Askofu Dkt. Josephat Gwajima amechangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

JOSEPHAT GWAJIMA AKICHANGIA BUNGENI BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Mbunge wa Jimbo Kawe lililopo Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima amechangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega ya Tsh. Bilioni 295.6

Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima alianza kwa kumshukuru Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa bidii yake anayoifanya katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linaendelea kujengwa na kubakia salama.

Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima alisema kwmaba Kwenye document ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi inaonesha Sekta ya Uvuvi inachangia asilimia 1 ya pato la Taifa, jambo ambalo ni hatari kulisikia au kusemwa mbele ya watu wenye akili timamu.

Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima alisema kuwa Tanzania tuna Mikoa 16 ambayo iko kando ya Maziwa, na Mikoa 5 imezungukwa na Maji Chumvi (Bahari) pamoja na Zanzibar yote. Haikubaliki sekta ya uvuvi kuchangia asilimia 1 pekee ukilinganisha na rasilimali tulizonazo.

Aidha, Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima aliongeza kuwa Ni muhimu sana kuifanya Sekta ya Uvuvi kuwa na Mamlaka, kama tulivyofanya kwenye Wakala wa Huduma za Misitu na TANAPA, tukifanya hivyo tutaongeza chachu ya kutumia rasilimali ya Maji tuliopewa na Mwenyezi Mungu na kuongeza pato la Taifa.

Vilevile, Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima alisema wakati umefika kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na vision (maono) ya muda mrefu ya nchi, kwani alipata faraja alipoona uzinduzi wa mpango wa taifa lakini alikuwa disappointed kuona ni wa miaka 20, angalau tungewaza miaka 50 ya mpango wa Taifa.

"Tunasema tuna ng'ombe milioni 36.6, mbuzi milioni 26.6 na kondoo milioni 9.1, tunazalisha lita za maziwa lita bilioni 3.6, wakati huo huo tuna idadi ya mifugo yote hii na lita zote hizi za maziwa lakini tumetoa vibali 605 vya watu kuingiza maziwa nchini" Askofu Josephat Gwajima

"Ziwa Tanganyika linategemewa na nchi nne na sehemu kubwa ya ziwa ipo Congo DR na samaki huwa wanahama hama. Hivyo uamuzi wa kufunga ziwa Tanganyika si uamuzi wa kisayansi, ni uamuzi ambao utainufaisha nchi nyingine kwamba kile ambacho ulipaswa kukipata wewe atakipata mwingine kwa kuwa wengine wataendelea kuvua" Askofu Dkt. Josephat Gwajima, mbunge wa jimbo la Kawe.

FvJ9u_QWIAE5x-K.jpg
 
..alitakiwa awasemee wavuvi walio ktk jimbo lake la Kawe wanaovua ktk bahari ya Hindi.

..pia ile ahadi ya kupeleka vijana kwa mafunzo Japan na Alabama-USA mbona bado hajaitekeleza?
 
..alitakiwa awasemee wavuvi walio ktk jimbo lake la Kawe wanaovua ktk bahari ya Hindi.

..pia ile ahadi ya kupeleka vijana kwa mafunzo Japan na Alabama-USA mbona bado hajaitekeleza?
Nakazia....hii itakuwa ni ahadi ya pili kutoitekeleza. Ya kwanza ni ya kumfufua Amina Chifupa kipindi kile anafufua misukule feki
 
Back
Top Bottom