Bungeni: Mjadala wa Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 uliosomwa kwa mara ya pili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,981
Leo 01/11/20220 muswada wa sheria ya ulinzi wa Taarifa binafsi wa mwaka 2022 ulisomwa Bungezi na Waziri Habari mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye.

Mswada huo unajadiliwa wakati huu bungeni fuatana nami kufatilia mjadala huu.

=====

Zahoro Muhamadi Haji: Malengo ya kudhibiti, yapo malengo 5 maana yake hapa duniani aidha tunapenda au hatupendi lakini lazima tulinde faragha za watu, dunia sasa ina mitadao na taarifa tunatafuta kupitia mitandao hivyo lazima tulinde taarifa za watu, na tunazilinda vipi, tunalinda kwa sheria ndio maana wenzetu wameleta mswada wa kulinda taarifa.

Amesema ni vizuri tuwe na sheria ili mwananchi yoyote ambaye taarifa zake zitatumika kinyume na takwa lake ili aweze kwenda mahakani maana kutakuwa na sheria ya kuzilinda na hii itasaidia kufanya taarifa zetu hazichezewi maana sasa ni ulimwengu wa kubadilishana taarifa, taarifa lazima ziwe na za kweli na ziwe fasaha.

Miraji Jumanne Mtaturu: Niipongeze serikali kwa kuja na sheria hii kwani watanzania walihitaji muda mrefu sheria hii kwa ajili ya kulijda taarifa zao.

Leo hii tunafanya mambo mengi kwa kutumia TEHEMA hivyo kuwa na sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi kutawaweza watu kuwa na ujasiri wa kuwekeza zaidi kwenye TEHAMA kwa kuwa taarifa zao ziko salama na wawekezaji wengi walikuwa wanasita kuwekeza kwenye TEHAMA ila kuja kwa sheria hii kutawafanya wawekezaji wengi kuwekeza kwani uchumi mkubwa sasa uko kwenye teknolojia, hivyo nawaomba wabunge tuipishe.

Pia naomba sheria ikitungwa nzuri iende hivyo hivyo na kanuni ziwe nzuri sio tunatunga sheria ila mnaweka kanuni mbaya hadi tunaulizwa mliwezaje kutunga sheria hii? Naomba hata Spika zikitungwa kanuni ujiridhishe na hizo kanuni ili ujue kuwa ni nzuri kabla ya kupitishwa. Hii sheria ni nzuri na inabidi iwe na kanuni nzuri ili iwe na kama ilivyokusudiwa.

Stella Fiyao: Naamini muswada huu utaenda kuwa mwarobaini wa tatizo la watu kuigiliwa taarifa zao, sisi wote ni mashahidi miaka 2 au 3 watu waliingiliwa kwenye akaunti zao na kujulikana na hela na hela zao kufilisiwa.

Muswada huu unakwenda kuongeza wawekezaji wa ndani na nje kwa wengi walishindwa kuwekeza kwa kuwa hatukuwa na sheria hii.

Nashauri kwenye sheria hii liongwe neno FARAGHA, neno faragha limebeba maana nzito, Fine za kiutawala, sheria imesema fine ya mwisho itakuwa ni sh milioni 100 lakini haijasema hiyo mioni 100 ni kwa makosa yapi? naona hii itakuwa mwanaya wa wananchi kuonewa, wanaweza wakasema itasema kanuni lakini kanuni zinaweza zisiwe sawa hivyo iseme ni kwa makosa yapi.

Mwananisha Ulenge Mbunge wa viti maalumu wa CCM: Mwanaisha Ulenge akichangia hoja yake katika mjadala wa Muswada wa ulinzi wa taarifa binafsi ameweka bayana kuwa sheria hii imekuja kwa wakati sahihi na inakidhi maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sasa na wakati ujao.

Aidha, akifafanua zaidi, Mwanaisha Ulenge ameeleza kuwa ukiangalia vizuri vipengele vilivyopo katika muswaada wa ulinzi wa data binafsi utabaini kuwa umelenga kuleta maadili katika matumizi ya teknolojia ya habari.

Mwananisha Ulenge anasema katika ibara ya tano ya muswada huu imezungumzia kuhusu usafirishaji wa taarifa binafsi. Suala la usafirishaji wa taarifa binafsi linaweza kufanywa na mtu mwenyewe katika mitandao ya kijamii wanapoingiza taarifa kwenye akaunti zao. Hauna uhakika kwamba taarifa hizo unazoziingiza makampuni husika yatazitumiaje.

Makampuni mengi nchini kwetu yana saver ambazo zimehifadhiwa katika mataifa yaliyoendela hivyo hata taarifa za watu zinazochukuliwa zinahifadhiwa katika saver hizo.

Sheria hii imembana mkusanyaji taarifa kuhakikisha kwamba anatengeneza sera kamilifu zitakazolinda usalama wa taarifa binafsi. Akienda kununua saver popote anaponunua taifa hili lituhakikishie kwamba data hizo zotakazohifadhiwa ndani au nje zitaendelea kulinda usalama wa taifa letu.

Anaongeza kuwa, katika Muswada huu kuna haki ya kusahaulika kwa maana ya kwamba data zangu zilizokuwa zinatumika kwenye kampuni fulani ikitokea nimefariki natakiwa nipate haki ya kusahaulika baada ya muda fulani. Ukiangalia sheria ya uhujumu uchumiinazungumza kwamba mtu anasahaulika baada ya miaka 10, Sheria ya kodi miaka 7, TCRA miaka 5 lakini nisipotumia laini yangu kwa miezi mitatu unasahaulika.

Mwanaisha anashauri kuwa sheria hii iweke usawa kila mahali ili kuwe kuwa muda sawa wa mtu fulani kusahaulika.

Ally Mlagila Jumbe: Kwenye jina la taarifa hii kuna kitu kinapungua, tunaposema tu ulinzi wa taarifa haitoshi, inabidi iwe ulinzi wa taarifa na faragha, nchi nyingine wameshafanya hivyo sisi tunasita nini? Kwa kuwa mtu anaweza simama tu hadharani akakuuliza jina, unaishi wapi badala ya kukuuliza kwa faragha, inabidi tunapotoa taarifa kuwe faragha na kama neno hili kwa kiswahili ni zito basi tutafute neno lingine lenye maana hii.

Lakini pia mtu akifariki inabidi taarifa zilindwe sio kubaki zikizagaa inabidi tuone jinsi ya kulinda taarifa za marehemu.

Mbunge Abdulwakil: Mbunge Ahmed Abdulwakil amesema kuwa Sheria hiyo ni muhimu na endapo itapitishwa na Bunge italinda utu, heshima na faragha ya wananchi.

Kutokana na Tanzania kutokuwa na sheria hii watu wengi wamekuwa wahanga wa taarifa zao binafsi kutumiwa kiholela, mfano kwa baadhi ya Wabunge ambao taarifa za mazungumzo yao binafsi zilitolewa hadharani bila ridhaa yao.

Muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utakomesha matumizi mabaya ya taarifa binfasi na watu watakuwa na amani linapokuja swala la taarifa zao na faragha zao kuwa salama

Nape Nnauye: Majumuisho ya hoja, Natambua zipo hoja nyizi za ushauri nami niwatoe hofu wajumbe kuwa tutazizingatia kwenye utengenezaji wa kanuni.

Hoja1. Haki ya marehemu nataka niwathibitishie kuwa sheria imezingatia haki ya mtoto, marehemu, au asiye na uwezo wa kutoa ridhaa sheria imesema mzazi, mrithi au wakili aweze kusimama kwa niaba yake.

Kanuni zitakazotungwa zitazingatia sheria iliyotungwa na pia tutawahisisha wadau ili kuzingatia matakwa yaliyokusiwa na ikiwezekana kanuni hizo kupitiwa tena ili ziwe nzuri na analihakikishia bunge kuwa kanuni zitakuwa nzuri.

Muswada wa ulinzi wa taarifa binafsi utavutia wawekezaji wengi kwani ni takwa la kimataifa na wawekezaji wa TEHEMA wanahitaji sheria hii ili kuweza kuja kuwekeza nchini kwetu. Hivyo sheria hii ni muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wa nzhi yetu.

Pia soma:
 
Back
Top Bottom