Bunge letu na mahudhurio ya aibu!

kama unachaguliwa maneno ya kuongea, na kuendeshwa kibabae kuna haja gani ya kuudhuria, bora wafanye hivyo tuu
 
tatizo litaisha lini, mpk mkutano huu bado maudhurio ni hafifu
 
Nimekuwa mfatiliaji wa bunge letu la tanzania kwa muda mrefu. Kuna kitu ambacho nimejiuliza bila kupata jibu. Kuna kipindi unakuta zaidi ya asilimia 75 ya viti vikiwa vitupu(havina wakaaji ambao ndio wabunge tuliowachagua) na zaidi ya hapo unakuta baadhi yao walifika asubuhi kusaini. Sasa je hakuna sheria inayoongoza kuhusu mahudhurio ya wabunge? Na je mda huo hawa wabunge wanakuwa wapi na wanawawakilisha vipi wananchi? Je kwa hao wanaosaini bila kuhudhuria si matumizi mabaya ya kodi za watanzania?

Naomba kujuzwa na pia nawakilisha. Tuache ushabiki wa kivyama
 
Back
Top Bottom