Hatia 4 - Dizasta vina ni best story teller tangu hiphop ya bongo ianze mpaka sasa

Feisal2020

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
772
1,672
Mimi ni muumini wa muziki wa Rap, navutiwa sana na nyimbo za Hip-hop zilizojikita katika masimulizi.

Nimesikiliza story telling rap songs nyingi mno, tangu story 3 ya Jay Moe, Sister sister ya GK, Nikusaidiaje ya Prof. J, Hayakua mapenzi ya 2 Proud mpaka Rafiki ya Sterio,Playboy ya Nikki Mbishi, Enzi za Utoto/Usiku/Sorry za Songa, Mama Pili ya Nash, Nashindwa kuacha pombe ya Mbeya Boy, Kiboss ya Nala Mzalendo na Huna Jipya ya P the Mc..lakini nikiri kuwa sijawahi kubahatika kumsikia msimuliaji hodari kama Dizasta Vina.

Wachanaji wengi huwa wanajitahidi kutoa ngoma zenye stori kali, nawaheshimu kwa hilo.. Lakini kwangu mimi hilo haliwafanyi kuwa wakali kama au zaidi ya Dizasta. Hakuna mchanaji mwenye uwasilishaji mzuri kama jamaa.

Namna Dizasta anavyoweza kuchezea maneno, ku twist plot na ubunifu katika uwasilishaji wake vinamfanya kuwa dunia ya peke yake kabisa! You can kill me bro but nasema kuwa, when it comes to story telling.. Dizasta ni fundi kama mafundi wenzie wakina EMINEM (Yeah I said that) na hapa bongo hana mpinzani. Dizasta anaweza kukuwekea movie ya masaa mawili ndani ya dakika 5 tu tena kwa ufundi wa hali ya juu, umesikia Stan na Kim za Eminem? Yeah nazungumzia vitu kama hivyo.

Dizasta Vina ni mchanaji ambaye huwasilisha nyimbo zake kwa mtindo wa masimulizi ya hadithi, lakini kwa ufundi mkubwa pengine kuliko wasimuliaji wengine wote waliowahi kutokea katika game ya Rap bongo.

Ukitaka kuuona ubora wa Dizasta katika masimulizi chukua muda wako kusikiliza mfululizo wa nyimbo zake Hatia (1-4), Kikaoni, Kanisa na nyinginezo nyingi.

Binafsi nimesikiliza nyimbo karibia zote za Dizasta, na mara kadhaa nilishawishika kuandika kitu kuhusu yeye lakini nikasita. Lakini nisingekua nimemtendea haki kama ningeacha huu wimbo HATIA 4 upite bila kukiri ubora wa jamaa.

HATIA 4, kama jina lake linavyojieleza, ni wimbo wa nne katika mfululizo wa nyimbo zake ‘Hatia’ ulioachiwa juzi tarehe 13 ukiwa sehemu ya album yake inayoitwa The Verteller.

Wimbo huu unaelezea masimulizi juu za vijana wawili, John na Jenny ambao walikuwa katika mahusiano ya upande mmoja ambayo baadae yalikuja kuisha vibaya (tragedy) kwa mmoja kumuua mwenzie.

Hatia 4 umewekwa kwa masimulizi ambayo yanawasilishwa kutumia nafsi ya kwanza (Dizasta kama John) na nafsi ya tatu (msimuliaji, ambaye huyu anatusaidia kuelezea matukio yanayowazunguka John na Jenny).

John alimpenda sana Jenny, licha ya umaskini aliokuwa nao alijitahidi sana kumpa Jenny kila alichokitaka. John alijua kabisa kuwa Jenny hakumpenda, lakini bado alijitahidi kufanya kila alichoweza ila kum impress Jenny. Malengo yake ilikua ni kuja kumpa mwanamke huyo magari na majumba, na badala yake akaishia kumudu kumnunulia chai, chipsi mayai na vocha.

Pamoja na jitihada zake zote, John kila alipomwambia Jenny kuwa anampenda hakuwahi kujibiwa! Jambo hilo lilimuumiza sana John, lakini bado akaendelea kusubiri kwani “atafutae hachoki”.

Pamoja na yote John alijua sababu ya Jenny kutokumpenda sawa na yeye anavyompenda..Jenny alizaliwa kwenye familia maskini sana. Umaskini huo umemuumiza sana na nd'o chanzo cha kifo cha mama yake kufariki kwa kukosa matibabu. Na hii ndo sababu Jenny akaweka nadhiri ya kuwa hatokubali kuishi katika umaskini, na nadhiri hiyo ndiyo chanzo cha mateso ya John.

Jenny aliuchukia umaskini na asingeweza kusubiri hustle za John zilipe. Alimuomba Mungu John ‘aokote' utajiri na alivyoona hilo halikaribii kutokea akaamua kuchukua hamsini zake.

Jenny akapata bwana wa kizungu, bwana ambaye angeweza kumfanya aishi maisha aliyoyataka. Japo jamb hilo lilimuumiza John hadi kufikia hatua akawa ‘mwendawazimu' na kupoteza kabisa muelekeo wa maisha yake lakin hakuona kama ni sahihi kumlazimisha Jenny abaki kwani yeye aliamini kuwa ukilipenda ua sio lazima ulikate,liache likue. Jenny akaenda zake Miami kufuata ndoto zake, kuufuata utajiri aliohusudu.. Na john akabaki na upendo wake.

Kitendo cha Jenny kuondoka kilimuachia John maumivu makali ambayo yalichelewa sana kupona kiasi kwamba akaweka nadhiri kuwa kamwe asingejihusicha tena na mapenzi. Lakini kama tujuavyo, muda ni daktari mzuri zaidi! Baada ya miaka kadhaa kupita John akasahau (au akafikiri amesahau) kuhusu Jenny. Akapata msichana mwingine ambaye japo yeye (John) hakumpenda ila yeye alimpenda na alijitoa sana na hivyo ikambid John ajifunze kumjali.

Mapenzi ya John na huyo mwanamwali yakafikia hatua ambayo wakakubaliana kufunga ndoa. Michango ikaanza na maandalizi yakapamba moto, lakini haikua mpaka pale ambapo John alipopokea ujumbe kutoka kwa Jenny kupitia mtandao wa kijamii. Ujumbe huo ukamkumbusha kuwa sio kweli kuwa amemsahau Jenny kama ambavyo yeye alifikiri:

“Habari naamini u bukheri wa afya

Unaendeleaje maisha na huyo mpenzi wa sasa?

nashukuru nahema, ughaibuni si kwema
Nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa…

Maisha niliyowaza yote ni uongo
Nauzishwa madawa nalazimishwa ngono
Nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani

Roho yangu rehani kiasi sasa naitamani Bongo

Ukubwa umekuja kunisafisha jicho
Ndoto imeisha na taswira imenionyesha sivyo,

Naomba unifate uniondoshe kwenye hiki kifo

Na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo”


Ni kweli kuwa John alimpenda sana Jenny na kamwe hakuwahi kumsahau! Kitu ambacho hakujua ni kuwa Jenny hakumpenda kama yeye alivyompenda. Akaamua kubeba pesa za michango ya harusi ambazo tayari ametolewa kwa ajili ya harusi yake na ‘mwanamwali'. John akaianza safari yake kuelekea ughaibuni kumfuata “njiwa” wake…


NARUDI SOON KUMALIZIA
 
Hii ngoma nimeisikiliza kwa umakini wa kutosha, nimebaini mwandishi bado hajaitendea haki, iko juu kuliko alivyotusimulia. Ukitaka kubaini hilo jipe muda uusikilize wimbo huo uliojaa ujumbe tele na burudani ya kusisimua masikio yako.
 
Mzee nakukubali sana kwenye upande huu Endelea kuwakilisha
Kuna movie ya Kiafrika imefanya vizuri Cannes.Inaitwa "Farewell Amor". Ya Ekwa Msangi.

Nilikuwa naiangalia siku moja kabla Dizasta hajatoa huu wimbo.

Movie ina maudhui yanafanana kidogo na wimbo, ingawa tofauti.

Dizasta akipata team nzuri na budget, script ya kutokana na huu wimbo inaweza kutoa movie nzuri zaidi ya "Farewell Amor".

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom