Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,689
Kwa wale tulioingia Chuo Kikuu cha Dar-es –Salaam faculty of Medicine enzi hizo intake ya mwaka 1982 tutamkumbuka ndugu yetu huyu mcheshi sana Rosemery Nyerere.

Miaka hiyo intake moja ilikuwa inachukua wadahiliwa 50 na majina yote tulikuwa tunayakuta kwenye gazeti la Daily News, gazeti la serikali. Basi mwenzetu huyu alifanikiwa kuwa mojawapo wa wateule wachache waliofanikiwa kuingia katika intake ya mwaka 1982 July. Katika intake hiyo tuliofanikiwa kumaliza tulikuwa 24, wengine either walidsco, waliacha tu au walibadilisha course jukwaju.

Rosemary Nyerere hakufanikiwa kumaliza kwani walimdiscontinue mwaka wa pili. Baada ya hapo aliajiriwa Print park kama sikosei.

Wakati huo Dean of Faculty alikuwa ni Professor Honnoli sijui kama yuko hai, siyo kwamba Rosemary Nyerere alidisco hivihivi bali figisu zilitaka kufanyika ili aendelee lakini nakumbuka kuna Lecturer mmoja toka Jamaica alisimama kidedea mpaka Rosemary aling`oka, nakumbuka kama alikamatwa masomo mawili.

Timu wa walimu wetu enzi hizo ninaowakumbuka ni Professor Massawe, Mwaluko, Makene, Karashani, Kimati, Hiza, Msele na Shaba hawa ndo ninawakumbuka.

Tulikuwa tukiishi Muhimbili na kula cafeteria chakula kizuri kweli ambacho kwa sasa hata mkurugenzi hali, Mfano wali kwa kuku na saa nyingine kuku wa kukaanga, ugali na mbogamboga n.k

Rosemary hakuwa kabisa na mbwembwe zozote kama watoto wa Ma-rais wa sasa kama Yule wa Chalinze, alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa na wala usingemdhania ni mototo wa Rais. Cha kushangaza watoto wa mameneja wakati huo ndo walikuwa wanatisha mfano kuna mtoto alikuwa ni wa meneja wa RTC akuwa anakuja na gari Peugeot 504.

Kama Rosemary Nyerere ametangulia mbele za haki basi Mungu amlaze mahala pema na ninakumbuka kama aliwahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa au Viti Maalumu mwaka 2000-2005.
 
Hapana she was far from Newton

Muhimu kujua hawakutelekezwa
Alipewa ubunge .. angekuwa active angepewa zaidi vyeo vingine..
But alikuwa so silent
Ninavyosikia ni wale watu ambao wako down to the earth, wapole na wasiopenda ''viti vya mbele''. Hata huo ubunge alikuwa haupapatikii kama hawa wanasiasa wengine la sivyo angefia kwenye ubunge.
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom