JOTO LA MOTO
JF-Expert Member
- Apr 11, 2018
- 758
- 555
John Lester Nash-1940-2020
Nikiwa bado Bw mdogo nyumbani alifika Baba yangu mdogo mmoja akiwa na kaseti kadhaa alizotoka nazo ng'ambo..miongoni mwa nyimbo zilizonivutia kwenye moja ya kaseti ni ngoma ya "rock me baby"
Sikujali sana ni nani aliyeimba kibao hicho ila baadae nilikuja kujua kimeimbwa na John Nash...nakumbuka siku moja kulikuwa na pati kwa jirani nikawapelekea hiyo kaseti, hii ngoma ilivyoanza tu karibia Watu wote waliokuwa nje wakaingia ndani.
John Nash amefariki jumanne iliyopita, tarehe 6 mwezi huu wa kumi. Pumziko La Amani apate Mwendazake.
Ni miaka 30 iliyopita lakini bado ukisikiliza vocal za hawa 'Waswahili' wenzetu waliozamia huko ughaibuni na ukilinganisha na Wasanii wetu ni kama kuna utofauti mkubwa...sasa huwa najiuliza kama Watu wa jamii hiyo hiyo kwa nini vocal za aina hiyo zisipatikane pia hapa Bongo?.
Huwa nasikiliza Wasanii kama Gregory Abbort, Bill Ocean, Luther Vandros na wengine wengi wenye asili ya Africa na kujaribu kuzitafuta vocal za aina hiyo hapa nyumbani bongo
Hivyo bado huwa najiuliza kama tunao Wasanii wa kaliba hiyo au ni mpaka nao wahamie huko ughaibuni?.