhusu mambo ya kipuuzi kama haya pia Yatokee kwa watoto zake lakini pia Hakufanya jitihada za wazi kuwainua watoto zake kabisaa.. leo hii mtoto wa mwinyi anakuwa Rais wa nyerere hata Ubunge anakosaa...!! Legacy ya Urais aliondoka nayo mwenyewe watoto zake hawakufaidika hata kiodgo na potential ya baba yao mpaka Inafikia kipindi Lectures wanamdico mtoto wa Rais Nasema wangetafuta kazi ya Kufanyaa maza fakazzz tena sio tanzania idiots kabisaa... uprofesa ushuzi huko huko kwao.
Alafu wazee wengi wa zamani ndio zilikua itikadi zao. Hata kama tajiri, anakwambia mali ni zake, wewe ukuwe utafute vyako hana mpango na wewe. Ingekua mambo haya ya sasa nadhani mbaka kina edward nyerere wangekua mawaziri sahivi
 
Kwanza pale UD ilijengeka tabia ya kudhani kwamba wasomi wa sayansi hasa engineering ndio wasomi hasa, hi kitu imebadirka sana juzi kati tu hapo baada ya Kikwete kuingia madarakani, alipoweka makamu mkuu wa chuo Ngwini, kina profesa Matthew Luhanga waliwajengea akilini wanafunzi wa sayansi kua ndio hasa vipanga na hi pia ilipelekea hata wahadhiri wa masomo hayo sometimes wamefelisha sana wanafunzi makusudi hasa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90; sio kweli kwamba mara zote wanafunzi ni wazembe, mara nyingi wamefelishwa makusudi.
Hii ni ya zamani sana lakini nimeona isiruhusiwe kuendelea kueneza uwongo bila kupingwa kwani unajenga hisia ya kuwa UDSM ilikuwa ni ya kipindi wewe uko pale tu chini ya Luhanga bila kuwa na picha kubwa cha chuo. Kulingana na record za University of Dar es Salaam- mkuu wa kwanza wa chuo kikuu cha Dar es salaam tangu bado ikiwa ni College of East Africa alikuwa ni Ngwini (Dr Cranford Pratt) wa political Science. Huyu alifuatiwa na mganga wa biandamu (Dr WIlbert Chagula) ambaye aliondoka kwenye kiti hicho mwaka 1970 alipochaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa na Nyerere kuwa waziri wa Maji na Nguvu za Umeme (wakati huo). Kuanzaia mwaka 1970 hadi 1991 ambayo ni miaka 21 maVC wote wa wa UDSM ukianzia na Kaduma, Msekwa, Kuhanga na Mmari, wote walikuwa ni ngwini. Hata hivyo kipindi hicho ndicho ambachoo ndipo UDSM ilikuwa maarufu sana kwa Supps zikiitwa Cancun Conferences na madisco kibao. Vile vile ndipo wakati ambapo UDSM ilivutia wanazuoni maarafu sana sana kama akina Wadada Nabudere (Uganda), Mahamood Mamdani (Uganda), Walter Rodney (Guyana), Ali Mazrui (Kenya), Euphrace Kezirahabi (Tanzania) na wengine wengi.

Ingawa Luhanga alikaa madarakani muda mrefu sana, mchango wake (pamoja na Prof Mbwete ) ni kufanya transformation ya kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 3,800 hadi 18,000 na kuingiza siasa hizi za kuingilia maamuzi ya waalimu ili kupunguza percentages za disco. Wakati Luhanga anaanza madaraka tu mwaka 1991 niliwahi kuitwa na Prof Mrama ambaye ndiye alikuwa Chief Academic Officer wakati huo nijibu malalamiko ya mtoto mmoja aliyekuwa amedisco kwa kufeli masomo zaidi ya matatu, mojawapo likiwa la kwangu. Baada ya kumpa data, Mama Mrama akakubaliana na data nilizoweka mbele yake, yule mtoto akadisco ingawa alipata nafasi ya kujiunga na IDM Mzumbe wakati huo na kupasaua sana kwa diploma ya ADCA ya wakati huo.

Katika maisha yangu ya UDSM, nadhani viongozi nitakaowakumbuka sana ni Professor Mmari, Professor Msuya, Professor Mkude, Professor Mrama, na Professor G-Mgongo Fimbo.
 
Sio tu akiwa hai bali akiwa Rais wa nchi

Kuna Mkuu wa Shule alimpiga barua ya kumwita Mzazi mtoto wa Nyerere, alipofuatwa kuulizwa akajibu nimemuita Julius Nyerere Mzazi wa Mwanafunzi sio Rais

Huyo ni Mama Siwale alikuja kupata Uwaziri wa Elimu

Baadae nae akaja kutumbuliwa kwa kosa la kupeleka Uwaziri chumbani akiwa na Mumewe

The rest is history
Unanikumbusha TAMBAZA mtoto wa mkuu wa Majeshi mwanae na wengineo walifanya Fujo walipigana na wanafunzi wa JITEGEMEE sijui AZANIA vile wakaumizan vibaya basi wakasimamishwa shule wakaambiwa wawaite wazazi wao waje nao
Huyo mtoto hakuna aliyejua kama ni mtoto wa mkuu wa MAJESHI
Ahmad MKUU WA MAJESHI huyo na walinzi wake Shule nzima macho pima MKUU WA MAJESHI kaitikia wito wa MZAZI
kufika kakaa anasubiri KIKAO CHA WAZAZI kianze mwalim mkuu hayupo anauliza kaenda wapi
Jibu kapewa kaitwa na WAZIRI WA ELIMU
akauliza kwa hiyo WAZIRI WA ELIMU ni muhimu kuliko wito alotuita sisi kiasi kashindwa kwenda muda mwingine
Mimi nimeitwa na RAISI(EDHI hizo Raisi mwinyi) na sijaenda nimeitikia wito wa MWALIMU kama mzazi
Inamaana huyu MWALIMU ametudharau sana sisi WAZAZI kwa kutupotezea muda
sasa akija umwambie yeye aje kwa kila mzazi nyumbani kwake kuongea nae ama lah kama hawezi jumatatu WATOTO wote warudi shule

Umenikumbusha mbali sana
 
Nimeshangaa umesema mcheshi wakati alipokuwa mbunge hakuwahi kuongea chochote hadi anamaliza ubunge.

Sikuwahi kujua alifika UDSM

Interesting
Aliwahi kutoa mchango wake bungeni juu ya viongozi wa Sengerema waliokuwa wanafyeka mahindi ya wakulima eti kuzuia mazalia ya mbu mjini... Alihoji sera ya kilimo nchini ni Kilimo Kwanza au Mbu Kwanza. Bunge Iote waliangua vicheko na makofi. Shida yetu hautufuatilii Bunge.
 
Kwa wale tulioingia Chuo Kikuu cha Dar-es –Salaam faculty of Medicine enzi hizo intake ya mwaka 1982 tutamkumbuka ndugu yetu huyu mcheshi sana Rosemery Nyerere.

Miaka hiyo intake moja ilikuwa inachukua wadahiliwa 50 na majina yote tulikuwa tunayakuta kwenye gazeti la Daily News, gazeti la serikali. Basi mwenzetu huyu alifanikiwa kuwa mojawapo wa wateule wachache waliofanikiwa kuingia katika intake ya mwaka 1982 July. Katika intake hiyo tuliofanikiwa kumaliza tulikuwa 24, wengine either walidsco, waliacha tu au walibadilisha course jukwaju.

Rosemary Nyerere hakufanikiwa kumaliza kwani walimdiscontinue mwaka wa pili. Baada ya hapo aliajiriwa Print park kama sikosei.

Wakati huo Dean of Faculty alikuwa ni Professor Honnoli sijui kama yuko hai, siyo kwamba Rosemary Nyerere alidisco hivihivi bali figisu zilitaka kufanyika ili aendelee lakini nakumbuka kuna Lecturer mmoja toka Jamaica alisimama kidedea mpaka Rosemary aling`oka, nakumbuka kama alikamatwa masomo mawili.

Timu wa walimu wetu enzi hizo ninaowakumbuka ni Professor Massawe, Mwaluko, Makene, Karashani, Kimati, Hiza, Msele na Shaba hawa ndo ninawakumbuka.

Tulikuwa tukiishi Muhimbili na kula cafeteria chakula kizuri kweli ambacho kwa sasa hata mkurugenzi hali, Mfano wali kwa kuku na saa nyingine kuku wa kukaanga, ugali na mbogamboga n.k

Rosemary hakuwa kabisa na mbwembwe zozote kama watoto wa Ma-rais wa sasa kama Yule wa Chalinze, alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa na wala usingemdhania ni mototo wa Rais. Cha kushangaza watoto wa mameneja wakati huo ndo walikuwa wanatisha mfano kuna mtoto alikuwa ni wa meneja wa RTC akuwa anakuja na gari Peugeot 504.

Kama Rosemary Nyerere ametangulia mbele za haki basi Mungu amlaze mahala pema na ninakumbuka kama aliwahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa au Viti Maalumu mwaka 2000-2005.
Mbona hujaweka chanzo cha habari yako. Au unataka kutuaminisha ww ndio uliupiga nae? Kwa uandishi huu mhh napata ukakasi
 
Nimeshangaa umesema mcheshi wakati alipokuwa mbunge hakuwahi kuongea chochote hadi anamaliza ubunge.

Sikuwahi kujua alifika UDSM

Interesting
Aliwa hi na ali kuwa na kinzana sana na Waziri Rita Mlaki kwnye maswali na majibu. Nina kumbuka wakati bado nina ujiko wa cheo cha babangu , nilikutana naye hapo JKN airport VIP, mimi nilikuwa na mama yangu tuna safiri kwenda UK na yeye alikuwa ana kwenda Cuba , tulisafiri ndege moja tukaachana Amsterdarm ninadhani alikuwa na mume huko CUba na kipindi hich alikua mkono wake bado ume fungwa hogo baada ya kuvamiwa na majambazi na kumjeruhi mkono .
 
Sema ukweli kuwa alikuwa shemeji yetu bwana we mbona umezunguka sana. Pole ndugu yetu Kwa kufiwa na shemeji yetu
 
Unanikumbusha TAMBAZA mtoto wa mkuu wa Majeshi mwanae na wengineo walifanya Fujo walipigana na wanafunzi wa JITEGEMEE sijui AZANIA vile wakaumizan vibaya basi wakasimamishwa shule wakaambiwa wawaite wazazi wao waje nao
Huyo mtoto hakuna aliyejua kama ni mtoto wa mkuu wa MAJESHI
Ahmad MKUU WA MAJESHI huyo na walinzi wake Shule nzima macho pima MKUU WA MAJESHI kaitikia wito wa MZAZI
kufika kakaa anasubiri KIKAO CHA WAZAZI kianze mwalim mkuu hayupo anauliza kaenda wapi
Jibu kapewa kaitwa na WAZIRI WA ELIMU
akauliza kwa hiyo WAZIRI WA ELIMU ni muhimu kuliko wito alotuita sisi kiasi kashindwa kwenda muda mwingine
Mimi nimeitwa na RAISI(EDHI hizo Raisi mwinyi) na sijaenda nimeitikia wito wa MWALIMU kama mzazi
Inamaana huyu MWALIMU ametudharau sana sisi WAZAZI kwa kutupotezea muda
sasa akija umwambie yeye aje kwa kila mzazi nyumbani kwake kuongea nae ama lah kama hawezi jumatatu WATOTO wote warudi shule

Umenikumbusha mbali sana
Siku hizi Walimu kazi ya awali baada ya kupokea Mwanafunzi mpya ni kuuliza kazi ya Wazazi ili ageuke chawa wa Mwanafunzi
 
Hii ni ya zamani sana lakini nimeona isiruhusiwe kuendelea kueneza uwongo bila kupingwa kwani unajenga hisia ya kuwa UDSM ilikuwa ni ya kipindi wewe uko pale tu chini ya Luhanga bila kuwa na picha kubwa cha chuo. Kulingana na record za University of Dar es Salaam- mkuu wa kwanza wa chuo kikuu cha Dar es salaam tangu bado ikiwa ni College of East Africa alikuwa ni Ngwini (Dr Cranford Pratt) wa political Science. Huyu alifuatiwa na mganga wa biandamu (Dr WIlbert Chagula) ambaye aliondoka kwenye kiti hicho mwaka 1970 alipochaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa na Nyerere kuwa waziri wa Maji na Nguvu za Umeme (wakati huo). Kuanzaia mwaka 1970 hadi 1991 ambayo ni miaka 21 maVC wote wa wa UDSM ukianzia na Kaduma, Msekwa, Kuhanga na Mmari, wote walikuwa ni ngwini. Hata hivyo kipindi hicho ndicho ambachoo ndipo UDSM ilikuwa maarufu sana kwa Supps zikiitwa Cancun Conferences na madisco kibao. Vile vile ndipo wakati ambapo UDSM ilivutia wanazuoni maarafu sana sana kama akina Wadada Nabudere (Uganda), Mahamood Mamdani (Uganda), Walter Rodney (Guyana), Ali Mazrui (Kenya), Euphrace Kezirahabi (Tanzania) na wengine wengi.

Ingawa Luhanga alikaa madarakani muda mrefu sana, mchango wake (pamoja na Prof Mbwete ) ni kufanya transformation ya kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 3,800 hadi 18,000 na kuingiza siasa hizi za kuingilia maamuzi ya waalimu ili kupunguza percentages za disco. Wakati Luhanga anaanza madaraka tu mwaka 1991 niliwahi kuitwa na Prof Mrama ambaye ndiye alikuwa Chief Academic Officer wakati huo nijibu malalamiko ya mtoto mmoja aliyekuwa amedisco kwa kufeli masomo zaidi ya matatu, mojawapo likiwa la kwangu. Baada ya kumpa data, Mama Mrama akakubaliana na data nilizoweka mbele yake, yule mtoto akadisco ingawa alipata nafasi ya kujiunga na IDM Mzumbe wakati huo na kupasaua sana kwa diploma ya ADCA ya wakati huo.

Katika maisha yangu ya UDSM, nadhani viongozi nitakaowakumbuka sana ni Professor Mmari, Professor Msuya, Professor Mkude, Professor Mrama, na Professor G-Mgongo Fimbo.
Heshima sana kwako mkuu Kichuguu.
 
Hapana she was far from Newton

Muhimu kujua hawakutelekezwa

Alipewa ubunge .. angekuwa active angepewa zaidi vyeo vingine.

But alikuwa so silent
Wanaojua wanasema alipopata Ubunge alikua na sonona la moyo...
 
Back
Top Bottom