Bunge letu na mahudhurio ya aibu!

Yah jana ata nami nilikereka kweli bse of poor attendence mbaya zaidi mahundhurio hayo hayo yalipitisha budget ya wizara ya viwanda na biashara.
Ivi allowance hawapewi kutokana na mahudhurio?
 
Naomba msaada,

Wakihudhuria tunapata nini? na wasipohudhuria tunapata?

Wakihudhuria - wanajustify "sitting allowance"

Wasipohudhuria - wanapata "allowance" mbili : "sitting allowance" na "walking allowance"

see - abseentism cost us more.
 
Mkuu hasara niya kwetu sote Watanzania. Tena nasikia baada ya bunge hili kuvunjwa ( ijumaa 16 Julai) itaanza kufanyika renovation kubwa mno na kuongeza viti zaidi ili kulifanya bunge lijalo liwe kubwa zaidi. Ama kweli nchi inaliwa! tena na wateule wachache>
 
Na kinachouma zaidi no one cares, si PM wala Spika wa kukemea hali hii, kwanini basi PM akazanie kuwafukuza kazi ma DED kwa matumizi mabaya ya mali ya umma anaacha hata kukemea hali hii wakati ni matumizi mabaya yale yale, au mishahara ya wabunge haitoki hazina.

Wengi tunaangalia utoro wa wabunge tu lakini tuangalie pia who is responsible, nafikiri PM na Spika ni viongozi wa shughuri zote za bunge, wakiwa wakali mfano mbunge yeyote atakayekosa kuhudhulia kikao bila ruhusa maalum anapata barua ya warning au hata karipio la mdomo nafikiri next time mbunge huyo kabla ya kutoroka atafikiria mara mbilimbili, tuna mifano mizuri kama mwalimu asipokuwa responsible kumhimiza mwanafunzi kuhudhulia vipindi darasani mwanafunzi atachukulia kama jambo la kawaida na hatajali, matokeo yake ni mwanafunzi kufeli na mwalim kupoteza credibility yake inagawa ataendelea kupokea mshahara.

Kama mleta hoja anavyosema zaidi ya 75% ya wabunge hawakuwepo ina maana zaidi ya wabunge 150 hawakuhudhulia kikao na sidhani kama wote walikuwa wameomba ruhusa, na iwapo walikuwa na ruhusa tatizo litakuwa kwenye kanuni za utaratibu wa uendeshaji wa Bunge kuwapa ruhusa wabunge wengi kwa wakati mmoja hasa siku muhimu ya bunge la bajeti ya serikali.
 
Huwa aghalabu naangalia LIVE broadcast ya sessions za bunge letu 'tukufu' kama linavyorushwa na TBC 1 kwa sababu nimechoshwa na maigizo yanayofanyika hapo bungeni. Jana 'kwa bahati mbaya' nili-tune TBC 1 na kuona kituko....nashukuru Mungu sina historia ya matatizo ya ugonjwa wa moyo otherwise ningepata mshtuko wa moyo na kupoteza fahamu!!! Naweza ku-estimate yale mahudhurio kwamba yalikuwa ni robo au chini kidogo ya hapo (20-25%). inauma sana ndugu zangu watanzania!!! ni lini tutakuwa serious na mambo ya msingi kwa taifa hili? ni eneo lipi tupo serious? naomba nitumie maneno haya yanayoonekana kama mepesi lakini naomba nieleweke kwamba 'niliumia sana'!!!

hivi column ya bunge ni ngapi kwa bunge ku-proceed? Jana ilijadiliwa na kupitishwa bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na masoko, je kikanuni ni halali basing on that column?

je, inawezekana sherehe za mkwere kurudisha fomu ndio zimesababisha hilo? kama ni kweli,je huko sio ku-subotage kazi ya bunge? kwa nini vikao vya chama na shughuli kama hizo za chama zisifanyike nje ya muda wa bunge, mathalani weekend? yet you want me to believe you that you push us towards the dvelopment rather pulling us back?

TBC 1 ipo ndani ya dstv hivyo inaonekana nje ya tanzania, je huko si ku-publicize ujinga wetu?

Lakini posho zinaendelea kila siku kuvilipa viti tupu? Hata mimi nilipomwona Komba akijikomba kumfagilia Jk nikashangaa! Kumbe priority za wabunge ni sifa za kujikoki kwa wakubwa zao lakini sio za nchi na wala sio kwa wapiga kura wao?
 
Siku zao zinahesabika Watanzania hawatakuja kuwa wajinga siku zote,hawana uzalendo kabisa wanapokea posho bure kazi kunenepeana matumbo na ****** tuu, hawana maana kabisa wakufukuza wote kasoro wale tunao wajua wanaotumikia Wananchi na Bunge kwa ukamilifu
 
Kilembwe uko sahihi wawepo wasiwepo we have nothing to loose nor gain.
 
Wamesema sababu ya bunge kuwa tupu ni kutokana na Kikwete kurudisha fomu za kugombea urais.Bunge halina maana kwao sasa hivi wana focus kwenye uchaguzi zaidi.

mbaya zaidi uchelewi ukakuta posho wamepewa kwa hizo siku walizo kosa.
 
wadau,
Hebu tujadili hili. Asubuhi nilipowasha TV wakati bunge linaanza wabnge walikuwepo kidogo mno?Jee, ni kweli kwamba wasiwasi wa kutorudi tena mjengoni kunawafanya wasitulie na kuhaha huku na kule na kutugawia simu, baiskeli na pikipiki huku majimboni?Jee?hakuna kanuni inayotaka mahudhurio yawe kiasi kadhaa?
Naomba kuasilisha.
 
wadau,
Hebu tujadili hili. Asubuhi nilipowasha TV wakati bunge linaanza wabnge walikuwepo kidogo mno?Jee, ni kweli kwamba wasiwasi wa kutorudi tena mjengoni kunawafanya wasitulie na kuhaha huku na kule na kutugawia simu, baiskeli na pikipiki huku majimboni?Jee?hakuna kanuni inayotaka mahudhurio yawe kiasi kadhaa?
Naomba kuasilisha.


Hii mada ilisha wasiliswa humu siku nyingi. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/66109-bunge-letu-na-mahudhurio-ya-aibu.html
 
Kuna masuala mawili hapa kuhudhuria Bungeni na idabi ya wabunge.

Tatizo la kwanza kabla hatujadili kuhudhuria kwao naona tujadili ni kitu gani muhimu wanachoongea wakiwa bungeni, kule ni pumba tupu nikiwa PM leo , afadhali kuwapa wabunge Deskpots za bei poa na kutafuta ISP rahisi ili mijadala ya bunge isiwe expensive wapitishe miswada kwa e-mail na chochote wanachofanya kwa e mail wasilipwe allowance yoyote ile.

Hivyo mmjejiuliza wale wadau mashururi wanaokwenda Dodoma na kufadhili matamasha na kuwafanya wabunge wawe wanaonekana, mara meechi za mpira, mara marathon mara dansi mbona kikao hiki wako kimya?? Kwa kweli mahudhurio yao yanajikita kenye maslahi ya fweza bwana ndo maana hutuwaoni.

Idadi ya wabunge hili ni suala lingine la msingi sana, tuna wabinge wengi sana lakini hawana tija, idadi ya viti vya wabunge inaongezeka bila sababu. Viti maalum vya wanawake walioweka walikuwa na sababu lakini sisi tunaharibu. Kuliko kuchaguliwa na vyama kwa nini wasihaguliwe akina mama wa vijijini ambao hawana itikadi kabisa na ambao ndio wanajua matatizo yao wenyewe kuliko kuchukua watu wanouza sura zao bungeni?

Kama kuna mtu ana picha za wabunge wa miaka ya sabini alete picha zao hapa ili tulinganishe na wa sasa.

Kwa kweli, Hela wanazolipwa wabunge wa viti maalumu kwa vyama vyote kama zingepelekwa kwa akimama wenye shida ingeleta tofaiti kubwa sana.
 
Tatizo la Bunge letu ndiyo tatizo la nchi yetu nzima. Sheria zipo lakini hazi tekelezwi. Kuna sheria kwamba mbunge asipo hudhuria bunge lazima atoe taarifa kwa spika. Kuna sheria ya idadi mbunge anazo ruhusiwa kukosa kabla haja fukuzwa. Kuna sheria zinazo sema idadi gani ya wabunge wana hitajika kufanya shughuli zipi. Sheria hizo zote zipo! Tatizo ndiyo hilo tu kwamba hamna anaye jali.
 
Sherehe za kurudisha FORM ndiyo sababu cha "EMPTY SEATS" ndani ya Jengo la Bunge la JMT!

You wonder ni sherehe ngapi zitafanyika mpaka JK atakapoapishwa tena kuwa RAIS

- Kuchukua Form sherehe
- Kurudisha Form sherehe
- "Kuvunja bunge" sherehe
- Kupitishwa "Jina la mgombea U-rais" sherehe
- Kutangazwa ushindi wa "Kishindo" sherehe
- Kuapishwa kuwa RAIS sherehe

umesahau
-mtoto kupata uwakili sherehe kubwa Ikulu
 
Do.jpg

East African Cooperation minister Samuel Sitta (front row) &
deputy Finance minister Gregory Teu clearly
the only ones in the Government section of the National Assembly Hall
at one point during yesterday`s morning session of the august assembly in Dodoma yesterday.

ZAIDI ya nusu ya wabunge wote 357 wanaotambuliwa kikatiba katika Bunge la Tanzania jana hawakuhudhuria bungeni na viti vingi vilikuwa wazi.Takwimu zilizochukuliwa na gazeti hili saa 5:40 asubuhi, zilionyesha kuwa ni wabunge 58 tu waliokuwapo.

Kwa mahesabu ya haraka, idadi ya wabunge waliokuwapo ni sawa na asilimia 16.2.Kama kanuni za Bunge zingekuwa zinazingatia kuwa ili kikao kiendelee ni lazima kuwa na nusu ya wabunge wote, kikoa cha jana kisingefanyika.Taarifa zilizopatikana zilisema wabunge wengi waliondoka Jumatano jioni, kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Sabasaba juzi.

Kwa sababu hiyo, baadhi yao hawakurejea Dodoma kuendelea na mkutano wa 20 wa Bunge uliofanyika jana.Badala yake waliamua kuunganisha moja kwa moja na siku za mapumziko wa mwisho wa wiki (leo na kesho).
Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili, walisema ingekuwa ni suala la kuzingatia kuwa ni lazima zaidi ya nusu wahudhurie, basi kikao cha jana kisingefanyika.

Kulingana na kanuni za kudumu za Bunge, toleo la 2007, kanuni ya 77(1) kuhusu uhalali wa shughuli za Bunge, uamuzi wowote wa Bunge ni lazima upitishwe na nusu ya idadi ya wabunge waliohudhuria.

Kipengele hicho kinasema: "Akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanya maamuzi itakuwa ni nusu ya wabunge wote."Lakini katika kifungu cha pili, kanuni hizo zinaeleza mbunge anaweza kumjulisha spika kwamba wabunge waliopo ni pungufu ya akidi inayohitajkika kwa ajili ya shughuli inayoendelea.

Vile vile inaeleza kwamba hoja ya mbunge itategemea uamuzi wa spika, iwapo ataridhika kwamba idadi ya wabunge waliopo hawakidhi mahitaji ya kuamua mambo muhimu.
 
Kwa mazoea haya ikitokea siku Spika amebakiwa na wabunge watano ukumbini ataendesha kikao
 
Kwa mazoea haya ikitokea siku Spika amebakiwa na wabunge watano ukumbini ataendesha kikao
"Akidi kwakila kikao cha Bunge wakati wakufanya maamuzi itakuwa ni nusu yawabunge wote."Napenda kufahamu kwamba kulikuwa na maamuzi gani ya kufanya kulingana na Kanuni ya 77 (1) maana naona kuna maneno "wakati wa kufanya maamuzi?"
 
Kuvunja kwa makusudi kanuni za bunge ni kosa la jinai kuanzia leo. Na wahusika wote wapigwe risasi hadharani. Order.

FaizaFoxy.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom