Bungeni: Askofu Gwajima agoma kukalia kiti na kutumia kipaza sauti alichoandaliwa na Kamati ya Maadili

Ingekuwa ni wa upinzani angekuwa Segerea au Ukonga kwa kuikashifu serikali. Mnyika katamiwa ajieleze kwa kumwita rais mwongo. Huyu kaitwa kamati ya maadili kwa kumtuhumu rais na waziri kupokea rushwa anatembea huru kabisa kifua mbereeee
Shida mnapenda sana habari za kusikia!
Naomba clip inayomuonyesha Gwajima kasema raid kapewa hela hapa!

Uzuri nimeangalia na kusikiliza clip zote za Gwajima live sijaona mahali akimtaja rais na waziri kuwa wamepewa hela!
Hiyo aliisemea wapi,tunaomba ushahidi!
 
Mbona huwa anajigamba kwamba Mungu hashindwi na kitu na ndiye alituvusha kwenye wimbi la kwanza bila chanjo iweje Mungu huyo huyo leo asimwamini?
Hajigambi ndivyo ilivyo!

Mungu alituvusha!

Sa kukataa kukalia kiti ndo kutomuamini Mungu?

Hebu someni neno vzr ndo maana tuliachiwa msaidizi Roho Mtakatifu kwa akili ya kutupa taarifa zilizopo,zijazo na zilizopita!
Kama kapewa hiyo taarifa asikalie ulitaka aache kumtii Mungu wake kwa kufuata maelekezo awafurahishe watu km nyie?

Kasome neno tena usikariri andiko!
 
Rashidi bwana. Sasa kama anaweza kufufua nini kitamtisha tena duniani, uchawi? Sumu? Mzee wa amfifiro ana imani haba
Pole sana...

Ni kwa sababu hujui jinsi Mungu Yehova anavyolinda watu wake...

Hayo ndiyo maisha ya MTU WA ROHONI contrary na MTU WA MWILINI maana maandishi yako haya yametoka katika fikra za MTU WA MWILINI, wewe...

Kuna wakati anaweza kukuambia kwa njia ya Roho wake mtakatifu kuwa:

å Ukifika usikae kwenye kiti kile, waambie wakuletee kingine; na usitumie microphone ile, waambie wakupe nyingine...

å Usipite njia hii, pita ile

å Au usifanye jambo hili kwa namna hii, fanya kwa namna hii

å Usikae hapa, kale pale

å Usiishi nchi ile, kaishi nchi ile nitakayokuonesha nk

Huku ndiko kuishi kwa KUONGOZWA NA ROHO na siyo kwa HISIA ZA MWILI AU MATAMANIO YA KIBINADAMU...

Kama wewe ni Mkristo wa kweli, ukaacha kutii sauti ya uongozi wa Roho Mtakatifu [Holy Spirit], utaangamia na kuteswa na shetani kupitia mwakala [satanic agents] wake hapa duniani mpaka utakoma....

Kwa mfano [Biblical examples];

1. Yusufu na mkewe wakaonywa na Roho Mtakatifu wamkimbize mtoto Yesu wakamfiche Misri kwa sababu Herode alikuwa anamtafuta amuue... [Soma: Mathayo 2: 13 - 14]

## Je, unadhani Mungu hakuwa na uwezo kumlinda mtoto Yesu hapohapo alipokuwa na kumwangamiza Herode na serikali yake yote kwa usalama wa Yesu...?

Jibu ni HAPANA, kwa sababu ktk kila jambo Mungu ana KUSUDI lake na ana utaratibu wake kulitenda...

2. Abraham [Ibrahimu] aliamuriwa na Mungu atoke katika nchi ya Ukaldayo ya Uru alikoishi miaka mingi na
 
Je kama kaoteshwa hivo na Mungu wake asikalie wala kutumia mic aliyoikuta hawezi kupingana na maono yake
Hii huhitaji kuoneshwa na Mungu,ni mitego ya kawaida ya dola zote duniani pindi unapoonesha yafananayo na ya Rashidi dhidi ya dola
 
Yupo sahihi, na Mwenyekiti kampa haki zake.. Ila kwenda kwenye maadili na unasindikizwa na Polisi inajenga hofu kwa walio kuita wana nia gani kwako..
 
Yaani hivi ni kweli kuwa kashindwa kuyakemea yale ' mapepo'yashindwe, yaliyokuwa kwenye kiti na 'mic' ?' kweli hiki ni kizungumkuti na walio na macho wameona...........
Anajifanya mcha Mungu halafu anakuwa na imani za kishirikina! Ni kipi kinamshinda Mungu iwe uchawi au sumu?
 
Hilo Mc Linaloongea hapo km linataka kumkazia kitu hivi Gwajima, ila kuna nguvu flani zililishinda, likakubali kiaina aina gwaji kubadili MIC, na kiti!! lkn kama lina kitu kinalikereketa moyoni lime kimiss!! linashindwa tamka!!! sasa naijua ccm..

Mtaona halitapata kuwa na nafasi ya maana Tena ccm! hata ya u MC ! kwa sababu kamati ya mauaji ya CCM imelistukia jambo hili ku fail?? kuwa huenda MC limekula cha juu kutoka kwa Gwaji boy! make limeshindwa kumkomalia akalie hicho kiti!!

hilo moja! mbili hivi ccm wanajisikiaje kuwa wauaji? yameridhika kabisaaa kuwa mumiani watu? hivi wanajisikiaje kuwa kwenye hii kamati ya mauaji tena wanachukua picha kabisaaa!
 
Back
Top Bottom