Bunge livunjwe kwa sababu limejaa wahuni - Ole Sendeka

umejaa siasa za maji taka lema sio mbunge ukisoma mistari usisahau kukariri akili ndogo kuongoza akili kubwa(ccm)

Mtu wa kwanza kukariri ilitakiwa uwe wewe..Ila ni tatizo la kujifanya unajua sana..
Angalia kwanza hii thread imeletwa lini na Lema amefukuzwa ubunge lini..
 
Siasa UCHWARA, Wabunge WAHUNI, SILLY Government, Serikali legelege... Wonderful quotes of our time!
Uhuni upo wa aina nyingi. Kuzomeana kama vile wako Kariakoo, Kukacha vikao vya Bunge, Kupiga kelele wakati shughuli za Bunge zinaendelea, Kushabikia mambo ki CCM! Waongoza vikao wanafanya hivyo KIHUNI.. Wabunge kushindwa kuzungumza . Kwa mfano Edward Lowassa hajachangia CHOCHOTE katika kikao kinachoendelea, hali kadhalika wabunge wengine wengi tu....UDHAIFU, ULEGELGE, UHUNI.. UUCHWARA!....Kick them out!
 
Ni kweli bunge limepoteza maana kwa sasa.Lakini na huyo Ole Sendeka alikuwa wapi siku zote
aje aseme sasa?Au kwa kuwa ameshikwa pabaya?Mbona kile kipindi akimkomalia Edward Lowassa
hakusema ni la kihuni?
 
Mule ndani Pinda ndiyo anaongoza kwa uhuni. What do you expect for the rest!!!?. Haiwezekani ahalalishe Zanzibar iendeshwe kidini, kwa kuruhusu serekali ya Zanzibar kufunga hoteli na migahawa yote visiwani. Mtu atakayeonekana anakula hadharani akamatwe na police. Waislamu wa Zanzibar ni muhimu kuliko wa Bara?? Shame on Pinda. Huu ni uhuni. Na kama hajuwi kwa uhuni wake huo ana-instigate waisilamu wa Bara kudai haki kama wanayopewa wenzao Visiwani. Itakuwa ni haki yao. Wote ni waislamu, kwa nini wa Visiwani wawe special kuliko wa Bara!! Shame on Pinda. Usiniambie swala la mazingira ya Visiwani. Kama mnajuwa mazingira ya Visiwani hayawezi ku-match na mazingira ya Bara, kwanini unang'ang'ania muungano? Kwani mazingira ni kitu gani kwanza!!! Mazingira utakayonieleza umeyajenga wewe mwenyewe kwa uhuni wako na akili zako fupi, kama ambavyo unaendelea kuyajenga. Hii ni aibu kwako na kiongozi aliyekupa dhamana ambayo huiwezi. Hata siku ile uliposimama bungeni kumpinga Msigwa, ulianza kutafuna maneno na macho yako yalionyesha dhahiri shahiri unafiki na uhuni wako. Pinda unatuharibia nchi!!!!. Nasema tena, Pinda utataabisha wajukuu zangu kwa uhuni wako. Wewe Sendeka ni brach ya wahuni toka katika shina kuu la uhuni humo Bungeni. Unajuwa uhuni ulioufanya unakuelekeza kwenye kaburi la kisiasa. Sasa unataka ufe na wengi ili lile neno la wahenga lipate kutimia "kifo cha wengi harusi". Niishie hapa maana naweza nikavunja monitor yangu.
 
Ameshindwa kufikiri.Amefilisika kisiasa.Kwani uchaguzi ukifanyika katika mfumo huu huu,na sheria hizi hizi ni kipi kitakachobadilika? Kinachotakiwa ni uchaguzi mpya chini ya tume huru ya uchaguzi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki
 
Huyu jamaa (Mh.Sendeka) asitake kupoteza ushahidi wa ufisadi wake. Yani uhuni wa BUNGE ndiyo anauona leo???
 
don't think of what ccm members never accept because if they try now they wll be putting themselves under bad situation.
 
Ameanza kuweweseka huyu kwa sababu anajua yeye ndio anawafanyia uhuni watz kwa kujifanya mpinga ufisadi wakati yeye mwenyewe ndiyo fisadi....anakwepa adhabu ya wananchi...sendeka akija kurudi tena bungeni ntawashangaa sana wana simanjiro
 
Kwani sheria zinasemaje iwapo rais atalivunja bunge?

ni uchaguzi kurudiwa ila mtu kama ole Sendeka ameshaona mbeleni hakuna njia ona maana 2015 harudi tene bungeni.Lisu kamwaga mboga dhidi yake sasa anamtaka rais amwage ugali.Kazi iko kweli kweli
 
Kwa kweli nimeangalia bunge na kugundua halina maana yoyote na haliisaidii au kuisimamia serikali.wabunge wako kishabiki zaidi wanaboa sana!

Halina maana hivyo livunjwe rasmi na tuitishe uchaguzi upya.

Kuanzia sasa upigaji wa kura bungeni uwe wazi na ijulikane nani alipiga kura ipi katika hoja iliyojadiliwa ili makosa yanapotokea mbeleni tuwahukumu waliohusika.

Update:
Mwananchi | July 13, 2011

Inshort Ole sendeka ndiyo amekosa mvuto anaameshajua kuwa maji yamefika shingoni na hata uchaguzi ukirudiwa leo hawezi tena kupata ndani ya CCM kwenye ameshajulikana kuwa yeye ni mtetea mafisadi na Jimboni This time atasimama na Kamanda Milya na yeye mwenyewe Sendeka kwa kauli yake akiwa Monjez B Arusha Kaloleni alikiri utawala wake kufika kikomo.
Bye Bye sendeka :israel:
 
Wanaojua sheria watusaidie kama inawezekana kutumia nguvu ya umma kuliondoa bunge madarakani
 
Back
Top Bottom