Bungeni Live: June 19, 2012

Bungeni Live: June 19, 2012

hawa wabunge wa ccm wengi wao hawajui wasemalo. Wanawakashifu wapinzani kwa kukosoa serikali ya ccm kisha na wao wanarudi kukosoa mapungufu yaliyopo kwenye bajeti ya serikali ya ccm. Hawa nawafananisha na nyoka anayemeza mkia wake mwenyewe!
 
Naibu spika: Anamtoa mnyika nje ya bunge , kwa utovu wa nidhamu. na anaamuru mnyika atoke nje ya bunge.

Wana ubungo, mmechagua BOMU. AIBU SANA

CCM wanajikaanga kwa mafuta yao. Jazba za Ndugai ndiyo furaha na neema ya CDM. Hakuna jipya aliloongea Mnyika ambalo mwana-CCM hajawahi kuongea, hili ni bunge la double standard. Wananchi wanajua na hukumu wanaitoa kwa kuongeza chuki dhidi ya CCM na wabunge wake.

Jana Komba kaita watu machizi kwa na kuwataka waanzie Mirembe kabla ya kwenda Bungeni wakamshangilia, Lowassa aliwahi kuiita serikali inashindwa kufanya maamuzi magumu bungeni-> dhaifu wakamshangilia. Kwenye hili la kumtoa nje Mnyika Ndugai atajutia uamuzi wake kwani unaipaisha CDM zaidi.
 
Mrema: Anagusia, ahadi ya barabara, hospitali, maji safi katika jimbo lake la vunjo, miradi inasuasua.
 
By the way who's President? lazima ifike mahala tusimtukuze mtu bila kufikiria mnyika katolewa out kwa kumwita mdhaifu kwani si mdhaifu
 
Mrema anatoa point, kwa nini fedha wanazoidhinisha haziendi huko kwenye halmashauri za wilaya?
 
Nitaunga mkono hoja kama fedha zinazoidhinishwa zitafika kwenye halmashauri, Nitaunga mkono hoja mafisadi hawatakula pesa zinazoidhinishwa.
 
Je serikali ina mkakati gani wa kufidia pesa zilizopelekwa kweye halmashauri na kuibiwa? mbona hawa watu walioiba pesa kwenye halmashauri hawastakiwi?
 
Nadhani baadhi ya wabunge huwa wanaongea kama vile wamekurupushwa na hawakujua kuwa wako kwenye orodha ya kuchangia. Mtu anaongea mtiririko huuoni. Mara vijembe mara kejeli. Tarime Kazi mnayo 2015.
 
Kwani kuna tofauti yoyote ya alichoongea Lusinde na Nchemba?? Wapinzani wanaonewa bwana....
 
Mrema kajitahidi sana, na atleast ameongelea kuhusu bajeti. hajatoka nje ya mada.
 
Yaani leo kazi ipp ndani umo eti atplewe hadi nje ya geti!

kikao hiki tutarajie meeeng,,,,kila mtu atatengeneza habar humo ndani,some tym hao polisi huwa hawana kazi,,,,bora nao kesho waonekane kwenye MEDIA
 
  • :flame::flame::flame::flame: , kuna mbunge wa ccm anatoa point sana. wabunge hawajasoma vyema bajeti, wanachangia tu. Anawaomba wabunge wasome vyema.
 
Back
Top Bottom