Bungeni Live: June 19, 2012

Mbunge wa CCM mkoa wa Mtwara jimbo la masasi,Mh.Mariam Reuben Kasembe ameikebehi CDM kwa kudai kuwa Rais anaweza kutoka chama chochote lakini Rais bora atatoka CCM.Maneno haya ameyanukuu kutoka kwa hayati Mwl.Jk Nyerere katika hotuba yake ya mwaka 1995.Mh.Mariam amedai CDM watafute chama kingine kama wanataka kuwa marais hapo baadae!Kwa hali ilivyo CCM wanakwepa hoja za ukweli pale bungeni na badala yake wanatumia muda wa kuzungumzia mambo ya maana vibaya kwa kurusha maneno ya ukakasi kwa CDM.Hivi CCM inatarajia kuendelea kutawala milele?
 
Rais bora atatoka ccm,kwasababu mikoa ya Lindi, na Mtwara ,hakuna maji hakuna barabara,shule vituo vya afya,sipajui maeneo yote ila nilikopita na nilivyoona kupitia itv chadema walivyopita huko,ni dhairi kuwa wabunge wa ccm na serekali yao ni dhaifu mno!
 
Mh Lusinde aichana chadema aitetea bajeti ya serikali na kusemma sasa inatakiwa kuelekezwa katika mikoa mingine na kuacha mikoa ambayo ilinufauka enzi za ukoloni.

Mbowe atakiwa kujiuzulu baada ya kuudanganya umma kuwa hatatembelea gari VX V8 La serikali lakini amechukua gari hilo na kutembelea kinyemela pia alisema hatapokea posho za vikao ilihali posho hizo anakula kinyemala mbowe; mh lusinde amesema kabla mboye hajataka mawaziri wajiuzulu anatakiwa kujiuzulu yeye kwanza.Aidha Mbowe afananishwa na Mwisamu asiye safi anayekula Nguruwe

NB

Mh Lusinde kachangia kwa kusema anaunga mkono hoja ya serikali kuendelea kutegemea pombe na sigara katika pato la nchi lakini kama wananchi wataokoka itakuwa vizuri pia kwani watatumia muda wao mwingi katika kuliombea Taifa lipate maendeleo makumbwa


!? Hivi mwenye matatizo ni yule aliyempa gari au anayetumia !?, hivi yule anayetafuta pesa za kulipa posho kisha akalipa, mpokeaji anakasoro gani !?"
 
Sijaona spika katika Bunge letu mwenye hekima na busara wa maamuzi ya usawa kama Sitta.

Bunge ni la changamoto na vijana waliosoma na wanajua nn wananchi wanataka.

Bunge la ubabe kitukana watukanwe wapinzani na mipasho lakini ikigeukia kwa serikali ni kosa kubwa.

Wananchi tumeona naomba tuamue 2015
Sitta namkubali kwa 100%, majungu na uzandiki ndo umetuleta hadi hapa tulipo.
Mzee yule alikuwa anasimamia ukweli bila ya kujali itikadi/ ushabiki wa upande wowote ule. ukweli wake na kusimamia haki ndo kilikuwa kitanzi chake. lakini mungu mkubwa, Makamba mropokaji alipigwa zengwe na kufanywa msukule wa muda, na kutamka wazi kuwa tunataka spika mwenye ufa na wala si mwenye muhogo kwa kipindi hiki.
Matokeo yake, Makamba hayupo ktk ramani, mzee wetu Sitta amewekwa ktk kilengeo, atapotezwa (kisiasa) mida si kitambo sana.
Sitta nakubali confi zake sana. pamoja na kunyamazishwa na wizara nyeti, bado anaichana Sisiem kwa kwenda mbele. Huu ndo uzalendo!
 
Kwa kweli Mh. Spika (Bi Kiroboto) ni hovyo kabisa, ila mtu mswafi ni Mh, SITTA pekee na wamemtoa USpika kwakua amekata kulinda Ufisadi yao na maslai yao Bungeni ndio maana, lakini wengine ni chachandu tuu ambae imechacha na avai kula.
 
​Katika mchango wake katika bajeti ya Serikali, Mhe Mbatia amegusia suala moja ambalo kwakweli lina utata sana.
Taasisi ya Aghakan nchini ina mkataba na serikali wa kutolipa kodi zote (zero tax) nchini kwa sababu kwamba wanatoa huduma za elimu na afya kwa watanzania masikini kwa ghafama nafuu

Lakini cha ajabu ni kwamba hospitali na shule za aghakhan ni most expensive kuliko shule na hospitali nyinginezo. Je kuna maaana gani watu hawa kuendelea kupewa exemption. Naambiwa hata toilet paper inayonunuliwa na aghakhan hailipiwi kodi...achilia mbali magarim vifaaa n.k

Tena wanachofanya, wanawatoza watanzania waswahili na makampuni ya nchini very high premium pale hospitali alafu wana wa subsidize wahindi wa jumuiya ya ISMAILIA ndio wanatibiwa bure pale. Kufanya operation ya appendix pale ni shilingi milioni 2, wakati same operation Tumaini Hospitali ni shilingi 400,000 na St Benard hospital ni shilingi 600,000.

Iweje Agakhan wasilipe kodi ihali Hindumandal ambayo nayo ni ya kidini wanalipa kodi?. Tunaambiwa Regency Hospital ni moja ya walipakodi wakubwa katika TRA kanda ya Ilala.....wanalipa kodi karibia shilingi bilioni 2 kwa mwaka.....sasa aghakhan ambayo ni ghali kuliko regency na ina operations maradufu ya regency si ilipe kodi tu. hii ndio mianya ya upotevu wa fedha za serikali...

Hongera Mhe Mbatia kwa kuliongelea suala hili bungeni
sasa hii wazee wa vurugu wala hawatakomenti chochote
 
Wabunge wa CCM wote ni vilaza sana na sijui hawajui kwanini wapo bungeni? Badala ya kuwatetea wananchi wao wanakitetea chama. Je Tutafika?
 
Back
Top Bottom