Bungeni: Watakaowapa mimba wanafunzi miaka 30 Jela

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ukiwemo mswada namba 2 wa 2016, watakaowapa wanafunzi mimba kufungwa miaka 30 jela
 
Kutoa adhabu ni sawa lakini miaka 30 naona kuna tatizo. Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani pamoja na wizara ya sheria na katiba wanatakiwa wapitie upya muda wa vifungo unaotolewa kwa makosa mbalimbali. Miaka 30 maana yake serikali itakuwa na jukumu la kugharimia huyo kwa miaka 30. Huu ni mzigo. Lakini pia kumfunga miaka 30, huyo mtoto anayezaliwa atahudumiwa na nani? Kuna mbinu gani wameweka ili huyo mhusika naye awajibike kumtunza mtoto pindi anapozaliwa?
 
Ndoa zinapigwa vita bila kujua, wanaolengwa ni wanaume kutishiwa uthubutu wao, au ni promo ya ushoga kiaina.

Usinitafsiri kwamba napenda wanafunzi kututikwa mimba, nadhani tunaweza kuchakata tupate njia bora zaidi ya kuifanya jamii imheshimu na kumpenda mtoto wa kike.

Sio kwa staili hii ya kumuogopa ogopa mtoto wa kike hali ya kuwa naye ana mambo mengi anatakiwa kujifunza kutoka kwa jamii.
 
Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ukiwemo mswada namba 2 wa 2016, watakaowapa wanafunzi mimba kufungwa miaka 30 jela

Nakala ya sheria hii ipelekeni mbio HARAKA kwa wabunge WANAUME wa UKAWA walio nje ya bunge TAFADHALI
 
Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ukiwemo mswada namba 2 wa 2016, watakaowapa wanafunzi mimba kufungwa miaka 30 jela
Wajgesema wanaogegeda wanafunzi wafungwe miaka hiyo... haya mambo ya kisubiri matokeo ya kugegeda hayafai
 
akumfunga miaka 30, huyo mtoto anayezaliwa atahudumiwa na nani?
haramu haihalalishi haramu
Dume wa namna hiyo si mtunzaji.Angekuwa mtu wa kujali na kutunza angemtunza huyo aliyemtia mimba amalize masomo yake salama salimini bila mimba.Kama kamtunga mimba mtoto wa shule hata hako katoto alikokazaa kama ka kike aweza pia kuja kukatunga mimba MAANA KAZOEA KUPARAMIA VITOTO HUYO
 
Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ukiwemo mswada namba 2 wa 2016, watakaowapa wanafunzi mimba kufungwa miaka 30 jela
Wanafunzi gani ningependa kufahamu hili. Nini maana ya wanafunzi kisheria ili uchorwe mstari wa vya kuguswa na kutokuguswa. Hata chuo kikuu kina wanafunzi lakini wake za watu, na pia wengine wako under 18.
 
Presha imekupanda tayari.Usijali wa vyuoni ni wanachuo sio wanafunzi.
 
haramu haihalalishi haramu
Dume wa namna hiyo si mtunzaji.Angekuwa mtu wa kujali na kutunza angemtunza huyo aliyemtia mimba amalize masomo yake salama salimini bila mimba.Kama kamtunga mimba mtoto wa shule hata hako katoto alikokazaa kama ka kike aweza pia kuja kukatunga mimba MAANA KAZOEA KUPARAMIA VITOTO HUYO

Yehodaya, siongelei mwanaume, bali mtoto. Au na mtoto kwako ni haramu?

Lakini miaka 30 huoni kama mzigo kwa mlipa kodi?
 
Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ukiwemo mswada namba 2 wa 2016, watakaowapa wanafunzi mimba kufungwa miaka 30 jela
Aise safi kabisa wale Walafi wote hadi kwa watoto wao watakiona cha moto a.k.a Mafataki
 
Hili jambo limepitishwa jana na tayar nadhan kuanza kutumika. Sasa wale WANAUME WAKWARE MASHETANI wanaovizia vitoto vidogo na wengine kuonesha ushetani zaidi wanaoa mjihadhari.

Wanawake wasitumike kma ni chombo cha starehe. Kumekuwa na utamaduni huu mbaya wa kifedhuri wa watu wazima kujihusisha na watoto wadogo kimapenz.nmeshuhudia mambo haya nikiwa nasoma shule moja mkoa wa pwan ambako watoto wadogo walikuwa wanaachishwa shule kidato cha kwanza mpka cha nne ili wkaolewe.
Mambo haya ni ya aibu kumekuwa na matendo ya ajabu mtu kuoa msichana kama mtoto wake na bila aibu kumvulia nguo.
 
Hii sheria si ilishakuwepo? Maana ni kama sielewielewi vile kinchoendelea!!
Au kutakuwa na sheria mbili za miaka tofuati juu ya kosa hili? au inaondoa kile kipengele cha 'mtoto anaweza kuolewa akiwa na miaka 16 au chini ya hapo lakini kwa ridha ya wazazi??
 
Back
Top Bottom