Bunge: Wafanyakazi hewa wamerudi, mamilioni yalipwa

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imebaini viashiria vya kuibuka tena kwa mishahara hewa Serikali baada ya kiasi cha mishahara kutoka Hazina kutofautiana na mahitaji halisi ya mishahara katika mfumo wa Lawson.

Hayo yamesemwa leo Alhamis Februari 17, 2022 na Mwenyekiti wa LAAC, Grace Tendega wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za Kamati hiyo katika kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Ametoa mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ambapo mahitaji ya Lawson ilikuwa ni Sh13.16 bilioni lakini Hazina ilitoa Sh13.30 bilioni na hivyo kusababisha ziada ya Sh145. 73 milioni.

Amesema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mahitaji ya Lawson yalikuwa ni Sh17.67 bilioni lakini Hazina ilipeleka Sh17.88 bilioni hivyo kuwa na ziada ya Sh209 milioni.

Ametaja pia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mahitaji ya Lawson yalikuwa Sh17.06 bilioni lakini Hazina ilipeleka Sh17. 37 bilioni na ziada ya Sh309.34 milioni.

“Hoja hii inaashiria kwamba serikalini kuna usimamizi hafifu wa mfumo wa mishahara. Udhaifu huu usipodhibitiwa utaibua upya mishahara hewa serikalini,” amesema.

Mwananchi
 
Kwani waliondoka lini? C tu lile jama lilibadilisha tu kuondawa watu wasio lipenda na kuweka wa kabila lake tu
 
***** zao wameanza tena, kwani hatuwezi thibiti hii kitu hata kwa kuipa kesi uhujumu uchumi au kifungo kikali jata miaka 20 kwa wausika. Lawama iende kwa treasurer na waahasibu wote wa mikoa
 
Uhuru wa maoni sasa upo. Mapungufu tutakayowekewa wazi bila woga basi Ufisadi utaonekana ni mkubwa kweli kulinganisha na nyakati nyingine na hapo utaambiwa umeanza upya ulikuwa haupo.

Kuna awamu uhuru ulikuwa wa kutosha mpaka Rais akapachikwa jina dhaifu.
 
Kumbe ndio maana TRA wanahimiza tudai risiti mapato yaongezeke...kuvuja kunaenda sambamba na kuongeza mapato.
 
Wafanyakazi hewa hawakuwahi kuisha! Wangekamatwa na kuwajibishwa waliokuwa wanachukuwa hiyo mishahara ya wasiokuwepo ingeeleweka.....lakini kubaini 'wafanyakazi hewa' bila kuwagusa wafaidika ilikuwa ni ulimbukeni.
 
Back
Top Bottom