Bunge livunjwe kwa sababu limejaa wahuni - Ole Sendeka

Hawa wabunge wangeni wakishapiga bangi na tembo hawajui hata wanachokisema. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
 
KIKUPACHO RAHA NA UCHUNGU KITAKUAPA OLE SENDEKA ni mhuni numberr mmoja
ni mmoja kati ya wale waasisi wa CCJ na muwakilishi wa ccj ARUSHA na kwa sasa kashaona
chama chake kilichokuwa kinampa raha kimejaa wahuni na machanguu hawana mpya dodoma
zaidi ya kushangilia na kupiga makofi kuunga mkono hoja za kipumbafu zinazowakandamiza
wananchi zisizo na masilahi kwa wananchi kwa kuwa tu wao na familia zao na mahawara wao
wanapata matibabu nje ya nchi ,wanakuja na hoja za kifisadi na za kula kodi za watanzani
eti BAJAJI GARI ZA WAGONJWA? kweli kweli bajaji inawezaje kumtoa mama mjamzito kapata
uchungu wa kujifungu usiku wa manane sehemu ambayo kuna milima na bara bara mbovu na mvua
utelezi au zina 4WD acheni kuwatania watanzania kuna wahindi wamechonga dilli ya kutuuzia huo uchafu
wa bajaji ni 4bilion unaweza kupata magari yenye 4WD KAMA 200 HAYA na tusubiri tuone wahuni wa OLE
SENDEKA mpambanaji wa zamani wa ufisadi aliyesajilliwa kwenye ufisadi na kuwa papa wa ufisadi TZ tunasema

KIKUPACHO RAHA NA UCHUNGU KITAKUPA
 
Posho, kulala, kula, wanawake malaya, magonjwa, rushwa, unafiki, umaskini kwa watanzania.

Je tunategemea nini zaidi?
 
Naunga mkono hoja.Wavaa vidani wamo humo,watoto wa mipasho,akina Sugu,akina Vicky,mashoga,wasagaji,akina Berlusconi nk.. Hapana,kweli bunge letu la wahuni,livunjwe.Hatuwezi kufika popote na watu hao.Huwa mimi najiuliza sana,hivi tumefikaje hapo?

Hii kali!
inawezekana vipi? Wananchi hawakujua wasifu wa wawakilishi wao?!
 
Wabunge wote wa sisiem ni wahuni kisiasa. Tumechoka. Ndioooooo bungeni kama maroboti na midomo yao kupuuza mustakabari wa maisha ya watanzania. Tumechoka na ujinga wenu.
 
Mnakaa mnashadadia sisiem fuateni maoni ya werema na yule aliejivua gamba jana saa sita mchana, utajua wahuni ni wao wenyewe kijani na njano.
 
WanaJF hapa mmeniacha uhuni unaozungumziwa ni upi? kama ni wa mtu binafsi je waliomchagua/waliomteua hawakujua? sasa yupi ni muhuni hapo? katika mabunge yaliopita ambayo yalikuwa na wapinzani wachache hayakuwepo haya? Je wabunge wapinzani hawakudhalilishwa kutokana na uchache wao? Au kwa kuwa sasa wapinzani ni wengi kiasi na sauti zao zinasisika kidogo ndio tuuite uhuni? Mbona mabunge mengi tu duniani wanachapana hadi makonde??? Hii ya Ole si Hoja ya msingi inayoweza kuvunja Bunge
 
Kweli bunge limejaa wahuni wengi sana! Sugu, Wenje, Lema na wengine

kujaa ni ujazo haiwezi kuwa uchache. 3 kati ya zaidi ya 200 haiwezi kuwa kujaa.
kama angemaanisha hao baadhi angesema bunge lina wahuni wachache, lakini amesema limejaa. tafakari vizuri kabla ya kudandia.
 
Sendeka apewe likizo akaimalizie House of Commons Uingereza ajifunze - tuone kama atatoa hoja yake tata hii.
 
TUCTA Mwanza wataka ‘Bunge la posho' livunjwe

UONGOZI wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), mkoani Mwanza, umetoa kauli nziti ukitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano kuvunjwa kwa maelezo kwamba limeshindwa kusimamia na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Umma.

TUCTA_Mz1-250x187.jpg


Katibu wa TUCTA Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Mwendwa

Katika kauli yake Jumatano Januari 18, 2012, Katibu wa TUCTA Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Mwendwa alipendekeza Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge kwani sasa limegeuka kuwa kinara wa kuidhinisha matumizi makubwa ikiwa ni pamoja na posho kubwa kwao na kwa vigogo Serikalini.

Mwendwa amesema Wabunge wa Bunge la sasa wanaonekana kujali zaidi maslahi yao binafsi, badala ya Watanzania na maendeleo ya taifa kwa ujumla, hivyo chombo hicho kimepoteza sifa ya kuwa mhimili mkuu wa nchi.

Kiongozi huyo amesema Bunge limeonekana kushindwa kabisa kuisimamia Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo Rais hana budi kulivunja na kuitisha Uchaguzi mwingine.

Hata hivyo, utaratibu uvunjwaji wa Bunge ni mgumu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, utaratibu ambao unaigharimu hata serikali na Rais mwenyewe.

Kwa mujibu wa Mwendwa, wabunge wengi waliopo bungeni wanaonekana kuwa na lengo la kuwatalawa wananchi wao, na si kuwahudumia na kuwasilisha mawazo yao katika chombo hicho, na kwamba wamekuwa vinara wakubwa wa kuidhinisha matumizi makubwa ya posho zao na vigogo wengine waliopo katika taasisi na Wizara mbali mbali.

"Tanzania ya leo ipo kwenye wakati mbaya sana. Bunge limeshindwa kabisa kuisimamia Serikali juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma, badala yake limegeuka kuwa chombo cha kuidhinisha matumizi makubwa posho zao na vigogo wengine Serikalini.

"Wabunge wengi wanaonekana wapo kwa ajili ya maslahi yao bungeni. Hawawajali kabisa wananchi waliowachagua….hivyo tunamuomba sana Rais Kikwete ni bora alivunje hili Bunge maana Watanzania hawatapona kwa mtindo huu wa posho ya 200,000″, alisema Katibu huyo wa TUCTA Mkoa wa Mwanza.

Mwendwa ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), Kanda ya Ziwa alikwenda mbali zaidi na kusema: "Kwa sasa Bunge linaonekana kumtumikia kafiri ndiyo maana wameshindwa kuidhibiti Serikali kwa sababu nao wanajali zaidi maslahi yao binafsi".

Alisema, wapo baadhi ya wabunge ni wajumbe wa bodi za taasisi au idara fulani zaidi ya tano, na kwamba kwa hali hiyo wamekuwa wakiwaza vikao tu ili walipane posho, na alitoa angalizo kwa wabunge kuacha mara moja kujipendelea wao wenyewe, bali waishinikize serikali iwalipe mishahara stahili watumishi wa Serikali na si kama ilivyo hivi sasa.

Mwendwa anasema nchi yoyote duniani ikizungukwa na wezi kamwe wananchi wala taifa halitapata maendeleo, na kwamba inavyoonekana hata serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo taifa la Tanzania linakabiliwa na ombwe la uongozi na inatakiwa Katiba mpya haraka iwezekanavyo.

Aliitaka pia Serikali kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake, ikiwa ni pamoja na kuwaongezea mishahara na marupurupu, na kusema madaktati, walimu, askari polisi, watumishi wa kawaida na hata maofisa kilimo na mifufugo wanalipwa ujira kidogo sana ikilinganishwa na kazi kubwa wanazozifanya kila siku.



Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – Mwanza.

http://www.fikrapevu.com/habari/tucta-mwanza-wataka-bunge-livunjwe-kwa-kuendekeza-posho
 
Tanzania tumeingia katika aibu ya Dunia

Nchi inadaiwa sana, nchi ni omba omba.

Uchumi umedorara, mfumuko wa bei

Watanzania wanazidi kuwa masikini

ufisadi unafanyika mchana kweupe, mafisadi hawachukuliwi hatua.

Wafanya kazi ambao ni kada muhimu katika uzalishaji na huduma za jamii hawathaminiwi, badala yake wabunge wanakula keki yote ya taifa
wabunge wanabariki ufisadi, wabunge ni wabinafsi, wabunge wana miliki biashara na wanakwepa kodi

wabunge na mawaziri ni wafanyabiashara na wanapandisha bei ya mafuta


MGOMO WA MADAKTARI

MADAI YA MADAKTARI NI YA HAKI NA NI KWA AJILI YETU SOTE WANANCHI WALALAHOI

WABUNGE NA MAWAZIRI WAO WANATIBIWA NJE YA NCHI KWA KODI ZA WANANCHI

NDO MAANA WABUNGE NA MAWAZIRI WANAPUUZA MADAI YA MADAKTARI.

MADAKTARI WANATAKA VITENDEA KAZI ILI WANANCHI TUPATE HUDUMA BORA ZA AFYA

MADAKTARI WANADAI MASLAHI BORA ILI WATOE HUDUMA AKILI ZAO ZIKIWA TULIVU KWA FAIDA YETU.

WATANZANIA SHIME TUAMKE, HASA VIJANA TUAMKE.

VIJANA TUHAMASISHANE NA TUINGIE BARABARANI KUDAI HAKI ZETU.

TUTUMIE MAWASILIANO YA FACEBOOK NA SIMU,
 
NAUNGA MKONO, wabunge posho zenu kubwa kuliko madaktari kwa nini au mmesoma sana kuongea na kulala Bungeni?
 
Fikra za kimasaburi hizi "Bunge livunjwe, Rais ajiuzulu na Waziri mkuu awajibishwe".... hawa wameshaambiwa atakayeendelea kugoma atakuwa amejifukuzisha kazi.... wewe analeta upupu hapa! Hivi unajua madhala ya haya unayotaka yatendeke?
 
Kama hawatakuTISS kwa mada yako hii. Kuingia kwenu barabarani ndio kutaondoa matatizo?
 
Fikra za kimasaburi hizi "Bunge livunjwe, Rais ajiuzulu na Waziri mkuu awajibishwe".... hawa wameshaambiwa atakayeendelea kugoma atakuwa amejifukuzisha kazi.... wewe analeta upupu hapa! Hivi unajua madhala ya haya unayotaka yatendeke?
nahisi wewe ni mmoja wa washauri wa pinda
 
Back
Top Bottom