Bunge livunjwe kwa sababu limejaa wahuni - Ole Sendeka

Ni aibu kubwa sana kwa serikali kushindwa kushughulikia tatizo la madktari wetu kabla halijaleta madhara matokeo yake wamesubiri madhara ya mgomo ili waje na vitisho vya kipuuzi na vya kitoto. Hakuna daktari anayeogopa kufukuzwa kazi, daktari wa Tanzania hana tofauti na daktari wa india tofauti ni technolojia tu, mkiwafukuza mtakutana nao hospitali za nje mnapokwenda kutibiwa ukimwi wenu. Pumbavu zenu.
 
hayo unayoyaota hayawezi kufanyika kwa sababu madaktari wamemdharau waziri mkuu ambaye alienda kuwasikiliza wao wakamkwepa
Wamemdharau au kajidharaulisha mwenyewe? Lengo la kuita madaktari jumapili ni nini?au alitaka
awapumbaze kabla ya jumatatu akijua itajulikana kuwa posho za wabunge zimepanda!! Shame of you
wote mnaodharau wataalamu na kuendekeza wanasiasa mafisadi wa Tanzania.
 
NAUNGA MKONO, wabunge posho zenu kubwa kuliko madaktari kwa nini au mmesoma sana kuongea na kulala Bungeni?

Mkuu nashukuru kuliona hilo kwani nami nilikuwa nikijiuliza hiln swali pasipo majibu
 
Jamani tajeni tarehe hapa au tumieni njia mbadala ................... tujiandae kufa kwa ajili ya nchi yetu na vizazi vyake. Maneno ni mengi na watu wanasubiri. Let this start with us! Ubungo? ....Uwanja wa Uhuru....
 
Fikra za kimasaburi hizi "Bunge livunjwe, Rais ajiuzulu na Waziri mkuu awajibishwe".... hawa wameshaambiwa atakayeendelea kugoma atakuwa amejifukuzisha kazi.... wewe analeta upupu hapa! Hivi unajua madhala ya haya unayotaka yatendeke?

Acha ushamba na ujinga wako em ainisha hayo unayodai madhara, vinginevyo kaa kimya usituharibie hali ya hewa...nyang'iau ww.
 
Spika wa bunge la Tanzania ndiye chanzo kikubwa cha ukosefu wa uaminifu wa wabunge wa Tanzania kwani ameshindwa kusimamia sheria/kanuni/taratibu na nidhamu za wabunge wawopo bungeni na nje ya bunge. tuhuma za wabunge kupokea rushwa hazijaaanza leo wala jana baadhi ya wabunge wameshasemwa ni wala rushwa wengine wanatuhumiwa kupokea rushwa na wengi na vitabu vya nje vimwaandika kama ni manguli wa kupokea na kutoa rushwa. Bunge limekosa kabisa hadhi ya kuwakilisha watanzania. Nashauri Bunge livunjwe kwani halina maana tena ya kutuwakilisha. Bunge linanuka Rushwa.

Wabunge wetu kwenye kamati mbali mbali wakiwa kama ndio waangalizi na wasiamamizi wa mali na utendaji wa serikali wamekuwa wakitumia rushwa za jumla za ama kulipiwa hoteli/usafiri/chakula na posho na wale wanaokwenda kuwakagua hii ni rushwa.

kamati haziwajibiki kwa uozo na madudu yanayofanywa ama na viongozi wa kamati hizi au wabunge wa kamati. Kama kweli ndani ya kamati mjumbe anakula rushwa na mwenyekiti wa kamati anajua kwa nini asijiuzulu na kama kamati hizi zinatuhumiwa kwa rushwa na Spika anajua na hakuna anayewajibishwa tunamhitaji Spika wa nini kwa nini Spika asiwajibike????

Leo hii eti swala ni wabunge wa chama gani wamekula Rushwa na majina yapo ila wananchi wameachiwa kazi ya Utabiri na kuwa Sheikh Yahaya come on.

Bunge limekosa hadhi halifai tena hakuna jema lolote linatoka dodoma zaidi ya kuongezeana mishahara na kula rushwa.

Kama waalimu, madaktari wameweza kugoma kudai haki zao wakati umefika wananchi kugoma bunge livunjwe hatuwataki wabunge hakuna wanalotusaidia zaidi ya kula rushwa.

J. K. Nyerere aliwahi kusema mke wa mfalme akituhumiwa tu kufanya uzizi anakuwa amepoteza kabisa hadhi ya kuwa mke wa mfalme. Leo wabunge wanatuhumiwa kupoke/kutoa/kuomba Rushwa halafu bado wapo tu wanataka kujitetea. Swali la kujiuliza kwanini uhisiwe wewe , ni nini kimefanya wakuhisi je mwenendo wako uko sahahihi!! kwanini ujiweke kwenye mazingira ya kuhisiwa. Ukihisiwa uwezekano wa kupokea nafikiri ni mkubwa sana. Rushwa ziko za aina kuna za hali, mali, ngono, biashara, tenda, usafiri, chakula,magari, mashamba,cheo,elimu,madaraka,kura,kampeni nk

Ukiwa mbunge au kiongozi kama umepokea rushwa ya aina yeyote kati ya hizo au zingine wewe ni mla rushwa na hutufai kuwa kiongozi wetu.

Hatutaki wala rushwa tumechoka na wabunge njaa na tamaa. Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya serikali isiyowajibika na Spika asiyejua kazi yake . Tunahitaji uwajibikaji sio siasa za maji taka. Wala Rushwa wapelekwe mahakamani ili wasiwezi kuwa viongozi tena.

Chief Mkwawa wa Kalenga
Tumechoka kulia machozi yetu mmeyazoea tunataka mtoke ama tutawatoa
 
[h=2][/h]JUMATANO, AGOSTI 01, 2012 06:34 NA KHAMIS MKOTYA

RAIS Jakaya Kikwete, ameombwa kulivunja Bunge kutokana na chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi kukumbwa na kashfa mbaya ya rushwa.

Ombi hilo, limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, wakati alipokuwa akizungumza na Mtanzania kuhusu tuhuma za rushwa bungeni.

Akizungumzia suala hilo, Dovutwa alisema wabunge waliohongwa wamelichafua Bunge na kwamba kitendo hicho ni aibu kwa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Kuchafuka kwa Bunge, kumekuja baada ya kufichuliwa kwa taarifa kwamba baadhi ya wabunge wamehongwa na baadhi ya kampuni za mafuta ili kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Dovutwa, ambaye aliwahi kugombea urais 2010, alisema wananchi wamekosa imani na mhimili huo uliokuwa umesalia baada ya mihimili mingine kulalamikiwa kwa rushwa.

Alisema Rais Kikwete anapaswa kuonyesha kukerwa kwake na kitendo hicho kwa kulivunja Bunge ili kumaliza kiwingu hicho, kwani Spika wa Bunge hana uwezo wa kuondoa rushwa bungeni.

“Bunge letu limepoteza mwelekeo kutokana na kashfa hii, hili ni jambo la aibu kwa Bunge na wananchi wamekosa imani nalo, kwani kiranja wao naye ameingia kwenye mtego.

“Wananchi sasa wamebaini kuwa kumbe wanapoona wabunge wanasema kwa nguvu wanafanya vile kutetea maslahi yao binafsi na si kwa ajili ya maslahi yao.

“Rais ndiye mkuu wa nchi na mkuu wa dola, japokuwa dola imegawika katika mihimili mitatu, hapa anapaswa kulivunja Bunge tuingie katika uchaguzi kujenga heshima,” alisema.

Alitaka wabunge wanaotuhumiwa wasimamishwe ubunge ili kupisha uchunguzi, huku akishangaa majina ya wabunge hao kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge.

Alisema uwamuzi wa Spika Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini haina athari yoyote na kueleza kuwa hata kamati nyingine, ikiundwa haitakuwa salama kutokana na wabunge hao kuchafuka.

 
Haya Chama cha UPDP chamtaka Rais alivunje BUNGE kwa RUSWA na UFISADI...

Ooooh, Oooooh hii ilikuwa agenda ya Mh. Zitto Kabwe wakati Uleee, lakini Rais akaja akafanya Mabadiliko ya Mawaziri

Zitto Kabwe bado akasema ataliita bunge sababu bado hana Imani na Waziri Mkuu na Bunge lake; ilikuwa tarehe 17

Mwenzi April ikapita Mwezi ukapita sasa ni Miezi; hakutuambia ni kwanini hakuiweka HOJA yake pamoja na kuwa na

Signature za kutosha... Angeokoa JAHAZI LA MAFISADI na yeye Mwenyewe...

* UNAONA wenzetu wanasema ACTION SPEAKS LAUDER THAN WORDS not the other way round...
 
Mimi huwa nashangaa sana, bunge linapofika hatua ya kujadili mambo mhimu au miswada mhimu inayogusa maslahi ya wananchi direct huwa wanaibua vitu vingine visivo na uzito lakini vinapewa uzito wa ajabu sana.Tunajadili mstakabali wa madaktari then anaibuka Jairo, sasa tunajadili PPF, NSSF migomo ya walimu sasa yote hayo mhimu yanafunikwa eti na kashfa ya TANESCO shirika ambalo kila mtu anajua hata waliboreshe vipi haliwezi kupona maana lilishakwisha kuchafuka tokea enzi na enzi. Please naombeni sana mtoke Dodoma na majibu mwafaka ya mafao yetu mwachane na hayo mambo ya TANESCO maana Tanzania yetu hakuna msafi, shughuikieni kwanza mafao yetu kama ni kulala gizani sie tulishazoe hakuna jipya
 
Nani anapenda tena kumaliza hela kwa kuruka hewani na helcopter wakati hata mifuko ya hifadi ya jamii inafirisika,hapo itabidi itumike tu busara ya funika kombe mwanaharamu apite
 
hivi huyo mpuuzi anayejiita mpinzani si ndiye alimuendorse jk dakika za lala salama...shut the hell up puppet
 
Bunge la bajeti safari hii Olesendeka kapoteza umaarufu kiasi cha kutuhumiwa kula rushwa. Ndio maana anaona bora kuanza upya
 
Kwa kweli nimeangalia bunge na kugundua halina maana yoyote na haliisaidii au kuisimamia serikali.wabunge wako kishabiki zaidi wanaboa sana!

Halina maana hivyo livunjwe rasmi na tuitishe uchaguzi upya.

Kuanzia sasa upigaji wa kura bungeni uwe wazi na ijulikane nani alipiga kura ipi katika hoja iliyojadiliwa ili makosa yanapotokea mbeleni tuwahukumu waliohusika.

Update:
Mwananchi | July 13, 2011

Ni kweli Ole Sendeka bunge hili linastahili kuvunjwa sisi wenye akili tuliona bado mapema KABISA, eti wakina Aden RAge nawo wabunge utegemee bunge hilo liwe bunge , thubutu ni usanii mtupu.Aden Rage nae mbunge anawakilisha watu wenye akili, hainiingii akilini kabisa.
 
​bunge lina wapuuzi kama mwigulu, lusinde,mapumba, john komba,anna makinda hatuwezi kuendelea kwa hawa makada wa chama cha mafisadi
Kweli bunge limejaa wahuni wengi sana! Sugu, Wenje, Lema na wengine
 
umejaa siasa za maji taka lema sio mbunge ukisoma mistari usisahau kukariri akili ndogo kuongoza akili kubwa(ccm)
 
Serikali nzima imenuka rushwa sio Bunge, mahakama, Polisi, na taasisi zote hata wabunge wangu siwaamini tena cdm nzima nawaamini viongozi watano Ndio nadaiwa (the big five fighters)ccm wako watatu tu sasa watu 8 Kati ya watu miatatu mabadiliko ni njozi I hate all of the politician except those (8 big fighters)
 
Hali ni mbaya kila mahali, muhimu ni serikali kuwa makini na kubadilika. Kwa mwendo huu wa sasa Tanzania tutatimuliwa vumbi na nchi zote za Afrika.
 
Back
Top Bottom