Bungeni Live: June 19, 2012

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Tuhuma ya mkuu wa wilaya kuhongwa gari yaibukia bungeni.

Mh Meshak Opulukwa atakiwa kupeleka vielelezo kwa spika ili ishu ishughulikiwe rasmi.
 
Mkuu yupi wa Wilaya alihongwa?
Alihongwa na nani?
Ni wapi?
Ni lini?
Nia ilikuwa nini?
 
Angalau Mh. Meshaki Opulukwa ameanza kuunguruma. Amesumbuka sana na kesi ya uchaguzi huko Meatu, sasa baada ya kushinda kesi anaonekana. Inawezekana hizi kesi za uchaguzi zinamikakati ya kupunguza nguvu ya Upinzani Bungeni.
 
Kombo!
  • Naitazama matatizo ya bajeti hii katika mafungu matatu. serikali bunge na mahakama. na hii bajeti haiko hivyo
  • hii bajeti wanachambua wachumi si halali.
  • sisi tunaokaa mijini ndo tunauwezo wakuona haki kuwa nchi hii inatimiza haki hiyo. mihimili hii haina msingi.
  • sisi kama bunge tunaosimamia mhimili huu,
  • Judiciary haipewi haki ya kujiongoza, inaingiliwa. bajeti imepangwa, tunajadili sisi wabunge.
  • Mheshimiwa waziri haoni kuwa mishahara ya wabunge wa A/mashariki ipo sawa sawa na wabunge wa tanzania?
  • TRA inakusanya mapato kwenye bandari ya zanzibar. lakini hakuna hata mpango wa kuipromote ile bandari, kazi yao kukusanya mapato tu.
  • watalii wote wanaokuja zanzibar, wanalipa kodi kwenye ubalozi wa tanzania,
  • zanzibar wanafaidika na uwanja wa ndege peke yake!
 
​Katika mchango wake katika bajeti ya Serikali, Mhe Mbatia amegusia suala moja ambalo kwakweli lina utata sana.
Taasisi ya Aghakan nchini ina mkataba na serikali wa kutolipa kodi zote (zero tax) nchini kwa sababu kwamba wanatoa huduma za elimu na afya kwa watanzania masikini kwa ghafama nafuu

Lakini cha ajabu ni kwamba hospitali na shule za aghakhan ni most expensive kuliko shule na hospitali nyinginezo. Je kuna maaana gani watu hawa kuendelea kupewa exemption. Naambiwa hata toilet paper inayonunuliwa na aghakhan hailipiwi kodi...achilia mbali magarim vifaaa n.k

Tena wanachofanya, wanawatoza watanzania waswahili na makampuni ya nchini very high premium pale hospitali alafu wana wa subsidize wahindi wa jumuiya ya ISMAILIA ndio wanatibiwa bure pale. Kufanya operation ya appendix pale ni shilingi milioni 2, wakati same operation Tumaini Hospitali ni shilingi 400,000 na St Benard hospital ni shilingi 600,000.

Iweje Agakhan wasilipe kodi ihali Hindumandal ambayo nayo ni ya kidini wanalipa kodi?. Tunaambiwa Regency Hospital ni moja ya walipakodi wakubwa katika TRA kanda ya Ilala.....wanalipa kodi karibia shilingi bilioni 2 kwa mwaka.....sasa aghakhan ambayo ni ghali kuliko regency na ina operations maradufu ya regency si ilipe kodi tu. hii ndio mianya ya upotevu wa fedha za serikali...

Hongera Mhe Mbatia kwa kuliongelea suala hili bungeni
 
huyu habib kombo mbona hajui hata kutumia tafsida ktk maelezo yake.
Anasema maneno makali sana mfano.
Mimba badala ya ujauzito.
Kuzaa badala ya kujifungu.
Wamama wanatiwa mimba.??
 
Murtaza Mangungu:
  • Mkoa wa lindi umepangiwa 14bil, tunafanana na mkoa wa rukwa, na katavi ambayo ina wilaya mbili tu.
  • Wassira alisema mkoa unaoongoza na mtawanyiko mkubwa wa watu ni mkoa wa lindi.
  • Huu mfumo wa bajeti una matatizo
  • Siku zote tunalalamika tujengewe barabara, ili mazao ya wakulima yafike kwenye soko
  • dhana ya kilimo kwanza rais alilianza kwa nia njema, lakini sasa inaonekana ni kilio kwanza
  • kwani nmb au mabenki yetu wasipewe uwezo wa kuwakopesha wakulima .......... mawasiliano yame distort
 
naona wazee wanaserebuka ..mh. Mbatia kanifurahisha sana. anachangia mada kisomi..safi sana Mbatia
 
Back
Top Bottom