Ndugu zanguni,
Hasad ni maradhi mabaya sana kwani yanakula mwili na fikra za mtu kama moto unavyoteketeza kuni.

Labda hayo hapo chini yatasaidia:
''Naweza kusema balaa lilianza Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam ule wa zamani.

Ndege inaondoka saa sita usiku kwenda Cairo na hapo nitachukua ndege nyingine hadi London.
Tukatangaziwa tukiwa tushafunga mikanda tayari kuruka kuwa tuchukue mizigo yetu ya mikononi tutoke.

Ndege ilikuwa na hitilafu.
Tukakesha hapo uwanjani hadi mchana siku ya pili ndipo tuliporuka.

Tumefika Cairo ndege ya London inekwisha ondoka.
Tukawekwa Movenpick Hotel, Heliopolis kusubiri ndege ya kutupeleka London siku ya pili mchana.

Sikuwa mgeni wa Cairo nilikuwa nishafika kabla.

Asubuhi nikawapeleka abiria wenzangu vijana wa Kirietria Giza kuona Pyramids na kutoka hapo nikawapitisha Al Azhar, Chuo kikubwa sana cha Kiislam duniani.

Heathrow Airport nimetoa pasi yangu kwa watu wa Immigration.
Siku hizo tunaingia Uingereza bila visa.

Afisa wa Uhamiaji Muhindi mtu mzima.
Akaipekua pasi yangu taratibu ukurasa baada ya ukurasa.

Pasi imeingia Mozambique, Swaziland, Kenya, Sudan, Ethiopia, Egypt na kwengine mara mbili.
Afisa wa Uhamiaji akaniuliza, ‘’Huku kote umekwenda kwa shughuli gani?’’

Nikamfahamisha.
Inaelekea hakuridhika na majibu yangu akapiga simu akaja kijana wa Kiingereza.

Hapa sasa ndipo ilipoanza ‘’drama.’’
Wakanichukua chumba cha pembeni kwa mahojiano zaidi.

Nimebeba ‘’suit carrier,’’ na ndani kuna nguo chache lakini zote ‘’designer.’’
Raha ya ujana.

Wakaniamuru kuvua viatu.
Viatu pia ‘’designer shoes.’’

Wakaniambia kuwa wanataka kuvipitisha viatu kwenye X Ray kuangalia mihadarati.
Mtanzania na Waingereza wanatujua kuwa tulikuwa hoi lakini kijana aliyekuwa mbele yao anavaa nguo ghali.

‘’Umekuja Uingereza kufanya nini?’’
Nikawajibu nimekuja likizo.

Nawajibu bila hofu na wao nahisi wanashangazwa na ule utulivu wangu.
Wanatazamana hawaamini majibu yangu kuwa nimekuja London kutoka Dar es Salaam likizo.

Wanataka kujua nimekuja na fedha kiasi gani.
Nimekwishajua kuwa wananihisi mimi ni muuza unga.

Viatu vimerejeshwa havina unga.
Tumekaa kwenye viti tunaangaliana.

Wakachukua dairy yangu.
Miaka hiyo naweka dairy na naiandika kwa Kiingereza.

Kijana wa Kiingereza akawa anapekua kurasa anasoma.
Akaniluliza, ‘’Unesoma kwa kiwango gani?’’

Nadhani yale aliyosoma mle ndiyo yaliyomfanya aniulize elimu yangu.
Nikamjibu kuwa nina elimu ya Chuo Kikuu.

Tukawa tumemaliza mahojiano yetu na wakanitaka radhi wakaniambia isinipitikie akilini kwangu kuwa wamenifanyia yale kwa ajili ya rangi yangu.

Wakanambia kuwa walikuwa wanafanya ‘’random checking,’’ siku ile na kwa bahati mbaya kura imeniangukia mimi.

Hapa kwenye karatasi ni muda mfupi lakini waliniweka pale wananihoji kwa takriban saa nzima.
Siku nyingine niko Schiphol Airport, Amsterdam nakwenda Marekani.

Nikieleza niliyopitia Ubalozi wa Marekani katika kuomba visa makala itakuwa ndefu sana.
Tumefanyiwa ‘’security check,’’ abiria wote sasa tuko katika mstari tunaingia kwenye ndege.

Akaja ‘’Marine,’’ na nimemtambua kuwa ni askari wa Kimarekani kwa ‘’accent,’’ yake na mkato wa nywele zake.
Ananiita kwa kidole kama mbwa.

Nimemfuata kama mbwa kaona chatu.
Akanipiga maswali ambayo kwa kweli nilishayajibu Dar es Salaam kwenye ‘’Consulate,’’ wakati naomba visa.

Akataka kuona ‘’credentials,’’ zangu.
Akaniruhusu kuingia kwenye ndege.

Entry Point ni Detroit kisha napanda ndege za ndani kukamilisha safari yangu.
Foleni husimami hata dakika mbili ushapita.

Zamu yangu kapekuea pasi yangu.
Wamarekani hawagongi muhuri wana karatasi wanaweka kwenye pasi.

‘’Umekuja Amerika kufata nini?’’
''Kuzungumza chuo kikuu.''

Afisa akaniuliza nina kiasi gani cha fedha.
Akaniambia mbona hizo fedha ndogo.

Nikashangazwa na jibu hilo kwani fedha watu hawatembei nazo mifukoni zinakaa kwenye kadi.
Mastercard yangu ipo kibindoni.

Nikamjibu kuwa nitalipwa fedha na wenyeji wangu.

‘’Kiasi gani?’’
Nikamfahamisha.

‘’Mapesa hayo yote kwa kazi gani?’’
‘’Kwa kuzungumza.’’

Alichukua pasi yangu akafunga ‘’cubicle,’’ yake.
Aliporudi akaniambia, ''Good day Sir.''

Nalala Hilton lakini sikusema kwa kuwa hakuniuliza.

Haya ndiyo maisha yangu na sikuomba iwe hivi ni Allah mwenyewe kwa mapenzi yake ndiye aliyeyaelekeza huko.

Kwangu mimi haya sielezi chembelecho kwa ‘’kujimwambafy.’’
Wala haijanipitikia kuwa ni mambo makubwa sana.

Nina mengi sana mfano wa haya.
Fursa kama hii niliyopata hapa ikitokea tena nitaeleza mengine In Shaa Allah.''

View attachment 1794605
Columbia University, New York

Mzee Mohamed Said mbali ya kuwa comment yako umesukumwa na mwanaJF kutujuza, basi siku nyingine ufungue thread za safari za aina hii tupate kufaidi , maana hapa Jamiiforums mbali na mambo ya historia za ukombozi wa Tanganyika , stori kama hii ya mapito yako sehemu mbalimbali ulimwenguni ni darsa tosha na pia burudani. Shukrani kwa ku-'share' experience yako ya safari lukuki za kuvuka mipaka kimataifa.
 
Bagamoyo,
Nitaweka moja In Shaa Allah nilivyoshindwa kuvuta maji msalani ndani ya treni natoka Glasgow nakwenda Edinburgh.

Nilikuwa sijaona mabomba yanayofunguliwa kwa kivuli.

Mshamba wa Kariakoo.
 
Bagamoyo,
Nitaweka moja In Shaa Allah nilivyoshindwa kuvuta maji msalani ndani ya treni natoka Glasgow nakwenda Edinburgh.

Nilikuwa sijaona mabomba yanayofunguliwa kwa kivuli.

Mshamba wa Kariakoo.

Pole sana,

Kama wewe wa K'koo ulikuwa mshamba vipi sisi wa bara??!!😁
 
Bagamoyo,
Nitaweka moja In Shaa Allah nilivyoshindwa kuvuta maji msalani ndani ya treni natoka Glasgow nakwenda Edinburgh.

Nilikuwa sijaona mabomba yanayofunguliwa kwa kivuli.

Mshamba wa Kariakoo.

Shukrani kwa mchango wako katika kuifanya Jamiiforums kusomwa sana na pia kutuelimisha .
 
Wewe ni mpenda SULUHU kwakuwa huna tabia kama za mnywa POMBE.🤣
Mokaze,
Nimegundua kitu kimoja toka alfajir.

Watu walipokuja kusoma historia ya kweli ya TANU na kutambua ihsani iliyokuwapo baina ya Abdul Sykes na nduguze na Nyerere; na kutambua kuwa kuna mengi muhimu hayajapata kuelezwa baadhi yao walipandwa na hamaki.

Hamaki si kwa kudanganywa bali kwa nini huyu anaandika mambo haya?

Nikaanza kushambuliwa na kupachikwa kila aina ya majina.

Wengine nadhani umeona hapa wananitukana khasa.

Hivyo watu wa aina hii mara moja nakuwa nishawatambua na mimi hujitahidi sana kutuliza ghadhabu zao kwa kusemanao kwa upole.

Jambo lolote ukilitia upole litapendeza.
 
Ila sijui kwanini uhuru Watz lazima uhusishwe na dini utafikiri wazungu au Waarabu walitutawala kwasababu ya dini zetu na sio kwa sababu ya asili yetu ya uafrika hata uwe mkristu vipi mzungu atakuona kinyamkera na hata uwe muislamu vipi Mwarabu atakuona kibwengo tuu
 
Ed...
Historia ya ukombozi wa Tanganyika inaambatana na Uislam kwa kuwa Wazungu waliofika walikuwa Wamishionari na azma yao kuu ilikuwa kueneza Injili katika "dark continent."

Lakini mathalan Krapf alipofika kwa Chief Kimweri Vuga kamkuta anajua kusoma na kuandika yeye na wanae wake wote.

Kimweri akisoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu.

Haya yaliwadhihirishia Wamishionari kuwa ile fikra ya kuwa wanakuja kustaarabisha watu haikuwa sahihi kwani Uislam umewatangulia.

Wamishionari wakafungua njia kwa wakoloni na kwa pamoja wakaanza kuupiga vita Uislam.

Walichofanya Waislam ndiyo haya tunayojadili hapa sasa takriban mwaka wa 10.
 
Pole sana,

Kama wewe wa K'koo ulikuwa mshamba vipi sisi wa bara??!!😁
Mokaze,
Mie wa bara pia.

Sisi asili yetu Shirati kwenye boma la Wajerumani.

Bara yote imeamka siku nyingi sawa na pwani tu.

Dar es Salaam hapa nyumbani kwa bibi mzaa mama bafuni nabeba ndoo na dokidoki.

Nikiienda Tabora kwa babu bafuni bomba la mvua.

Namwaga maji hadi bibi ananiambia nitoke bafuni nishatakata.

Nyumba ina umeme na simu.
Maisha yetu hayajapitana sana.
 
Ed...
Historia ya ukombozi wa Tanganyika inaambatana na Uislam kwa kuwa Wazungu waliofika walikuwa Wamishionari na azma yao kuu ilikuwa kueneza Injili katika "dark continent."

Lakini mathalan Krapf alipofika kwa Chief Kimweri Vuga kamkuta anajua kusoma na kuandika yeye na wanae wake wote.

Kimweri akisoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu.

Haya yaliwadhihirishia Wamishionari kuwa ile fikra ya kuwa wanakuja kustaarabisha watu haikuwa sahihi kwani Uislam umewatangulia.

Wamishionari wakafungua njia kwa wakoloni na kwa pamoja wakaanza kuupiga vita Uislam.

Walichofanya Waislam ndiyo haya tunayojadili hapa sasa takriban mwaka wa 10.
Lakini Waarabu ambao walileta huo Uislamu si ndio walichukua Waafrika utumwani, mimi naona dini zote hizo ni zakitapeli zimekuja vunja ushirikiano wetu.. Leo hii mtu anaona Uislamu ni bora kuliko uafrika hata Ukristo ni bora kuliko Uislamu wakati mtu anapozaliwa anajulikana tuu ni Mwafrika ndio asili yake. So tuache kushupalia sijui ukombozi uliletwa na Waislamu au wakristu. Uhuru ulipatikana baada ya wazee wetu wakiafrika kuchoka unyonyaji wa wakoloni.
 
Inaelekea wewe si mjuzi wa hili somo unalotaka tujadili.

Utumwa ulifanywa na Waarabu, Wazungu na Waafrika.

Soma kwanza historia ya Transatlantic Slave Trade kwa uchache.

Kuhusu historia ya Waislam na uhuru wa Tanganyika hii ni historia ya kipekee kabisa wala haina mfanowe.

Unahitaji kuisoma kwanza ndiyo uweze kujadili na kufananisha.
 
Kuhusu historia ya Waislam na uhuru wa Tanganyika hii ni historia ya kipekee kabisa wala haina mfanowe.

Unahitaji kuisoma kwanza ndiyo uweze kujadili na kufananisha.
Ni muda sasa nimepoteza interest (kuvutiwa) na Makala zako Mzee Said kwani zimeegemea sana upande mmoja haswa wenye maslahi na wewe.

Na lengo lako fiche ni kupotosha umma wa Watanzania kama sio Dunia kwa ujumla...labda kwa kukusudia au lah.

Mpaka wa leo sijaona maelezo yako yanayojitosheleza kudhihirisha kama haswa hawa unaowahusisha walikuwa wanapigania uhuru wa kwao au wa Watanganyika wote?.

Nimewahi kuweka clip humu ya maelezo ya Mzee Waikela akielezea namna Waislam walivyokwenda UNO mara kadhaa wakidai uhuru ambao inavyoonesha hawakuwa wanakidhi vigezo kwani ni kama walikuwa wana agenda binafsi ya kundi kuliko ya wengi (sitaki kutaja agenda ya udini ingawa huenda ndivyo ilivyokuwa)....hukuwahi kukubali au kukanusha maelezo ya Mzee Waikela, na kama anachosema ni urongo basi tuambie wazi kwamba Mzee anasema urongo na tumpuuze....na nitasikitika sana kama unataka tukuamini wewe kuliko yeye aliyekuwa sehemu ya harakati wakati ule.

Hoja ya ukoloni wa Kiingereza kuhujumu Uislamu haina mashiko maana wao Wametawala nchi nyingi zikiwa na dini/imani zao....nyingine zilikuwa na 90% uislamu na wameziacha hivyohivyo, sasa ni nini kilikuwa cha mno kwa Tanganyika?.....hizi ni kati ya hoja zako za kuhisi au kudhani tu unazozihubiri mara kwa mara na kwa nguvu kubwa.

Pia usitake kupotosha kwa kutuaminisha kuwa ni Dar es Salaamu au Uislamu (kama unavyodai) pekee ndio kulikuwa na harakati za uhuru.

Naweka habari fupi kuhusu huku kwetu Upare....nina imani kila mahali kulikuwa na harakati ambazo wala hazikujali yanayoendelea Dar Es Salaam.

Independence movement​

The Pare Union formed in 1946 was one of Tanzania's first ethnic-based nationalist movements to begin activism against the colonial system. Among many grievances, was the exploitation through the production of export crops particularly Sisal and Coffee. Like many other ethnic-based political groups in Tanganyika, The Pare Union then became part of theTanganyika African Association (TAA) which later became the Tanganyika African National Union (TANU) in 1954. This avoided groups like the Pare Union forming into full political parties that were ethnic in orientation.

Harakati za Uhuru
Umoja wa Wapare ulioundwa mnamo 1946 ulikuwa moja wapo ya harakati za kwanza za kitaifa za kikabila kuanza harakati dhidi ya mfumo wa kikoloni. Miongoni mwa malalamiko mengi, ilikuwa unyonyaji kupitia uzalishaji wa mazao ya kuuza nje haswa Mkonge na Kahawa. Kama vikundi vingine vingi vya siasa vilivyokuwa vya kikabila huko Tanganyika, Umoja wa Wapare baadaye ukawa sehemu ya Chama cha Tanganyika African Association (TAA) ambacho baadaye kilikuja kuwa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mnamo 1954. Hii ilizuia vikundi kama Muungano wa Wapare kuunda siasa kamili.

Tofauti na harakati nyingine za mikoani ni kwamba tu Dar Es Salaam ilipata bahati ya kufikiwa na Mwalimu....ambaye alikuta TAA imesinzia, ingawa huwezi kukubaliana na hili lakini hata Mzee Waikela anaelezea namna Mwaimu alivyokuwa anafikia kwenye "Vijiwe" na kuishia kupiga soga tu ndipo akaamua rasmi kuingia mbele na kufufua TAA na kuipa uhai halisi wa chama cha kupigania uhuru.

Ni kupitia vijiwe hivi ndipo Wazee wa Dar waliiona nyota ya Mwalimu na kuamua kuwa wanamuhitaji sana Mtu huyu.

Hivyo ni dhahiri kuwa kabla ya hapo Mikoani kulikuwa na harakati halisi hunda kuliko hata ilivyokuwa hapo Dar na TAA yao na kabla ya Mwalimu.
 
Ni muda sasa nimepoteza interest (kuvutiwa) na Makala zako Mzee Said kwani zimeegemea sana upande mmoja haswa wenye maslahi na wewe.

Na lengo lako fiche ni kupotosha umma wa Watanzania kama sio Dunia kwa ujumla...labda kwa kukusudia au lah.

Mpaka wa leo sijaona maelezo yako yanayojitosheleza kudhihirisha kama haswa hawa unaowahusisha walikuwa wanapigania uhuru wa kwao au wa Watanganyika wote?.

Nimewahi kuweka clip humu ya maelezo ya Mzee Waikela akielezea namna Waislam walivyokwenda UNO mara kadhaa wakidai uhuru ambao inavyoonesha hawakuwa wanakidhi vigezo kwani ni kama walikuwa wana agenda binafsi kuliko ya wengi (sitaki kutaja agenda ya udini ingawa huenda ndivyo ilivyokuwa)....hukuwahi kukubali au kukanusha maelezo ya Mzee Waikela, na kama anachosema ni urongo basi tuambie wazi kwamba Mzee anasema urongo na tumpuuze....na nitasikitika sana kama unataka tukuamini wewe kuliko yeye aliyekuwa sehemu ya Wanaharakati zile.

Hoja ya ukoloni wa Kiingereza kuhujumu Uislamu haina mashiko maana wao Wametawala nchi nyingi zikiwa na dini/imani zao....nyingine zilikuwa na 90% uislamu na wameziacha hivyohivyo, sasa ni nini kilikuwa cha mno kwa Tanganyika?.....hizi ni kati ya hoja zako za kuhisi au kudhani tu unazozihubiri mara kwa mara na kwa nguvu kubwa.

Pia usitake kupotosha kutuaminisha kuwa ni Dar es Salaamu au Uislamu (kama unavyodai) pekee ndio kulikuwa na harakati za uhuru.

Naweka habari fupi kuhusu huku kwetu Upare....nina imani kila mahali kulikuwa na harakati ambazo wala hazikujali yanayoendelea Dar Es Salaam.

Independence movement​

The Pare Union formed in 1946 was one of Tanzania's first ethnic-based nationalist movements to begin activism against the colonial system. Among many grievances, was the exploitation through the production of export crops particularly Sisal and Coffee. Like many other ethnic-based political groups in Tanganyika, The Pare Union then became part of theTanganyika African Association (TAA) which later became the Tanganyika African National Union (TANU) in 1954. This avoided groups like the Pare Union forming into full political parties that were ethnic in orientation.

Harakati za Uhuru
Umoja wa Wapare ulioundwa mnamo 1946 ulikuwa moja wapo ya harakati za kwanza za kitaifa za kikabila kuanza harakati dhidi ya mfumo wa kikoloni. Miongoni mwa malalamiko mengi, ilikuwa unyonyaji kupitia uzalishaji wa mazao ya kuuza nje haswa Mkonge na Kahawa. Kama vikundi vingine vingi vya siasa vilivyokuwa vya kikabila huko Tanganyika, Umoja wa Wapare baadaye ukawa sehemu ya Chama cha Tanganyika African Association (TAA) ambacho baadaye kilikuja kuwa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mnamo 1954. Hii ilizuia vikundi kama Muungano wa Wapare kuunda siasa kamili.

Tofauti na harakati nyingine mikoani ni kwamba tu Dar Es Salaam ilipata bahati ya kufikiwa na Mwalimu....ambaye alikuta TAA imesinzia, ingawa huwezi kukubaliana na hili lakini hata Mzee Waikela anaelezea namna Mwaimu alivyokuwa anafikia kwenye "Vijiwe" na kuishia kupiga soga tu ndipo akaamua rasmi kuingia mbele na kufufua TAA na kuipa uhai halisi wa kupigania uhuru.

Ni kupitia vijiwe hivi ndipo Wazee wa Dar walipoiona nyota ya Mwalimu na kuamua kuwa wanamuhitaji Mtu huyu.

Hivyo ni dhahiri kuwa kabla ya hapo Mikoani kulikuwa na harakati halisi kuliko hata ilivyokuwa Dar na TAA yao na kabla ya Mwalimu.
May Day,
Uamuzi uliochukua wa kupoteza, "interest," kwa kuwa nimeegemea upande mmoja ulikuwa mzuri.

Hata mie hufanya hivyo kama kitu hakinipendezi.

Nini kimekufanya urejee tena kunisoma?

Nimenufaika na historia ya Upare kwani sikuwa naijua.

Kuhusu Mzee Waikela.
Mimi sitosema lolote kuhusu yeye.

Hivi sasa ni mtu mzima sana.

Hiyo picha hapo chini ni Mzee Waikela na mimi.

Mzee Waikela aliwekwa kizuizini na babu yangu Iyui Prison mwaka wa 1964.

20210525_102317.jpg
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom