Bungeni Jioni Hii….Giza haliondoi kivuli.

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Bungeni Jioni Hii….Giza haliondoi kivuli.

Herbet Mtangi…

Ukisimama na kivuli kinasimama, Kivuli hakifukuzi mwanga bali kinafuata Mwanga. Hivyo giza haliondoi kivuli Bajeti mbadala ya upinzani Bungeni ni kama kivuli haina Tija kwa serikali ya CCM.

Haya maneno ya Kishabiki yatakwisha lini kwa hawa wabunge hawa wenye fikara na mitazamo ya kishabiki?

Analalamikia MSD suala nyeti kabisa ambalo limezua maswali mengi kwa wabunge waliotembelea Bohari hilo la madawa la Taifa.

Huko napo ni uozo na ufisadi uliofichika haswa mpaka mfagiaji ana Bungalow, Miradi ya Uhakika ya kumwingizia riziki na usafiri wa ukweli kama wewe unafanya huko na hali yako ni hohehahe, unapigwa mswaki na wenzio.

Analalamikia kero ya kutopatikana kwa Dawa na huduma ya matibabu bure kwa wazee na watoto kama ilivyo sera ya Afya ya Taifa.
 
Mh. Martha Mlata anaongea sasa, ila anaongea mambo yale yale ambayo ni ya kishabiki kabisa
 
anazungumzia saula la kuongeza ambulance na kuboresha huduma za afya kwa akina mama vijijini
 
anahoji masuala ya afya vijijini kutokuwa na idara maalumu ya kushughulikiwa

analalamikia mishahara hewa kuwa inatia aibu hasa pale ambapo hata mtu aliyetangulia katika haki watu wanachukua fedha bila huruma
 
Anaendelea kusisitiza umuhimu wa huduma za bure kwa walemavu, watoto, wazee na wajawazito
 
Anauliza hivi serikali ina takwimu hasa ni wagonjwa wangapi walikwenda kupata kikombe kwa babu na ni tatizo gani sugu hasa likaagiziwa dawa kuliko kuagiza madawa yasiyokidhi mahitaji ya wananchi huku fedha zingine hazitumiki...anaunga mkono hoja
 
Mh. Mhonga luhanya: anahoji kuhusu tatizo la ukeketaji kwa wanawake. anasema viendo hivyo vinatokana na shinikizo la wanaume kutoka makabila hayo kuwa hawako tayari kuoa mwanamke aliyekeketwa
 
huyo luhwanya kagusia kamgomo ka ngono kaitishwe tz kwa siku angalau tano hivi............... hadi wanaume watambue kuwa wanawake ni muhimu................... eti watawaficha na watoto wao wa kike wanaume wasiwaone ng'o!!.............
 
Wapeni wauguzi haki zao watatuua kwa hasira, mishahara na malimbikio yao ni ya Muda mrefu wanatuhudumia huku wana msongo wa mawazo kwa kutokupata mshahara wao
 
TIBA ASILI:

Kuna mdau alitumia dawa za kuongeza nguvu za kiume huko Dar badala ya kuongeza nguvu mashine ikaongezeka kilo kumi na mbili, sasa pata picha hapo endapo akina mama wakiwa na ujauzito wa kilo 4 tu ni tabu kutembea

Hoja yake na madai ya msingi ni kuendelea kushamiri kwa Tiba asili bila wizara husika kuzikagua, hasa masai na Wachina.
 
  • Thanks
Reactions: Obe
MADAWA YA KULEVYA:

Anahoji kuhusu mirungi na vijana wanavyotafuna kwa fujo huku macho yametuna kama fundi saa, anasema hataji ni wapi.

Anamtaka waziri akija ajibu ni vipi wanawapima madereva kujua kama hawatumii madawa ya kulevya hasa mirungi

UZAZI WA MPANGO
 
kasema wanawake ndio waathirika wakubwa wa dawa za kuongeza nguvu za kiume............. eti mtu akishakula hizo dawa zake za kuongeza nguvu huwa ni vurugu tupu ndani..................... waheshimiwa wakavunjika mbavu.................
 
Fedha zilizotengwa ni kidogo itakuwaje tufikie mipango mizuri ya maendeleo kama tumeshindwa kucontrol ongezeko la watu hii haingii akilini kama tumekusudia kuleta maendeleo

Mhhhhh hapo pagumu sijui mnasemaje wadau
 
TIBA ASILI:

Kuna mdau alitumia dawa za kuongeza nguvu za kiume huko Dar badala ya kuongeza nguvu mashine ikaongezeka kilo kumi na mbili, sasa pata picha hapo endapo akina mama wakiwa na ujauzito wa kilo 4 tu ni tabu kutembea

Hoja yake na madai ya msingi ni kuendelea kushamiri kwa Tiba sili bila wizara husika kuzinguza, hasa masai na Wachina.
uingizwaji wa dawa hizi hapa pamoja na nyingine ambazo hazina viwango, kunaonesha kuwa mipaka yetu inavuja, na tbs/tfda wapo
 
kasema wanawake ndio waathirika wakubwa wa dawa za kuongeza nguvu za kiume............. eti mtu akishakula hizo dawa zake za kuongeza nguvu huwa ni vurugu tupu ndani..................... waheshimiwa wakavunjika mbavu.................

Ila pale kwenye kuongezeka hadi kilo kumi na mbili kama kapiga porojo hivi, ila ukweli anaujua yeye zaidi Mkuu
 
Mwisho: anasisitiza dawa zifike katika hospitali za wilaya...MSD Mpoooo???
 
Kajuajeee??????
kasema wanawake ndio waathirika wakubwa wa dawa za kuongeza nguvu za kiume............. eti mtu akishakula hizo dawa zake za kuongeza nguvu huwa ni vurugu tupu ndani..................... waheshimiwa wakavunjika mbavu.................
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom