Kisambusa
Member
- Aug 8, 2022
- 27
- 16
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum kwenye ujenzi wa stendi ya Kimataifa iliyopo kata ya Mfumuni, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya maelezo ya mradi kujikanganya.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seleman Zedi amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 3, 2022 mara baada ya kamati yake kuchambua CAG, zinazoishia Juni 30, 2021.
“Baada ya mahojiano yetu na halmashauri ya Moshi, tumemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum kuhusu mkopo wa Tsh. 20 bilioni ambao manispaa ilikuwa imeingia mkataba na benki ya TADB,” amesema.
Amesema wameagiza ukaguzi maalum kwasababu ya mkanganyiko wa maelezo ya manispaa hiyo kwasababu mara ya kwanza walituambia waliingia mkataba na TADB kukopa Tsh. 20 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo.
Hata hivyo, Zedi amesema baadaye walipata barua ya zuio kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wasipate huo mkopo lakini wakati huo huo ndani ya mkopo huo kulikuwa na Tsh. 378 milioni ambazo ni malipo ya mhandisi mshauri.
“Wametuambia wazuiwa wasiendelee na ule mkopo lakini hapo hapo wanatuambia, zile Tsh. 378 milioni yaani benki ya TADB walitoa fedha hizo kumlipa mhandisi mshauri ambaye anaitwa Digital Space Consultant,” amesema Zedi.
Amesema fedha hizo ni sehemu ya mkopo waliouomba na benki ya TADB, licha ya manispaa kusema walizuiliwa na Tamisemi kukopa fedha hizo Tsh. 20 bilioni.
“Tukaona iweje unatuambia fedha Tsh. 378 milioni ambazo ni sehemu ya mkopo wa Tsh. 20 bilioni ambazo zilizuiwa zilitolewa? Tumeagiza CAG akafanye ukaguzi kuhusu mkopo huo,” amesema ambaye ni Mbunge wa Bukene.
Amesema kwa maelezo ya manispaa, walisema walipeleka andiko Hazina kuomba Tsh. 20 bilioni kwa ajili ya mradi huo lakini walikubaliwa Tsh. 7 bilioni.
Hata hivyo, amesema hadi sasa wamepewa Tsh. 2 bilioni na kwamba fedha zilizokubaliwa ni ndogo sana kukamilisha mradi huo ambao unahusisha ujenzi wa hoteli katika eneo hilo.
Chanzo: Mwananchi