Bi Zainab, licha ya kukuhangaisha na swaum jana, napenda kutowa shukran zangu za dhati kwa kuwacha shughuli zako zote na kunipeleka kwenye kituo cha tiba. Nimeona bora niingie hapa hapa kutowa shukran zangu.
Ingawa tulichelewa lakini tunashkuru kwa "wasta" wako tukahudumiwa vizuri sana. Ahsante kwa hilo. Na ahsante sana kwa ukarimu wako, Mwenyeezi Mungu akuzidishie ukarimu daima milele, kwetu na kwa wengineo.
Zaidi ya hayo nimependa sana lile sofa la massage na nimependa namna wanavyopima na nimekubali matokeo.
Sema mwambie yule mchina mfupi, aache kukodelea watu kama hana akili vizuri. Lakini mwambie Ahsante sana kwa zawadi ya dawa ya meno na sabuni, kweli nimeitumia dawa ya meno jana usiku na leo, ni super kabisa, sijawahi kutumia dawa so refreshing kama ile. Gozi nalo limeisifu. Na sabuni ni so smooth nimeikubali. Mwambie tukija tena asichoke kutupa hizo offer - kwi kwi kwi teh teh teh. Najuwa ilikuwa ni kwa ajili yako tu ndiyo akatukirim kiasi kile, shukran sana Bi Zainab.
Pia In sha Allah ntakuja kwenye darsa la afya alilosema jana tumechelewa, ntajitahid niwahi Jumamosi ijayo. Anti Mu anakupa salaam na anasema kalipenda lile kochi, hamumuuzii? na kapenda sana ile nini sijuwi ya car massage, kaanza kuiweka kwenye gari jana hiyo hiyo na kufika nyumbani kaitowa kaiweka kwenye kochi, mpaka nnamwambia huo mwili utatepeta, kila saa anakiwasha kimkande, nnakwambia kimekuwa maonesho kila mtu anaoneshwa kinavyofanya kazi, mimi kanikatalia nisikitumie wala nisikiguse, ntakuja kuchukuwa changu. Bahili sana huyu mwanamke.
Zainab thanks again and Ramadhan Kareem.