Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Kufuatia swali la msingi lililoulizwa na Catherine magige viti maalum mkoa wa Arusha (CCM)kuhusu suala la madawa ya kulevya na kupewa majibu na wazira ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge mh Lukuvi, ambapo swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa Karatu kupitia chadema mchungaji Natse limeibua minongono baada ya kuuliza kuwa 'kazi ya serikali sio kutaja tu majina ya wauza madawa ya kulevya akitolea mfano kuwa hata mh Rais alishasema kuwa ana majina je ?nini kauli ya serikali kuhusu hilo'mh Lukuvi akijibu amesema wataendelea kutaja wengi maana hata ndani ya bunge wapo wengi tu wauza madawa majibu ambayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na kupelekea wabunge wengi kuguna na kuanza kunongona hali iliyopelekea Spika wa bunge kuwasihi wabunge kuwa watulivu ili wapewe majibu.tuendelee kufuatilia nini kinajili Dodoma.

Nadhani serekali haina nia ya dhati ya kutatua tatizo hili laiti wangelikuwa na nia ya dhati wala wasingehitaji kupelekewa ushahidi sasa nini kazi ya jeshi la polisi na usalama wa taifa kama serekali inataka raia ndio wafanye upelelezi then wawapelekee ushahidi? Kwani wangewachinguza hao wanaotuhumiwa si wangepata ukweli endapo wanahusika ama la? Je muheshimiwa raisi aliposema ana majina ya wauza unga na kuwaonya waache mara moja la sivyo atawachukulia hatua je alikuwa hana ushahidi wa kutosha. Endapo alikuwa hana ushaihidi je Ujasiri wa kusema kuwa siku zao zinahesabika na wasipoacha atawachukulia hatua aliutoa wapi? Mimi naomba serekali iwe serious na iwe tiari kuwajibika pale linapotokea tatizo. Dawa za kulevya Serious problem kwenye jamii yetu kwa hivi sasa ni kitu ambacho kimelitia taifa doa kubwa machoni pa jamii ya kimataifa sasa serekali inapodai inataka ushahidi ushahidi wa nini? Je serekali kama serekali inamikakati gani ya kukabiliana na hilo tatizo kwa kutumia vyombo vya usalama? tangu mambo haya yameanza kuzungumzwa hasa ile ya kupitishwa kwa kilo 150 za unga JNIA serekali imekuwa kimya nilitegemea hata mheshimiwa waziri mkuu au waziri wa mambo ya ndani au hata muheshimiwa raisi angesema jambo lakini walikaa kimya mpaka baadae mwakyembe alipohamua kutake some effort kuonyesha kwamba ameguswa na hili na ningeomba hata bunge limpongeze kwa hatua alizochukua lakini pia lisiache kumuhoji mchimbi ni kwanini amekaa kimya hadi leo
 
Bunge limeanza leo mjini Dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya madwa ya kulevya watajwe.Waziri Lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.Hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.Mama Kilango wa CCM na mbunge wa karatu kupitia CHADEMA ambae amehoji inakuwaje hata Raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo,waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

Vile vile mh.Lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.


MY TAKE:KAMA RAISI AMESHINDWA KUTAJA HAO VIGOGO HADHARANI, LUKUVI ATAWEZA VIPI?


Gazeti alilotaja ni JAMHURI
 
Bunge limeanza leo mjini Dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya madwa ya kulevya watajwe.Waziri Lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.Hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.Mama Kilango wa CCM na mbunge wa karatu kupitia CHADEMA ambae amehoji inakuwaje hata Raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo,waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

Vile vile mh.Lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.


MY TAKE:KAMA RAISI AMESHINDWA KUTAJA HAO VIGOGO HADHARANI, LUKUVI ATAWEZA VIPI?

Kesi ya madawa inachukua miaka kumi??

Nawashauri waende China kujifunza maana huko kesi kama hizo zinachukua siku moja tu kuisha.
 
Kesi ya madawa inachukua miaka kumi??

Nawashauri waende China kujifunza maana huko kesi kama hizo zinachukua siku moja tu kuisha.

lukuvi........
sijui jk. katoa wapi hivi vichwa panzi
 
Kwa hiyom lukukuvi anataka kusema mh rais alikuwa ana ropoka bila ushahidi? Lukuvi ana matatizo zaidi ya tunayo yafikiri.
 
swala la madawa ya lulevya si swala dogo hili ni swala zito sana, hata mtandao wake ni mkubwa saana. jiulize ni kwanini yalikuwwa yanapita airport zote?iwe kia au jkia?pale kuna watu wa usalama,mapolisi na wafanyakazi lakini bado mzigo unapita na utaendelea kupita.kwanini hujiulizi bado watu wanatumia. muda mwingine huwa najiuliza hivi na bandari ndogo za bagamoyo na mbweni hazileti mzigo kweli?na wasiwasi na ule mbweni kuna jamaa wa usalama wa taifa ila bado mambo ya ajabu yanaendelea.hii nchi imeshaoza. haifai hata kidogo.hawa mapolisi wanaolinda usalama wa raia na mali zake si lolote si chochote ifike mahali ifikapo 6pm asiwepo polisi yeyote barabarani ila awe manyumbani wamelala na hapo jeshi yaani jwtz waanze kuilinda nchi full stop tofauti na hapo hakuna suluhu,jingine awe ni mbeba unga au muuzaji au bosi wote wakikamatwa wanyongwe hadi kufa.tofauti na hapo hakuna atakayekamatwa sanasana wataendelea kutudanganya tuu.
 
Yaani utatuzi wa udhibiti wa Madawa ya kulevya ni bora hata Vijiwe vya kahawa wanaweza kuwa na gud solution thab Bunge
 
Viongozi wa serikali na majibu mbofumbofu...kwa akili ya kawaida mwananchi anaweza tafuta ushahidi wa muuza madawa ya kulevya kweli ? Mtaani kunakuwa na maneno kwamba mfano DON EMBE anauza unga taarifa zikishafikia vyombo vya Serikali ndio kazi yao kuchunguza na kuthibitisha ni za kweli au la...lakini wanposema leteni ushahidi ina maana serikali imeshindwa.
 
Yale majina ya wauza unga yalipelekwa kwa rais na nan? Je, ni watu wa usalama au raia wa kawaida?!

sasa kwa nini rais aseme anayo majina ya wauza unga kama hakua na uhakika kuwa ni kweli wanauza unga??
Ama tuseme alipewa majina ya washukiwa tu kisha mdomo ukatangulia ubongo?!
Hii nchi kiboko!
 
Wakuu,

Vita dhidi madawa ya kulevya inayoangamiza mamilioni ya watanzania inaendelea.

Gazeti la Jamhuri leo limekuja na story ndefu ya kesi na majina ya majaji wanaolinda wauza unga hao mahakamani. Majaji Pendo Msuya na Dr Fauz Twalib wametajwa na mifano ya kesi waliyochakachua ambayo huhitaji kuwa mwanasheria kujua kuwa kesi hii imechakachuliwa.

Nilitaka niwascanie gazeti lakini kutokana na kubanwa na kazi nimeshindwa.

Aidha mahakimu wa mahakama ya Temeke, Kisutu bila kuacha nyuma ofisi ya DPP ni miongoni mwa wahusika wa kulinda mtandao wa wauza unga hapa nchini kwa mujibu wa gazeti hilo.

I sadly submit

Chanzo, gazeti la jamhuri.
 
Hawa jamaa zaidi ya nusu yao ndo madigara wa unga. Wala wasikudanganye kwa kujikosha ha mjengoni.
 
Wabunge wamezomea maana wamechoka na tabia ya Serikali kutaka kupelekewa majina ilhali Mkuu wa Nchi alisema anayo,kwanini wasianze na hayo? hatimaye bunge la vioja limeanza tena.

mkuu sifongo nafikiri hamumuelewi huyu lukuvu na wala hamulazimishwi kumuelewa swala la majina hata mm ni nayo lakin nashindwa kuthibitisha lakin sasa linapokuja swala la investigation hili swala kwa wanaofahamu kwanza ni linachukua muda inabidi upandikize mchwa kwa muda mrefu laskin ni gharama sana kwaiyo wenye ushahidi wapeleke hilo ndo swala la msingi kuliko kulumbana na kuzomea wakati lukuvi anabaki kuwa lukuvi
 
Last edited by a moderator:
kwa nini huwa wanaona ugumu kuwataja, hii dhana ya kutowataja mimi inanikera kwa sababu kama mahakama haitafanya kazi yake na wananchi wakiwa wamejua ni dhahiri wananchi watawaadhibu kwa namna moja au nyingine.
watutajie tuwajue wanaoharibu jamii yetu ni akina nani haswa na baada ya hapo sheria ichukue nafasi yake.

Anza kutaja wewe unao wafahamu
 
nji yetu hii! Waziri analalamika eti watu wanatuma majina ya ajabu! Chunguza motive ya mtoa taarifa kama ni mbaya deal naye perpendicular uone kama yatakuja tena majina ya hovyo!
 
Sijawahi kuzingatia jambo lolote lisemwalo na Lukuvi, sijui kwanini!

asante umenisemea yaliyo moyoni mwangu ,ata mimi yaani namwona lukuvi kama kiere ere fulana vile wakizamani .yaana amechelewa kuzaliwa hadi kuwepo kizazi cha leo.yaani basi tuu
 
Back
Top Bottom