Bungeni: Watakaowapa mimba wanafunzi miaka 30 Jela

Bungeni kuna sheria imepitishwa kuwa kwasasa mtu yeyote atakayempa mwanafunzi mimba, kifungo ni miaka 30.
Je naomba kuuliza ile sheria inayoruhusu kuoa binti mwenye miaka 14 ilishafutwa au ndiko ubabe utatumika pale mnapompeleka mtu mahakamani na sheria kukinzana?
Maana je kutakuwa na maana gani kama sheria ziko mbili zinazokinzana?
Pili kwa maisha ya kitanzania, kweli tutaweza kuendana na hii sheria bila kuboresha sheria nyingine nchini. Maana kwa mfano hawa mabinti tunaokutana nao club za usiku na mara nyingi huwa ni wanafunzi, pale unapokutana naye na kulala naye na baadaye apate mimba katika hiyo process, kosa litakuwa la nani?
Mimi nadhani kabla sheria hazijawekwa kwanza lazima base ya sheria hizo ziwepo, kama ni club basi kuwe na sheria za kutumia ID cards kujua miaka ya watu, maana kuna watu wataangukiwa na hizi nondo (miaka 30), tena wengi tu.
Tatu, kuna mambo yanakujaga automatically tu, mtu anapokuwa na maisha standard, tamaa za kijinga jinga huwa zinapotea. Sasa imagine mwanafunzi wa form one anamajukumu mengine nyumbani kama kuchota maji na kadhalika, na hapo hapo kuna umaskini uliokithiri kwao, hivi unategemea watu wote watakuwa na moyo wa kumsaidia mtu bure.
ifike mahala nchi hii kama tunataka kuweka sheria, basi kuwe na base ya kutosha.
 
Hii inaweza ku-encourage abortion kwa wanafunzi.Pia kama ni sheria ya under 18[Satutory rape] mbona ilikuwepo,sasa Bunge wamerekebisha nini?SOSPA [SEXUAL OFFENCES SPECIAL PROVISION ACT] mbona ina haya mambo,ili bunge limeongeza au kupunguza nini? mi sioni geni lililoogezwa na Bunge labda kama wameongeza kuwa mwanafunzi hata kama ana miaka 20 ukimpa mimba ni kosa,inabidi pia wafafanue definition ya Mwanafunzi -Je ni wa primary?wa Veta?wa Sekondary? wa chuo? chuo gani,open university etc.Siku hizi kuna watoto wanaingia vyuo vikuu wakiwa na chini ya 18,je na hao ukiwabebesha mimba ni kosa?Nadhani wabunge makini wangejadili kwanza haya masuala kabla ya kukimbilia kugonga meza na kupitisha miswada
 
lakini kwa wale ambao dini yao inawaruhusu kuoa binti chini ya miaka 18 itakuwaje?
Dini gani iyo mkuu..? Na he ukiulizwa kifungu gani hicho kinachosema hivyo unaweza kukileta hapa jamvini..? Au ulisikia MTU anasema kuhusu hicho kitu na wewe ukajulia hapo...??
 
Kwani waislamu nao wamepiga kura ya ndiyooooo..? Basi ule msemo wa "tunalazimishwa" na Hajatulia ni wa kweli!!
 
mimi nilimuona mzee mmoja ameozesha mtoto wake mwenye umri wa miaka 14 na alikuwa amefaulu kuingia kidato cha kwanza, na huo mpango ulisukwa kwa ustadi na mwalimu mkuu wa shule ya msingi, mzazi watoto anaeolewa pamoja na mtendaji wa kijiji kile..... iliniuma sana kwa kuwa napenda watoto wa kike nao wapate elimu.
 
Sheria inasema utatiwa hatiani kwa kujamiiana tu, wala si lazima mimba itokee. Someni kwa umakini sana hiyo, tena imesema bila kujali kama mmekubaliana au la!
 
Kama wanaume wangekuwa wanashika mimba na kujifungua, ninaamini kuna mijanaume ingekua inajifungulia mafichoni halafu inapomaliza tu kujifungua hapohapo inakabaka katoto. Ukiona mtu anabaka hadi sabuni, au kiganja cha mkono wake mwenyewe jua huyo mtu ni hatari kuliko kitu chochote hapa duniani.
Kuna mwanamke mmoja nilisha mfuma ana baka dildo nilishangaa sana!!
 
wangetunga sheria kali kwa wanaofanya mapenzi na wanafunzi kutoa adhabu hiyo wala haiwezi kusaidia kwani mtoto atakayezaliwa nani atamtunza ila wakiweka sheria kali kwa watu wanaofanya mapenzi na wanafunzi itasaidia kupunguza mimba za wanafunzi tusishangae baadae wakaleta sheria ya kutoa mimba kwa wanafunzi kwani mzigo wa kuwatunza hao watotot utakuwa mkubwa
 
Hii sheria ya ajabu na kama kawaida tumekurupuka. Tumeangalia upande moja tu wa sarafu ili kuiwezesha serikali kukwepa jukumu la kuifanya elimu itoe motisha kwa wazazi, wanafunzi na jamii.

Ni wazi elimu yetu imeshindwa kumfanya mzazi apande mtoto wake kusoma na mtoto mwenyewe aone elimu ndio kila kitu. Kifupi tunapokuwa na wasomi lukuki mitaani wasio na kazi, tunapokuwa na wanachuo wadada wanaojiuza ili kuendesha maisha yao, tunapokuwa na wazazi wenye maisha magumu sawa na watoto wao waliovyuoni, tunapokuwa na mfumo wa elimu ulio ghali mno kwa watu masikini, Ni dhahiri wanafunzi na wazazi wataona vyema kuolewa kuliko kuendelea shule.

Uwingi wa mimba shuleni sio kielekezo muhimu cha uwapo wa wahalifu bali ni kielelezo tosha kwamba umuhimu wa elimu kwa wazazi na wanafunzi umepungua. Jukumu la serikali kuhakikisha elimu inaleta umuhimu stahiki kwa wazazi na wanafunzi. Ebu angalia, kwanini mimba nyingi ni miongoni mwa wanafunzi wa familia masikini? Hili kwanini halikuwa mjadala bungeni?

Pale serikali inapojigombeza yenyewe na kujiwekea adhabu kwa jambo linalolisababisha panastahili kibwagizo cha kicheko cha huruma kwa serikali na nchi hiyo. Tusipotafuta mzizi wa tatizo na kuukata tutatumia ela nyingi katika ujenzi wa magereza.
 
Naomba mnifahamishe mlioipitia hiyo sheria.
Sheria inasemaje ikiwa hiyo mimba kapewa na mwanafunzi mwenzake?
Yaani wote wapo under 18
 
Wajgesema wanaogegeda wanafunzi wafungwe miaka hiyo... haya mambo ya kisubiri matokeo ya kugegeda hayafai
Je mtoto atakaezaliwa atalelewa na nani na wakati aliebebeshwa ujauzito ni mwanafunz, hvo bado n mdogo kiumr kuweza kumhudumia mtoto.
 
Sheria zingine zinatia hasira na kuleta maswali kwa Waletaji na Wapitishaji wa sheria,inaingia akilini kwa Ulimwengu wa sasa au kizazi cha sasa jambo hili(suala la mimba) kurekebishika?,sidhani,kama siyo njia ya kutaka kupeana kifungo cha miaka 30 kwa chuki na mipango ya muda mrefu kwa wahusika,pil suala la mimba linakuja baada ya makubaliano ya hiari baina ya watu wawili,inakuwaje? mmoja tu ndiyo aonwe kama mkosaji.Na kuhusu vifungo vya Majangili,Wahujumu uchumi,mafisadi na Wala Rushwa vinasemaje?,au sababu hawa ni watu wazito ndiyo wanaambulia miaka 1/2/3 mpaka 5,ukifanya utafiti utagundua kuna vifungo vinavyomlenga Mtu wa hali ya chini tena zaidi Vijana,kifungo chake ni kikali kuliko hata aliyeibia Serikali mabilioni ya Fedha,kwa mfano Sheria ya makosa ya Kimtandao nayo inamgusa sana Kijana.Simaanishi natetea maovu Bali nazungumzia adhabu na kosa lenyewe na Walengwaji wakubwa ni Vijana
 
Kumpiga mtu miaka 30 ni kuoadhibu serikali kwa kuwa Mtoto atakaezaliwa atajenga chuki na serikali kwa kosa la kumfunga babake
Idadi ya machokoraa na watoto wanaolelewa na single parents itaongezeka.
Serikal itabeba zigo la kulisha watia mimba wanafunzi kwa kutumia kodi zetu sie tusiotia mimba wanafunzi
 
Back
Top Bottom