EDO KUMWEMBE: Mzee Kikwete anapokesha kumsubiri Lunyamila mwingine

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
1687964337287.png

ZAMANI mzee Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kupigwa picha akipanga foleni kuingia katika pambano moja la timu yake aipendayo Yanga. Wakati ule alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Alipenda zaidi soka na kikapu.

Akizungumzia kitu kuhusu michezo anazungumzia kitu anachokifahamu. Majuzi nilikuwa namsikitikia mzee wangu akishangazwa namna ambavyo vipaji vya kigeni vimetawala nchini kwa sasa. Kina Clatous Chota Chama, kina Fiston Mayele, kina Djigui Diarra na wengineo.
Alizungumza kutoka moyoni. Akawataka viongozi wajitafakari. Kwanini wasifiwe wageni tu? Kwanini vipaji vile havipo tena? Ni topiki pana. Topiki mtambuka. Sidhani kama viongozi wa michezo ndio ambao wanapaswa kulaumiwa au kujitafakari katika hili.

Mzee Kikwete aliwahi kuwaona kina Sunday Manara, Hamis Gaga, Edibily Lunyamila, Hussein Marsha na wengineo. Ni kweli walikuwa na mfumo imara wa kuibuliwa? Sidhani kama kulikuwa na mifumo imara. Hakukuwa na shule za soka badala yake kulikuwa na michuano ya shule za sekondari.
Lakini hata leo, kwa kupitia mfumo huohuo kuna michuano mingi ya vijana. Swali, kwanini hatuwapati kina Lunyamila wengine? Hapa kuna majibu magumu. Tunaanzia kwa wachezaji wenyewe. Nadhani wana kesi nzito ya kujibu kuliko viongozi.
Binafsi naamini kwamba inaanzia kwa mchezaji binafsi. Hili ni suala la mchezaji binafsi. Ni suala la maisha yake binafsi. Ni suala la kupuuza kila mkwamo na kuamua kupambana kwa ajili ya maisha yako binafsi. Sio suala la jamii. Siku hizi maisha yetu ya familia sio ya jamii. Una jukumu lako la kulipambania.
Hapa ndipo ninapomkumbuka baba yangu Sunday Manara. Siku moja nilimtembelea nyumbani kwake pale Temeke. Aliniambia kitu ambacho ndicho msingi wangu wa mkubwa ninapowatofautisha wachezaji wa zamani na wachezaji wa sasa. Wakati huo kina Athuman Idd ‘Chuji’ walikuwa katika fomu.

Mzee Manara aliniambia kwamba tofauti ya wachezaji wa zamani wa enzi zao na hawa wa sasa ni kwamba wachezaji wa zamani walikuwa wanacheza asilimia 80 ya uwezo wao wakati hawa wa sasa wanacheza asilimia 20 tu ya uwezo.
Mzee Manara aliniambia kwamba vipaji ni vilevile na bado vipo lakini kinachowatofautisha wao na hawa wa sasa ni vitu kama stamina, nguvu, kasi na kadhalika. Nilijaribu kumuelewa Mzee Sunday. Nchi ambayo imewahi kutoa wachezaji mahiri kwanini wasizaliwe wengine mahiri?
Ni kweli haiwezekani ghafla India ikaanza kutoa wanasoka wazuri kama Brazil. Hawana vinasaba vya soka na wala soka sio mchezo namba moja nchini kwao. Kwa Tanzania haiwezekani kama tuliwahi kumtoa Sunday Manara tukashindwa kuendelea kuwatoa akina Sunday wengine. Mbona Mbwana Samatta amekwenda Ulaya na akatamba na sio mchezaji wa zamani?
Wachezaji wanashindwa kujiongeza na kujiamini. Mzee Kikwete akumbuke kwamba hawa wageni sio kwamba wanapendelewa. Wanapambania nafasi zao kuanzia mazoezini hadi katika mechi. Wakati mwingine hata wenyewe kwa wenyewe huwa wanapambania nafasi zao katika timu zetu.
Mfano ni namn ambavyo Mayele aliweza kumuondoa katika nafasi Herritier Makambo. Nilianza kuhisi jambo hili lingetokea wakati nikiwa katika kambi ya mazoezi ya Yanga pale Morocco. Mayele alionekana kupania na kuwa fiti kuliko Makambo.
Lakini hapa hapa tukirudi kwa wazawa. Kuna mshambuliaji gani yuko fiti kama Mayele? Achilia mbali suala la kufunga mabao, nazungumzia suala la kuwa fiti. Ni wazi kwamba utahisi kuwa Mayele ana mazoezi ya ziada lakini pia anajitunza vema. Ni tofauti na ilivyo kwa wachezaji wetu walio wengi ambao wanapenda kukesha instagram.

Lakini Mzee wetu Kikwete anapaswa kukumbuka kwamba kuna wazawa ambao wamejihakikishia nafasi katika klabu hizi. Nafasi hizi hazijaja kama zawadi kwao. Pale Simba kuna kipa wao, Aishi Manula pamoja na walinzi wa pembeni, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe.
Pale Yanga wana walinzi wao wa kati Dickson Job, Bakari Mwamunyeto na Ibrahim Bacca. Wanakaba kama vile kesho haipo. Wamejitafuta wamejipatia uhakika wa nafasi. Hawa Simba na Yanga katika miaka ya karibuni wamefika mbali katika michuano ya Afrika wakiwa na wachezaji hawahawa.
Kwanini tusipate wachezaji wengine kama hawa katika maeneo mengine ya uwanja? Mzamiru Yassin na Fei Toto walijitengenezea umuhimu mkubwa katika eneo la kiungo, kwanini tusipate wachezaji wengine katika kila eneo.
Tatizo ni kwamba wachezaji wetu binafsi hawajitumi kuwa fiti, hawafuati miiko ya mpira lakini pia hawana ubunifu wa kujifunza mchezo wenyewe ulivyobadilika. Na hii sio kwa wachezaji wa Ligi kuu tu, bali hata vijana wanaotazamiwa kuja kuchukua nafasi zao. Na ndio maana hatuoni moja kwa moja wabadala wa akina Kapombe.
Huyu mlinzi wa Yanga anayeitwa Bacca nimemchunguza vizuri. Yuko imara katika mipira ya juu, yupo imara katika ‘tackling’, yupo imara katika ukabaji, yupo imara katika kusambaza mipira ya chini. Yupo imara katika kila idara. Hata hivyo kila kitu anakifanya kwa ufasaha kwa sababu yupo fiti sana.
Binafsi naamini kwamba vijana wa sasa wana mazingira mazuri zaidi ya kujiandaa kuliko vijana wa zamani. Siku hizi kuna gym ,viwanja vizuri, wanavaa viatu vizuri, raba nzuri za mazoezi, na kila kitu. Sidhani kama kina Hamis Gaga walikuwa katika mazingira haya.

Tatizo ni wao wenyewe kabla ya uongozi. Tena wana bahati ya kutazama mechi nyingi za soka ulimwenguni kote. Wana bahati hata ya kutamanishwa mishahara mizuri ya wachezaji ndani na nje ya uwanja. Mpira upo katika mahakama yao.
Wachezaji wengi wa Afrika Magharibi wanapambana wenyewe. Ni wapiganaji hasa. Wapo kwa ajili ya kuziokoa familia zao. wanatoka katika mazingira magumu ya kisoka kuliko wachezaji wetu. Tunaona jinsi ambavyo mastaa wao wakubwa wanaporudi katika nchi zao wanaungana nao kucheza katika viwanja vya vumbi.
Lakini hapo hapo tujiulize, ni kweli mfumo wetu ulimuandaa Samatta kwenda kucheza katika Ligi Kuu ya England? Hapana. Alijiandaa mwenyewe baada ya kupata kiu ya kufika mbali. Hawa wanasoka wetu wazawa wanadeka wenyewe.
Kama kweli wanakosa nafasi ya kujiunga na timu kubwa kama Azam, Yanga na Simba, tujiulize wanazifanyia nini timu za kawaida ambako wamejaa wengi tu. mbona huko wanapata nafasi lakini wanashindwa kufanya mambo makubwa?

CREDIT: MWANASPOTI
 
View attachment 2671955

Huyu Kumwembe ni moja ya watu wa ajabu ambao wamepewa nafasi ya kunajisi tasinia ya habari. Anavyosema zamani kulikuwa hakuna mfumo mzuri wa kutengeneza wachezaji naona ni kituko. Hivi Eddo anaweza kutoa hata mfano mmoja wa mechi aliyoweza kuwepo uwanjani? hivi anajua hata historia ya mpira vizuri huyu?
 
Hajaliona tatizo badala yake kaongea nadharia
1.Viwanja kwa Sasa hakuna
2.Watoto wanatumia mda mwingi kusoma kuliko kucheza.
3.Tv zinawafanya watoto wakae chini au kwenye viti mda mrefu
4.Vifaa vya michezo vipo ila ni ghali sana na kiwango Cha umaskini ni kikubwa
5.Jamii haiamini katika michezo ni rahisi kwa anaecheza kuonekana anapoteza mda.
6.Dhurma michezoni kwa wazawa ni kubwa
7.Elimu ya michezo haipo kwa walimu na wachezaji (tazama sakata la dube na Azam lilivyoisha kirahisi)naamini imechangiwa na elimu kwa dube na Wala sio ustaraabu kwa azam maana ndio wao waliocharurana na kina sure boy na muda wakati flani.
 
President Kikwete naye ni sehemu kubwa ya tatizo hili, yeye alifanya juhudi gani kuona vipaji vya athletics wetu vinaboreshwa?au ndio yale yale kakaa kwenye comfort zone na kuanza kunyosha kidole,nimechukia mno juzi kati ,timu ya Ihefu inayopigana kutoshuka daraja imeanza game na mzawa mmoja tu(goalie),wengine wote sio wazawa ni craze hii!,angalia muziki wetu umekufa kisa BASATA nao wapo politicized, nchi inapoteza vocalists na soloists (hawa ndio key player's)wao wamelala tu, mpaka sasa muziki wetu huwezi kujua ni wa Tanzania au ni wa ghetto ya Harlem
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom