Mh.Mkasomali na Myika wameomba mwongozokuhusu sakata la madaktari, kwamba imefika wakati sasa liruhusiwe kujadiliwabungeni kwani serikali mado inafanya maamuzi kibabe wakati swala lipo mahakamanina Madaktari wanaendelea kigoma huku wananchi wakizidi kuathirika.
PiaMh.Mnyika amelalamila kuwa jana Mwenyekiti aliwatolea kauli mbaya kwa Mbunge Mkasomali na yeye yaliyokiukaa kukiuka kanuni mbalimbali kwa kuwaambia kauli zamatusi, maudhi na kashifa kufuatia kumwambia Mkasomali kwamba aache kimbelembele,anadandia hoja na anajitafutia umaarufu. Na kwa mnyika kuwa ameshindwa kujibu taarifa (kufatia hoja za Mwigulu ambazo sikubahatika kuzisikia) ambapo hajapewanafasi ya kujibu na kuwa eti Mnyika nawashwa (kauli amabyo aliitafasiri kama nitusi). Majibu ya Mwenyekiti: Kuhusu sakata la madaktari hakutolea jibu lolote,bali Mwenyekitu amemgeuzia kibao Mkasomali na kusema yeye ndiye alivunja kanuni kwanza (hakutaja zipi), ila kuhusu Mnyika amesema atalijibu baadaye ama siku atakayoona inafaa.
Kama na muhilili huu utabaki kimya kwenye huu mgogoro wa madaktari na serikali, basi itabidi wananchi tutumie nguvu ya UMMA.