Hiyo hoja ya posho imewakamata pabaya CDM. Wameonyesha unafiki wa kutupwa. Kwenye posho wameishia maneno tu na Zitto kuwa shujaa wao na kwa hilo CDM hawampendi kweli Zitto. Mkuu kwa taarifa yako Mbowe ameishaichikua V8 ya serikali. Tuache unafiki na uzandiki yanapokuja masiala ya ukweli. Mbowe kama kiongozi wa kambi ya upinzani ameshindwa kuonyesha uongozi kwa mfano, kama kiongozi alitakiwa yeye ndiye azikatae posho kwa vitendo kama Zitto. Alipoona Zitto kazikataa kwa vitendo kutekeleza sera ya CDM, Mbowe akakurupuka na kurudisha gari ya KUB, lakini sasa ameichukua tena.
Katika posho CDM wamekuwa wanafiki kuliko mashujaa kama wanavyotaka watu wawajue.