Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Kuna mwenye link ama ya Radio au TV kuweza ku access Bunge online ? Msaada tafadhali
 
Wana JF wengine tuko mbali na kwa kuwa hapa ni hazina ya GT tafadhali naomba msaada wa Link ya ama TV ama Radio yenye access na Bunge Live .Ili name niweze kufuatilia tokea huku mbali .
 
Hivi kumbe kuna BUNGE linaendelea au it is just a mere joking?
 
Wabunge wamezomea maana wamechoka na tabia ya Serikali kutaka kupelekewa majina ilhali Mkuu wa Nchi alisema anayo,kwanini wasianze na hayo?

Simple, LUKUVI akachukue majina kwa KIKWETE na siyo ayatake kwa wabunge.
 
Serikali ya ccm ni mzigo,kikwete alisema anayo orodha kwa nini Lukuvi asiende kuyachukua au wanataka wachakachue majina ya vigogo? Jk ni janga
 
Wana JF, Tanzania bila maombi haiwezekani. Viongozi wetu wanahitaji kuombewa ili wasimame kwenye zamu zao maana kama wanahusishwa na issue hizi maana wenyewe wanahutaji kupona kwanza. Kila mtu anajua jambo unaloshiriki si lazima awe na biashara hiyo but even kupokea pesa zake ni umeshiriki na CCM tunajua inaendeshwa na wafanya biashara tena wakubwa na wadogo. Kama unajua kuomba its your time kumwomba Mungu kwa Imani yako aingilie kati tupate viongozi wenye Integrity ambao wanaweza kusimama bila shinikizo lolote. Tunajua ukila cha mtu unakuwa Mtumwa kwake. Au kama unashiriki uovu huwezi kukemea uovu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lukuvi anajaribu kuteka hoja ya wanaotaka kuanoika drug dealers kwa faida ya ma-tycoon. Hivi bado serikali inadhani watanzania ni wajinga kiasi cha kuwapiga change la macho hata kwenye mambo ambayo kimsingi yanaiumiza jamii. Yapasa tugeuze kibao kama ile wale watafiti wa Marekani walioamua kila mwanasiasa anae pinga vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa kimbunga kinapotokea kitabatizwa jina la mwanasiasa anaethibitika kuwa ni kikwazo kwa kampeni hizo.
 
nilishawahi kumsikia kiongozi mmoja akisema MAFISADI wakishitakiwa nchi itayumba so na hawa jamaa wa madawa wakikamatwa nchi itafanyaje sijui au ndo utakuwa mwisho wa tz..loading
 

Hivi kweli wale mabinti wakibanwa sawsawa hawatataja walikoutoa huo mzigo wa madawa na wahusika halisi?
 
Mimi nna ushahidi 100% wa mtu wa karibu yangu but sijui ni upeleke wapi..maana amesababisha maafa makubwa kwenye ukoo....maana police ndo kwanza wanamfata anawapa rushwa

Si uuweke huo ushahidi hapa jukwaani?
 
Itakuwaje Rais awe na majina ya wauza unga yasiyofanyiwa kazi kabla ya kupelekwa Ukulu? Kwanini Rais autangazie umma kumiliki majina ya wauza unga, bila ya kuwa na ushahidi?
 

kama ccm haitaondoka madarakani tutaendelea kuimba huo wimbo
 
Eti polisi kakaa sebuleni kwake anasema apelekewe ushahidi! Kuna wakati huwa najiuliza kuwa wajibu wao ni nini hasa?
anatoka na gari la umma kuelekea kazini huku raia wengine wakitakiwa kulipisha, alafu anafika ofisini kwenye kiti cha kuzunguka huku kiyoyozi kikiendelea kupuliza. ....anangojea wananchi walete ushahidi!
Likitokea deal la meno ya tembo utasikia wapo kwa maana ya wamiliki, kilo 150 zikipita JKIA utasikia ndio walikuwa lindo.
Inafikia sehemu unajiuliza kuwa hivi kuwa na bendera kama ilivyo Kenya au USA wote tu haki ya kuitwa mataifa!?

 
Eti ushahidi/sembe uhifadhiwa hata miaka kumi hadi kesi iishe/ikamilike...Teh teh teh teh teh!

Huo ushahidi baada ya miaka kumi utakuwa ushageuka kuwa unga mahindi ama muhogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…