Ngoma za Marekani zilizofanana mashairi na ngoma za Bongo zilizotangulia

Greater thinker

JF-Expert Member
Sep 12, 2011
286
38
Kuna msemo mmoja wa kizungu usemao, Great
minds think alike, ukiwa na maana ya ‘Akili
kubwa hufikiri sawa sawa.’
Hii hutokea mara nyingi sana katika sanaa bila
ya wasanii husika kulitambua hilo. Unaweza
ukakuta wasanii wako sehemu mbili tofauti kwa
nyakati tofauti lakini wakatunga mashairi
yanayofanana bila kuwepo na wizi wowote.
Kwa mara zote ambapo muingiliano wa idea
hutokea na ikiwa tu wameanza wasanii wa nje
ya bchi na kisha msanii wa Tanzania akafuata
huwa anahukumiwa moja kwa moja kuwa ni
mwizi pasipo mashabiki wa Bongofleva kuamini
kuwa kuna muingiliano wa wazo kuu(idea).
Lakini je vipi kwa ishu ambazo wasanii wa
Tanzania wameanza halafu ndio wakafuata
wasanii wa nje? Je nao wamewaiga wasanii wa
bongofleva? Ni kweli hatukatai bado hadi leo hii
wapo wasanii wa bongofleva wanatafsiri mistari
ya wasanii wa nje au kukopi kazi za wasanii wa
nje aidha idea za nyimbo, video au uchezaji.
Lakini hapa chini nakuletea mifano ya kazi za
wasanii wa bongo na zinazofanana kabisa na
kazi za wasanii wa nje lakini wasanii wa
Tanzania ndio walikuwa wa kwanza kutoa kazi
hizo kabla ya wasanii wa nje na ndio
itakayoonesha muingiliano wa idea jinsi ulivyo.
PROFESA JAY (PIGA MAKOFI ) NA BUSTA
RHYMES ( MAKE IT CLAP )
Mwaka 2001 msanii wa Hip hop Tanzania
Profesa Jay aliamua kuwa msanii binafsi baada
ya kukaa kando na kundi lake la ‘Hard Blasters
Crew'(HBC) aliloanza nalo muziki mwaka 1994.
Na mwaka huo huo alitoa album yake ya kwanza
binafsi ‘ MACHOZI JASHO NA DAMU.’
Singo yake ya ‘ Piga Makofi ‘ ilikuwa inapatikana
katika albamu hiyo. Mwaka mmoja
baadaye,October 13, 2002 msanii wa hiphop
kutoka Marekani, Busta Rhymes aliachia wimbo
ulioitwa ‘ Make it Clap ‘ aliomshirikisha msanii
wa dancehall wa Jamaica, Sean Paul ,ukiwa na
maudhui sawa na wimbo wa Professa Jay wa
Piga Makofi.
MWANA FA (UNANIJUA UNANISIKIA?) NA LIL
WAYNE (JOHN)
Rapa wa zamani wa kundi la East Coast Team
(ECT) mara baada ya kumaliza masomo ya
shahada ya uzamili ya fedha aliyokuwa
akisomea katika chuo kikuu cha Coventry nchini
Uingereza, alirudi tena katika ramani ya muziki
wa Bongofleva kwa kuachia ngoma iliyojulikana
kama ‘ UNANIJUA UNANISIKIA ‘ ambayo ilitoka
redioni Feb 23, 2011 na mtandaoni, Feb 25 2011
katika mtandao wa gongamx.com.
Mstari wa tano katika ubeti wa kwanza unasema
‘hela hazilali so ukilala wewe tu.’ Machi 24
mwaka 2011 rapa Lil Wayne aliachia wimbo
uliofahamika kama ‘JOHN ‘ ama wengine
wakiufahamu kama ‘ IF I DIE TODAY ‘
aliomshirikisha Rick Ross. Mstari wa 15 katika
ubeti wa kwanza unasema ‘ The money don’t
sleep so Weezy can’t rest ‘ Ukiwa na maana
karibia sawa na wa Mwana FA.
Laiti kama wimbo wa Lil Wayne ungekuwa wa
kwanza kutoka watu wangedhani kuwa Mwana
FA ameuiga mstari huo.
FID Q (NAMBA 8) NA NICK MINAJ (ALL EYES
ON YOU)
FID Q : ‘ Anahisi asha niona sehemu tatizo
ameshanisahau jina,Unaitwa nani? (FID Q)
Unaishi wapi (Ghetto ) Kazi yako nini? (muziki)
NICK MINAJ: He was like (What’s your name?)
My name Nick (Where you from?) New York in
this chick (Choose and pick).
Rapa Fid Q aliichana hiyo mistari katika wimbo
alioshirikishwa na Msanii Daz Baba ‘Namba
Nane ‘ miaka 10 iliyopita na mistari hiyo ya Nick
Minaj inapatikana katika wimbo wa ‘ All eyes on
you ‘ alioshirikishwa na rapa aliye kwenye
uhusiano naye wa kimapenzi Meek Mill
ulioachiwa June 26 2015.
MWANA FA ( AMEEN ) NA DRAKE ( R.I.C.O )
Juni 7 2012 kupitia kipindi cha XXL, Clouds FM.
Mwana FA aliachia wimbo ‘AMEEN’ akiwa na
Dully Sykes & A.Y ulioandaliwa katika studio ya
4.12, Dully aliyekuwa mtayarishaji wa wimbo
huo.
Katika mstari wa tisa wa ubeti wa pili, kuna
mstari unasema,”kuna viumbe hata huwajui na
bado wana beef na wewe. ” Na huu mstari “How
you hate me when I never met the man’ ni wa
rapa Drake unaopatikana katika wimbo
alioshirikishwa na Meek Mill, ‘R.I.C.O’ uliotoka
June 29, 2015.Nadhani umeshapata picha ya ule
msemo wa ‘Great Minds think alike. ‘
Imeandaliwa na FARAJI FOWZ ZEGGESON
IG: @xfowz
Twitter: @fowzwheezy
Email : xfowz@icloud.com

SOURCE ; www.bongo5.com
 
r city-locked away... inafanana na diamond-utanipendaga, pia na Mike tee(mnyalu)-je utanipenda..
 
21 questions ya 50 cent naona kama Dimond ameikopy na je utanipenda?, Ally kiba na Christian Bella wimbo wa huyu demu naona kama wamekopy kwa R Kelly na Usher Raymond Same girl ni mtazamo tu.
 
Unajua maana ya paragraph! Uandishi wako unachosha. Halafu mstari mmoja kufanana haimaanishi ngoma zimefanana, hawa wa waandishi wa siku hizi vilaaza sana
 
Mzee umetoa boko sana.....umetumia kigezo gani kusema ideas ni sawa? Mbona vitu tofaut kabisa
 
ukumbuke pia...machoz,jasho na damu...ni album ya underground wa USA iliyotoka kabla ile ya geez..iliitwa ..tears,sweat and blood...google it...pia lyrics za fid q...kuna line a memquote nas.."u were a slave to the page of my rymhes book...i made u look"... nyimbo..inaitwa i made u look..google it...
 
21 questions ya 50 cent naona kama Dimond ameikopy na je utanipenda?, Ally kiba na Christian Bella wimbo wa huyu demu naona kama wamekopy kwa R Kelly na Usher Raymond Same girl ni mtazamo tu.
Km ni kukopi nahisi walianzia kukopi kwa mchiz mox na ngwea ngoma inaitwa demu wangu. Kufanana idea si jambo la ajabu.. Idea ni zile zile, labda mtu akopi kuanzia mashair mpaka beat, au melody kama tid na nyota yangu, hapo tunasema kakopi.
 
Umeniudhi ulipo sema nyimbo ya busta imefanana maudhui na nyimbo ya Prof kisa title ya nyimbo hizo. Mchambuzi Uchwara.
Though nakupa high 5 kwa kua creative na umejifikirisha sana... Ila kulishana matango pori sio uungwana dogo. Nice try though.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom