Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Hivi kazi ya serikali ni KUTAJA MAJINA AU KUCHUKUA HATUA. Unataja majina unamtajia nani badala ya kuwachukulia hatua. We umekamata kina dada na ma bag ya madawa si waulize tu mabegi ni ya nani kisha uwachukulie hatua. Ni aibu sana kauli kama hizo kubungeni. Only in Tanzania!
 
Kufuatia swali la msingi lililoulizwa na Catherine magige viti maalum mkoa wa Arusha (ccm)kuhusu suala la madawa ya kulevya na kupewa majibu na wazira ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge mh lukuvi,ambapo swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa karatu kupitia chadema mchungaji Natse limeibua minongono baada ya kuuliza kuwa 'kazi ya serikali sio kutaja tu majina ya wauza madawa ya kulevya akitolea mfano kuwa hata mh Rais alishasema kuwa ana majina je?nini kauli ya serikali kuhusu hilo'mh Lukuvi akijibu amesema wataendelea kutaja wengi maana hata ndani ya bunge wapo wengi tu wauza madawa majibu ambayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na kupelekea wabunge wengi kuguna na kuanza kunongona hali iliyopelekea Spika wa bunge kuwasihi wabunge kuwa watulivu ili wapewe majibu.tuendelee kufuatilia nini kinajili Dodoma.

Hata yeye yumo, kuna Dada mmoja alisoma UDSM alikwenda kwake kutaka msaada apate kazi serikalini alichomjibu kilimkimbiza yule dada ofisini bila kuamini kama kweli ni yeye amemwambia vile. Alisema "Kazi kwa sasa ni vigumu sana kupata ninachoweza kukusaidia nikutafutie passport ili uwe unasafiri kwenda Pakistani tufanye biashara, japo hakueleza biashara gani hasa huko Pakistani kunafahamika. Kwanini anajifanya yeye ni msafi wakati hata yeye alishawahi kushawishi kazi hiyo. Sina update kwa sasa lakini kimya hiki cha serikali kinasababishwa na wenyewe kwa kuwa wanahusika. Kila siku wanasema wanyo orodha ya wauza madawa hatuitaki orodha ya wauza madawa ya kulevya tunachotaka ni kuwakamata hao wanaouza na wale wanaowatuma kuyaleta hapa nchini kwanini kila mara mna pinpoint wauzaji badala ya waagizaji?
 
Shortly namuonea sana huruma Dada Catherine Magige kwa kujitosa katika sakata hili akumbuke kwamba Amina Chifupa aliondoka hapa duniani kwa sababu ya msimamo huo huo, Mungu akulinde Catherine na Natse. Unganeni na akina Mwakyembe, Kigwangala na wengine wenye moyo wa kuthubutu kuingia vitani japo hawana silaha dhidi ya adui wanaye kula meza moja.
 
Mimi nna ushahidi 100% wa mtu wa karibu yangu but sijui ni upeleke wapi..maana amesababisha maafa makubwa kwenye ukoo....maana police ndo kwanza wanamfata anawapa rushwa
 
Majina aliyonayo JK kafanyia kazi gani mpaka wananchi tupeleke mengine. Labda kama anaandika kitabu ili akizindua yawemo yote!!!!
Watathubutu kuwataja wanaowapa pesa za uchaguzi?? Maana ndio wauzaji wakuu, hapa ni unafki tu tutashuhudia
 
kwa nini huwa wanaona ugumu kuwataja, hii dhana ya kutowataja mimi inanikera kwa sababu kama mahakama haitafanya kazi yake na wananchi wakiwa wamejua ni dhahiri wananchi watawaadhibu kwa namna moja au nyingine.
watutajie tuwajue wanaoharibu jamii yetu ni akina nani haswa na baada ya hapo sheria ichukue nafasi yake.
 
Wamtaje na mwanamfalme basi tujue moja aaagh!!
Tumechoka sasa na longolongo za lukuvi..
 
Bunge limeanza leo mjini Dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya madwa ya kulevya watajwe.Waziri Lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.Hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.Mama Kilango wa CCM na mbunge wa karatu kupitia CHADEMA ambae amehoji inakuwaje hata Raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo,waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

Vile vile mh.Lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.


MY TAKE:KAMA RAISI AMESHINDWA KUTAJA HAO VIGOGO HADHARANI, LUKUVI ATAWEZA VIPI?
kwenye bold tayari kaisharuka kimanga
 
Mimi nna ushahidi 100% wa mtu wa karibu yangu but sijui ni upeleke wapi..maana amesababisha maafa makubwa kwenye ukoo....maana police ndo kwanza wanamfata anawapa rushwa

Mtaje hapa tumuwashie spotlight fasta..
 
Hata hivyo,waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

MY TAKE:KAMA RAISI AMESHINDWA KUTAJA HAO VIGOGO HADHARANI, LUKUVI ATAWEZA VIPI?
hivi nchi yenye wakazi karibia million 50 imefikaje hatua hii!??? Haya ni dunia.

 
Usitegee chochote kwenye bunge lisiko la meno!!

Tatizo kubwa mkuu ni MACCM yamejaa bungeni,otherwise lingeweza kuwa na meno,na meno limekosa kuanzia kwenye kanuni,maana hata wanapobanwa na wabunge makini wa CDM mwisho wa siku spika anawapigisha kura za ndio na hapana na ndipo mambo huishia hapo.
 
Sidhani kama Lukuvi anajielewa..! Mzee huyu anaamini bungeni ni sehemu ya chenga Za porojo and nothing special. Bunge kwake Yeye ni Kijiwe Cha POROJO-lianze-liishe potelea mbali. Lukuvi naamini haamini Kama kuna kitu Cha Maana ambacho bunge linaweza fanya. Ni Mtu aliyejaa kiburi, maringo, jeuri Na majigambo flan ya upuuzi kabisa. Ati tutawataja leteni ushahidi hivi anamtega nani?. KWANINI mawaziri hawa hawako serious kiasi hiki?
 
bunge limeanza leo mjini dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya madwa ya kulevya watajwe.waziri lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.mama kilango wa ccm na mbunge wa karatu kupitia chadema ambae amehoji inakuwaje hata raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo,waziri lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

Vile vile mh.lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.


My take:kama raisi ameshindwa kutaja hao vigogo hadharani, lukuvi ataweza vipi?

mama kilango [ na idd azan ] nao wanataka watu watajwe????? Defensive position wallah!!!
 
Majina sijui bosi wako akiwa adui yako utapata tabu serikali ya ccm ndo inatesa wananchi na madawa ya kulevya watu wakaribu na ccm ndo wanafanya biashara iyo ccm ni janga
 
Back
Top Bottom