Buriani Mzee Nalaila Lazaro Kiula; Mwadilifu aliyeponzwa na Mfumo kifisadi

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,396
Usiku wa kuamkia Jana amepumzika Mzee Nalaila Lazaro Kiula. Alipata kuwa Mbunge wa Zamani wa Iramba, na Waziri wa zamani wa Ujenzi na Mawasiliano, Naibu wa Waziri wa Elimu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Mzee Kiula ni mojawapo ya Wahanga wa siasa za fitna, majungu na mitandao ndani ya CCM.

Akiwa ktk kiwango Bora Cha Utendaji ktk Awamu ya Pili. Mzee Kiula alionekana ni tishio kwa wanamitandao watafuta Urais, ndipo alipoanza kuwindwa na akanasa ktk Sakata la kutumia vibaya madaraka na kupata msukosuko wa mkubwa uliompoteza kisiasa,!

Pamoja na uzuri wa Ripoti ya Warioba kuhusu Rushwa inashangaza eti ni Mwanasiasa mmoja TU ndiye alionekana ni mla rushwa! ..Kiula! Of all the People!?

Pamoja na misukosuko yote aliyopata Mzee Kiula aliendelea kuwa mwaminifu Kwa CCM Hadi umauti!

Mara kadhaa aliombwa apewe shavu CHADEMA, lakini alikataa kukisaliti chama chake!

Nafikiri ni Waziri pekee wa enzi za Mwinyi aliyeishi maisha ya kawaida ya Mtanzania hadi umauti!

Wengine wakisikia haya watakumbuka udhaifu wa kibinadamu wa Nalaila! Ukiwaza hayo kumbuka histori ya Mfalme Daudi!

Nenda kapumzike Mzee Kiula ,huu ndio mwisho wako wa kujiuliza ...Niliwakosea nini!
 
Apumzike kwa amani Mzee Kiula na Poleni sana mkuu...

Hivi Kiula alifungwa pamoja na Katibu mkuu wa ujenzi enzi zile? Au ilikuwaje? Tukumbushe mkuu
 
Yaani alikula rushwa ya ujenzi barabarani ya kwenda kwa, ndio kitu Kilchowashangaza
 
Nakumbuka uteuzi wa mzee Kiula kuwa waziri wa ujenzi na mawasiliano.

Magazeti pia yalimpa kichwa cha habari kisemacho "Nalaila Kiula aula".

Ni kwamba tu kwa sasa hakuna vyombo vya habari vyenye uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa.

Ilitakiwa ifanyike tathmini ya ule wizi wa Ujenzi na kule ATC kwa marehemu Ernest Mwenewanda.

Vyombo vya habari vya Tanzania vimelala usingizi wa pono.

RIP mzee Nalaila Kiula.
 
Nakumbuka uteuzi wa mzee Kiula kuwa waziri wa ujenzi na mawasiliano.

Magazeti pia yalimpa kichwa cha habari kisemacho "Nalaila Kiula aula"...
Vyombo vya habari viliwahi kufanya Uchunguzi dhidi ya Magu kujiuzia nyumba za serikali na kugawia mdogo wake na vimada wake.

So vyombo havijalala.
 
..Msikilizeni Nalaila Kiula akizungumzia kilichomtokea.

Akizungumzia kesi ya tuhuma za rushwa dhidi yake, alidai ilipandikizwa kwa chuki binafsi za Rais Mkapa kutokana na umaarufu aliokuwa nao wakati huo.

“Wakati Mzee Mwinyi ananiteua kuwa Waziri wa Ujenzi alinisifu sana kuwa ni kijana mchapakazi na mwadilifu na alikuwa akinisifu mara kwa mara sasa naona hapo ikawa nongwa na gere,“ alidai Bw. Kiula ambaye mpaka mwaka 2000 alikuwa Mbunge wa Iramba...
 
Back
Top Bottom